Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Ulaya na Marekani, Serikali inawajibika kwa wananchi ila Uarabuni na Urusi wananchi ndiyo wanawajibika kwa serikali. Matokeo yake Marekani na Ulaya inawezekana wananchi kuandamana kwa maelfu kupinga kinachofanywa na serikali na wasiuawe kwa kukukusudia.
Lakini kwenye nchi nyingi za Kiarabu na Urusi, wananchi wakiandamana ni lazima kwa kukusudia watauawa, kuteswa na kufungwa jela bila wakati mwingine kanuni za kisheria kufuatwa.
Marekani na ulaya watu wao wakiuawa vitani, wananchi wanataka kujua ni kwa nini ndugu zao wamepelekwa vitani. Kuanzia vita ya Vietnam, Operesheni ya Somalia, vita ya Ghuba na hata sasa ya Ukraine, wananchi wa ulaya wasiozipenda vita hizo, huandamana kuonesha hisia zao.
Fikiria kama Wanajeshi wa Urusi waliouawa zaidi ya 20,0000 ingekuwa wanajeshi hao ni Wamarekani ama wametoka kwenye nchi mojawapo wa ulaya. Unadhani wananchi wa nchi hizo wangekaa kimya?