Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
1632937720117.jpeg

Kati ya viongozi wa Uingereza waliowahi kunikatisha tamaa ni Tony Blair. Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1997 mpaka 2007.

Wakati akipata Uwaziri Mkuu, ndiye alikuwa kiongozi kijana kuliko wote kwa miaka 185 ya historia ya Uingereza, na alikuwa na miaka 44 tu.

Na alikuwa kiongozi wa chama cha Labour, chama ambacho nami nikiwa Uingereza nilikipigia kura nikiwa huko. Kwa ujumla vijana nchini Uingereza walimkubali sana.

Tony Blair aliongoza vizuri hadi baada ya 9/11 Marekani ilipopigwa World Trade Centre, New York.

Katika hasira na mchecheto wa kulipiza kisasi, Uingereza na Marekani ilibidi waunde maadui, maana hawakujua nani amewapiga.

Adui mmoja aliyesingiziwa ni Saddam Hussein wa Iraq. Huyu akatengenezewa uongo wa kutisha, ati ana silaha za kutisha zinazoweza kupiga hadi New York ndani ya dakika 45?

Na kwamba silaha hizo hazikai sehemu moja zinazungushwa zungushwa ndani ya Iraq ili zisifahamike ziko wapi.

Tony Blair alikuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuwa Saddam ana Weapons of Mass Destruction!

Kilichotushangaza wengi ni kuona uongo wa dhahiri ukipigiwa upatu, na tukajiuliza hivi kuna silaha mbaya na hatari kuliko za Nuclear ambazo wakubwa hawa wanazo?

Pamoja na mapingamixi toka mataifa mengi, Marekani na Uingereza walipitisha Azimio Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa, kuwa Saddam apigwe.

Saddam akapingwa na kuuwawa.

Pamoja nao wakauwawa wananchi wengi, wanawake na watoto. Iraq haikuwahi kuwa salama tena.

Mwisho wa siku ikaja dhihirika kuwa hapakuwa na silaha zozote za maangamizi Iraq. Waliouwawa waliuwawa bure.

Wale waaarabu walioipiga WTC-World Trade Centre, ikaja gundulika walitoka Saudia. Tony Blair na wenzake waligwaya kwa aibu!

Sasa huyu T Blair aliyesababisha vifo vya watu mamilioni wasio na hatia, yupo hapa kwetu, Ikulu. Sijafurahia sana kiongozi mwenye mikono ya damu kuwa mgeni wa Mama Samia.

Sijawahi kuona nchi za Ulaya na Marekani wakimwalika Mugabe(Zimbabwe), Idi Amin(Uganda) au Mengiste Haile Mariam (Ethiopia) huko kwao.

Mwana JF, mpe neno!

 
Nakumbuka kama si 2002 au 2003 kuna mkaguzi wa silaha za maangamizi alienda kukagua Iraq akaambulia patupu. Mwishowe tukasikia amejinyonga, sasa sijui alijinyonga kweli au walimfanyizia sijui.


Wakati huo USSR ndio imetoka kusambaratika, hivyo ilikuwa dhaifu sana.

Kimsingi Marekani na Uingereza hawakuwa na mpinzani wa kuwadhibiti.
 
Back
Top Bottom