TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS hawawezi kukwepa lawama za utekaji na kazi hii waliianza tangu walipojaribu kumuua Dr Ulimboka bila mafanikio.
 
Mkuu kama TISS hawajitokezi kukanusha, ni wazi kwamba wao ndio wanahusika na utekaji, utesaji na uuaji.
 
Mbona povu? Ni lazima watekwe watanzania wote milion 50 ndipo uamini kwamba TISS wanateka watu? Hebu tuambie basi ni nani aliyewateka Dr Ulimboka, Absalom Kibanda, Roma na raia wengine wanaotekwa kila kukicha badala ya kutoa povu kavu pasipo maelezo mubashara. Pia usisahau kutuambia yule pimbi aliyemtolea Nape Bastola mchana kweupe ni nani na alitumwa na nani.
 
Kuna mtu aliniambia kwamba 80% ya maongezi ya vijana wa kitanzania ni pu.mba. Sasa nimeanza kuamini hilo kupitia comments zinazotolewa na vijana kwenye mijadala kuntu kama huu hapa. Mtu anaibuka kutoka kusikojulikana anakuja hapa kutetea wauaji pasipo sababu za msingi. Ama kweli viroba vimeharibu vijana wetu kwa kiasi kikubwa sana!
 
You have suggested to reduce their number....would you help us to tell how many are they? So that we decide to reduce them or increase the number of maintain it?
 
Kwa hiyo miaka yote tangu ianzishwe, ndio leo mnatuambia kazi yao ndio hiyo!? Mbona malalamiko juu yake ni siku hizi na sio tangu!?
Hata mimi nimemsoma na nimejiuliza mambo mengi sana, tatizo ni Nape!!!, hao TISS wanaoelezwa kuwa wanatesa watu uko Clouds waliteswa? walipigwa? Pasco anayo ajenda, awe wazi katika ajenda yake.
Pasco amezunguka zunguka lakini anayo ajenda.
 
umeona eh........ kama kisheria (yao ya kazi) wanaruhusiwa hata kumbana mtu korodani kwa praizi.... ili mradi wapate wanachokitaka..............how comes tunawahukumu??
Mkuu hapa tunaongelea utekaji, utesaji na mauaji....na hili sio moja ya majukumu ya TISS (usalama wa CCM). Umeelewa sasa?
 
Mkuu hapa tunaongelea utekaji, utesaji na mauaji....na hili sio moja ya majukumu ya TISS (usalama wa CCM). Umeelewa sasa?
Nilielewa kilichokuwa kinaongelewa na ndio maana nikaomba kujuzwa majukumu yao ya kazi ni yepi. Nimekwishaeleweshwa
 
TISS hawawezi kukwepa lawama za utekaji na kazi hii waliianza tangu walipojaribu kumuua Dr Ulimboka bila mafanikio.
Mkuu T Paul, TISS ni professionals, watu ambao ni ma professional hawafanyi kazi nusu nusu, they do a complete job, hivyo kwa Dr. Ulimboka hawakujaribu kumuua bila mafanikio bali lengo halikuwa kumuua bali kumpatia tuu ujumbe fulani ambao ulifika na kamwe hutakaa usikie mgomo mwingine wowote wa madaktari nchini na hutakaa msikie Ulimboka aliambiwa nini na watesi wake!.

Lengo lingekuwa ni kumuua, saa hizi hata unywele usingeonekana!.

Hawa jamaa wakiamua kufanya mambo yao wanafanya tuu na haijalishi ni nani!. Hebu msome huyu jamaa wa TISS humu JF kwenye uzi huu angalia jinsi roho ya mtu ilivyopotezewa na sababu zilizotolewa!.
Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

Political Assassins: Why TZ Politicians Must live in a State of Perpertual Paranoia

Angalizo UKAWA: Acheni hii Dilly Dallying Kutangaza Jina la Mgombea wenu! Toeni Jina, Vinginevyo...!

Wakuu tukumbushane vifo hivi & kuumwa:walidai haki za Watanzania

Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?

Paskali
 
Mkuu kama TISS hawajitokezi kukanusha, ni wazi kwamba wao ndio wanahusika na utekaji, utesaji na uuaji.
Protocol haziruhusu,wanakufa na tai shingoni.Lakini wao kwa wao na taasisi nyingine zenye mawasiliano mmoja kwa mmoja wanazungumza kwa mipaka ya kazi zao,nafasi zao na majukumu yao.Ni nadra sana kwa taasisi hiyo kujilipua wazi wazi.Yupo mtu mmoja aliwahi kusema mkewe aliishi nae miaka zaidi ya 30 asijue kuwa ni afisa kachero gwiji hadi anastaafu,na alivyogunduliwa alikanusha na kumkana mtu mmoja aliemtambua kuwa ni mwenzao.
 
Mkuu Paskali kwanza pole sana.

Naunga mkono hoja yako, watendaji na utendaji wa TISS unajadilika na ni muda sahihi tuujadili na kuupatia ufumbuzi.
 
Kujifanya unaifaham sana hiyo TISS kisa babaako alikuamo ni kujidanganya, hata angekuwa mkeo hutopata cha maana kutoka kwake, chamcngi acha tu wehu maana unaonekana kujifanya mjuzi kumbe mbumbu wakutupwa...Jina lako kikwetu ni njaa na umesadifu
 
Nyani Ngabu,
Mkuu hawa jamaa wanatukanwa sana maana hawana pakusemea, hao kina Roma, Mnafiki Zitto na Lilia Nape wana pakusemea ndio maana hawaishi kutukana, ila hawa jamaa wakiamua kufanya hivyo hata hakuna wakujua hilo hawa wehu wanatafuta kiki tu
 
Retired,
Mkuu kwanza asante kunifuatilia tangu vipindi vyangu hadi michango yangu, humu jf hadi kunidhania ni knowledgeable na influential.
Jee yanayofanyika ninayaona?. Yanayowahusu wamenyamaza na mimi nimenyamaza kwa sababu baadhi yao ni ma homeboy wangu!.

Hao wote uliowataja na yote uliyoyataja kwao they are nothing.
Kwa upande wangu, kwanza mwisho wa uwezo wangu ni kuandika tuu na kupaaza sauti. La kuhusu vyeti vya Bashite nililizungumza mapema hata kabla ya Gwajima.

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya sheria na haki, hivyo hata Bashite naye ana haki zake lazima ziheshimiwe, nikiwa ni mwana Kolomije, ikatokea homeboy wako anatuhumiwa kwa tuhuma za uongo, kwanza nikaitisha wana Kolomije wote kujitokeza kumtetea homeboy wetu

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia...

Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .

Kwenye uvamizi wa Clouds pia niliongea
Insane Anahitaji Huruma, Kusaidiwa. Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa na Kususwa! He Needs Help, Tumsaidieje?

Pamoja na yote lazima nikiri udhaifu wangu ni kuwa very frankly kwa kuwa mkweli too much kwenye jamii ambayo uongo, fitna na majungu ni mtaji hivyo kuwa an enemy of the people.

Mimi nimetanguliza mbele maslahi ya taifa na sio maslahi ya u homeboy!.

Paskali
 
Yaliyotokea Clouds TV wote tumeyashuhudia kupitia CCTV, na yale makirikiri tumeyaona, na ya Nape Mnauye tumeyashuhudia live mubashara kwenye TV huku huyo mpuuzi akionekana wazi hadi sura watu wanamjua.

Pamoja na porojo zote ulizoandika, na huko kujifanya unazijua kazi za TISS kana kwamba utesaji ndio kazi yao. Nikwambie tu kitu kimoja, hakuna CCTV iliyoonyesha tuhuma anazotuhumiwa Mh. Paul Makonda kuhusu Clouds. Otherwise kama unayo nyingine tofauti na iliyosambaa mitandaoni. Ila kama unarefer ile footage, basi bila shaka hata wewe una kiwango cha chini cha uelewa na pengine unaendeshwa na mihemuko ya siasa ndio maana unakimbilia hata kuituhumu idara nyeti kama TISS kwenye vitendo vya kidhalimu kama hivyo. Halafu eti unasema TISS wajisafishe, mhh hivi ni tangu lini umeona TISS wakiongea kwenye public?

Ni lini TISS wameanza kuzungumzia information zao hadharani? Huyo Tundu Lissu unayemuamini je alithibitisha kwamba aliyefanya hivyo vitendo viovu ni mtu wa TISS? Na kama alithibitisha je ametumia utaratibu gani unaokubarika kisheria kuweza kutoa malalamiko kuhusu vitendo hivyo? Kitendo cha yeye Lissu kuongea hadharani na kuwataja TISS kuhusika na hivyo vitendo, au mtu wa TISS kuhusika na hivyo vitendo je haoni kama anavunja sheria ya usalama wa taifa, THE TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICE ACT, 1996? Kama anaijua hii sheria vinzuri na akaamua kuivunja kwa maksudi kwa nini tusiseme lengo lake ni kutafuta mtaji wa kisiasa kwa kuichafua idara nyeti na muhimu katika usalama wa taifa hili? Hebu watanzania tufike mahali tuvae uzalendo na kuacha kuzichokonoa idara zisizotakiwa kuchokonolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…