TISS walibariki UJENZI wa GHOROFA linalotazama IKULU

TISS walibariki UJENZI wa GHOROFA linalotazama IKULU

Kwa taarifa yako ghorofa tatu za juu yaani 15-18 zimechukuliwa na Tiss .....kuna kitu kinaendelea .......tu ute subra kuna jambo kubwa ndani yake ......kwanza kuijua jinsi Kiwanja kilivyodhulumiwa toka kwa yule Prof.wa Mwalimu utatumika sana .

naona wewe umeandika kwa hisia tu au unakumbuka mjadala wa wakati ule kuhusu jengo hili. kuna wadau walishauri kuwa TISS wachukue ghorofa zilizoongezeka kwa sababu za kiusalama. Nadhani wewe unachanganya pia hoja hii. Hapa tunajadili hawa jamaa wa TBA kupewa mlungula ili ghorofa ziongezeka kutoka 15 hadi 18
 
Kwa hiyo kwa akili yako TISS haiwezi kuingilia kati na kushauri usimamishaji wa jengo lolote linalotishia usalama kama lile la Magogoni?No wonder badala ya kufundisha mmekua wapiga debe wa Gaidi,kama hujui majukumu ya Usalama wa Taifa hata huo u DC unaotafuta kwa hamu haukufahi
Mkuu wewe uliyeusalama wa taifa tusaidie kutuelimisha acha kujifanya mkali mjinga nini tiss na majengo wapi na wapi make ile ni idara ya usalama wa taifa sasa mambo ya ujenzi yanaingiaje.
 
Chaburuma,
Kwa nini TISS hawakusimamisha ujenzi?
Mkuu, kama umeelewa vizuri, hapo kulikuwa na udanganyifu fulani. inawezekana pia kibali halali kilichopelekwa Ikulu ni kile cha ghorofa 15, ila TBA walitoa kibali cha ghorofa 18. kuhusu TISS kusimamisha ujenzi wa jengo hilo, daah hapo napata shida kukujibu. Sheria ya TISS inahusu kuzuia. likiharibika nadhani ni jukumu ya vyombo vingine kuchukua hatua. TISS wangepewa meno ya kuchukua hatua, ni wazi kuwa nchi hii ingenyooka sana
 
hapa kunamtu anataka kutolewa kafara,,,ngoja tuone mwisho wake nini??

haya mambo yakula pekeyako,,,,,mabaya sana....
 
Mkuu, kama umeelewa vizuri, hapo kulikuwa na udanganyifu fulani. inawezekana pia kibali halali kilichopelekwa Ikulu ni kile cha ghorofa 15, ila TBA walitoa kibali cha ghorofa 18. kuhusu TISS kusimamisha ujenzi wa jengo hilo, daah hapo napata shida kukujibu. Sheria ya TISS inahusu kuzuia. likiharibika nadhani ni jukumu ya vyombo vingine kuchukua hatua. TISS wangepewa meno ya kuchukua hatua, ni wazi kuwa nchi hii ingenyooka sana

Nielewavyo mimi TISS ndiyo taasisi yenye nguvu sana nchi hii....wanayo meno ila wameamua kuyapaka HINA
 
Mkuu wewe uliyeusalama wa taifa tusaidie kutuelimisha acha kujifanya mkali mjinga nini tiss na majengo wapi na wapi make ile ni idara ya usalama wa taifa sasa mambo ya ujenzi yanaingiaje.

Lilipoporomoka lile jengo kule uhindini TISS walienda kufanya nini kama hawahusiki na majengo? Au kwako wewe TISS ni ushushushu tu?
 
Kwani Jiji hakuna Master plan?, Tanzania kweli ni nchi ya ajabu kabisa, katikati ya jiji unakutana na nyumba za ghorofa tatu mpaka nne na ukigeuka unakutana na ghorofa ishirini, mji ni shagala baghala
 
kwani kuna majengo mangapi marefu yamejengwa na hayana vibali vya TISS? kwani sheria inasemaje kuhusu ujenzi karibu na ikulu?

Sio ikulu peke yake, hata karibu na makambi ya jeshi na maeneo mengine muhimu kwa usalama wa nchi. Rejea kubomolewa kwa jengo la Masaki lililokuwa karibu na kambi ya jeshi.
 
kwani tiss ni idara ya majengo na ujenzi? bado hamjanipa jibu.
ni umburura wa hali ya juu kuuliza swali la kijinga kama hili, kuna tatizo TISS wakiwa na hiyo idara? TISS ni taasisi ya usalama, hivyo wanaweza wakawa na idara zote unazozijua wewe,
 
Kwani TISS ndo wanatoa vibali vya ujenzi? acheni jamani kuleta propaganda kwenye mambo ya msingi.

Sio propaganda...ni utetezi wa mshtakiwa mahakamani...na amesema kuna ruhusa ya kimaandishi..........Ninachojiuliza mimi hadi jengo litaoteshwa kufikia ghorofa zote hizo walikua wapi? wangeweza kuzuia
 
Mkuu wewe uliyeusalama wa taifa tusaidie kutuelimisha acha kujifanya mkali mjinga nini tiss na majengo wapi na wapi make ile ni idara ya usalama wa taifa sasa mambo ya ujenzi yanaingiaje.

Usalama wa Taifa unaweza ingilia na kushauri usimamishaji wa kitu chochote kinachotishia usalama wa Taifa ikiwemo hilo jengo,hiyo haihitaji kuwa na degree hata ya Mtwara kama yako kujua,sasa mimi na wewe nani mjinga?
 
Naona kuna watu wanacheza ngoma wasioijua halafu kibaya zaidi ni viziwi mnaeleweshwa lakini hamuelewi vilaza kweli
 
Shhhhhhhh! Kesi ipo mahakamani. Au hapa ni chamber court?

Historia haiishiwi wino.
 
Back
Top Bottom