Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

Pandora papers imeleta mtikisiko mkubwa kila kona ya dunia.
Vladimir Putin, Uhuru Kenyatta, Mama Ngina Kenyatta, Tony Blair, ... the list goes on.
 
Pandora papers imeleta mtikisiko mkubwa kila kona ya dunia.
Vladimir Putin, Uhuru Kenyatta, Mama Ngina Kenyatta, Tony Blair, ... the list goes on.
CC: MK254 weka neno lako brother.
Hali ipoje huko Nairobi?
 
Hii kitu inaitwa Pandora papers inaanza kuonesha ni watu wa aina gani tunaodhani wanastahili kutushauri. Blair na mkewe Cherie wametajwa kushiriki ujinga wa kukwepa kodi kwa kununua property offshore...
Kwao amehudumu kama waziri mkuu kwa vipindi vyake vyote, pia baada ya kuustafu hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kumfikisha mahakamani na kuhukumiwa kwa kosa la kutolipa kodi.

Sasa sisi tutamzuiaje mtu ambae si serikali wala mahakama yao ishathibitisha ukwepaji kodi wake?

Japo wengi wenu mmekabizi akili zenu kwa viongozi wenu, lkn muda mungine muwe mnatumia hata akili za kuazima kuandika kitu chochote kizito kama hiki
 
Nakumbuka kama si 2002 au 2003 kuna mkaguzi wa silaha za maangamizi alienda kukagua Iraq akaambulia patupu. Mwishowe tukasikia amejinyonga, sasa sijui alijinyonga kweli au walimfanyizia sijui.
Hans Bricks
 
Huyu ni mmoja wa washauri wa rais Samia, Vipi anafahamu kwamba Samia analeta DP world?
 

Kati ya viongozi wa Uingereza waliowahi kunikatisha tamaa ni Tony Blair. Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1997 mpaka 2007.

Wakati akipata Uwaziri Mkuu, ndiye alikuwa kiongozi kijana kuliko wote kwa miaka 185 ya historia ya Uingereza, na alikuwa na miaka 44 tu.

Na alikuwa kiongozi wa chama cha Labour, chama ambacho nami nikiwa Uingereza nilikipigia kura nikiwa huko. Kwa ujumla vijana nchini Uingereza walimkubali sana.

Tony Blair aliongoza vizuri hadi baada ya 9/11 Marekani ilipopigwa World Trade Centre, New York.

Katika hasira na mchecheto wa kulipiza kisasi, Uingereza na Marekani ilibidi waunde maadui, maana hawakujua nani amewapiga.

Adui mmoja aliyesingiziwa ni Saddam Hussein wa Iraq. Huyu akatengenezewa uongo wa kutisha, ati ana silaha za kutisha zinazoweza kupiga hadi New York ndani ya dakika 45?

Na kwamba silaha hizo hazikai sehemu moja zinazungushwa zungushwa ndani ya Iraq ili zisifahamike ziko wapi.

Tony Blair alikuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuwa Saddam ana Weapons of Mass Destruction!

Kilichotushangaza wengi ni kuona uongo wa dhahiri ukipigiwa upatu, na tukajiuliza hivi kuna silaha mbaya na hatari kuliko za Nuclear ambazo wakubwa hawa wanazo?

Pamoja na mapingamixi toka mataifa mengi, Marekani na Uingereza walipitisha Azimio Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa, kuwa Saddam apigwe.

Saddam akapingwa na kuuwawa.

Pamoja nao wakauwawa wananchi wengi, wanawake na watoto. Iraq haikuwahi kuwa salama tena.

Mwisho wa siku ikaja dhihirika kuwa hapakuwa na silaha zozote za maangamizi Iraq. Waliouwawa waliuwawa bure.

Wale waaarabu walioipiga WTC-World Trade Centre, ikaja gundulika walitoka Saudia. Tony Blair na wenzake waligwaya kwa aibu!

Sasa huyu T Blair aliyesababisha vifo vya watu mamilioni wasio na hatia, yupo hapa kwetu, Ikulu. Sijafurahia sana kiongozi mwenye mikono ya damu kuwa mgeni wa Mama Samia.

Sijawahi kuona nchi za Ulaya na Marekani wakimwalika Mugabe(Zimbabwe), Idi Amin(Uganda) au Mengiste Haile Mariam (Ethiopia) huko kwao.

Mwana JF, mpe neno!

Uzi wa 2021 kumbe.
Nilishituka nilifikiri huyu dalali wa ubeberu kaja kumuona tena samia. Unaona ukwasi wa samia umekua inadaiwa ni rais wa saba afrika kwa utaji. 2025 ifike haraka kabla hajaliangamiza taifa kwa mikataba ya ovyo.
 
wanajua kabisa africa kuna ulaji mzito na wanaelewa viongozi wetu wanawanyenyekea watu weupe eti uwekezaji ,uwekezaji upi huyo makinikia kwenda ulaya... je tusingekuwa na dhahabu, maziwa ,bahali na bunga za wanayama wazungu wasinge jikomba kwetu hata kidogo...
 
Huyu ni mmoja wa washauri wa rais Samia, Vipi anafahamu kwamba Samia analeta DP world?
Blair ndio alimshauri maana Blair ni dalali na pia ana hisa kwenye makampuni makubwa duniani

Ukiwa maarufu basi makampuni yote yanakuomba uingie kama mshauri au mwana hisa ili hata ukiona wamo viongozi wakubwa unakuwa na amani na hiyo kampuni

Kwa hiyo usishangae akawa ni mbia pia Dubai
 
Tony Blair sasa anafanya kazi ya kuwashauri (au kuwapotosha) watawala wa Afrika

He has been the executive chairman of the Tony Blair Institute for Global Change since 2016 and has made occasional "political interventions." .
 
Raia wote wanaotoka nchi za jumuia ya Madola wanaoishi UK wanaruhusiwa kupiga kura.
SI KWELI MKUU
May 25, 2023 — For UK Parliamentary elections you must be over the age of 18 to vote to vote. Obviously, British citizens in the UK can vote, ...
 
Tony Blair sasa anafanya kazi ya kuwashauri (au kuwapotosha) watawala wa Afrika

He has been the executive chairman of the Tony Blair Institute for Global Change since 2016 and has made occasional "political interventions." .
Tony Blair lazima ndiye mshauri wa haya madudu kama DP World!
Huyu jamaa hajalipwa kuleta machafuko nchini, ilimradi kaletewa cha kwake!
 
Back
Top Bottom