PETER THE ROCK
JF-Expert Member
- Feb 17, 2014
- 528
- 807
Kama kuna weledi wa uchambuzi kama huo nini kinawashinda kutoa maelezo Tony Blair anafuata nini Tanzania kumwona Rais wetu mpya mara ya pili. Matumizi bora kutatua matatizo mengi ya Tanzania ni muhimu kuliko kuonana na dalali. Tony Blair anaweza kutana na Balozi wetu Uingereza akawasilisha ujumbe wake ukamfikia Rais bila mbwembwe hizi za sasa. Msaidieni Rais wetu.Tukiangalia hivyo basi hakutokuwa na nchi kubwa duniani ambayo tutashirikiana nayo......
Pamoja na mh.Tony Blair kuwa na misimamo yake ile ....
Pamoja na washirika wake kuwa na misimamo yao ile.....
Ila.....
Kinachotuunganisha si misimamo yake "ile" bali ni haya:-
1)Tanzania Inaendelea kuwa nchi isiyofungamana na upande wowote....
2)Tanzania Inaendelea kuwa mshiriki wa mambo ya kidunia kwa kuangalia maslahi yake....maslahi jumuishi ya dunia kama mapambano dhidi ya "magonjwa ya mlipuko ,mabadiliko ya tabia nchi,makundi ya waasi wenye kuhatarisha utulivu na amani.
My take:
Pamoja na Tanzania kutaka nchi ya SAHARA MAGHARIBI iwe "huru" bado ni marafiki wa nchi ya MOROCCO......
Pamoja na Tanzania kutaka kuwaona Palestina wakiishi kwa utulivu kuliko ilivyo sasa ,bado tuna mahusiano ya kibalozi na ISRAEL....hili halikuwepo huko nyuma....haina maana tumekiuka miiko....dunia inabadilika.....misimamo inabadilika ...si sisi tu hata hao nchi za MAGHARIBI...Mathalani leo hii TALIBAN amegeuka kuwa "swahiba" wa Marekani baada ya kuwa naye vitani kwa miaka 20....wamarekani wameondoka Kabul tarehe 31/8/2021 na kusababisha nao MASWAHIBA ZAO(NATO) waondoke bila ya "kupenda sana"....je baada ya hayo hujasikia juzi UMOJA WA ULAYA(EU) ukitaka kuanzisha JESHI LAO LA PAMOJA LA KULINDA AMANI ?!!![emoji1787]
Umoja wa ulaya(EU) umeumia baada ya kutokuwa na uwezo wa kupeleka ASKARI 5000 kuulinda uwanja wa ndege wa Kabul pale walipokuwa wanawaondoa wakazi wa nchi za magharibi/washirika wao na raia waliokuwa wanaikimbia nchi yao....Je kwa hayo ndio UMOJA WA ULAYA wasiendelee kuwa washirika wa Marekani?!!!
Ushirikiano wowote ule hauna maana mnashirikiana vitu vyote.......
#SiempreSerikaliMbiliZaJamhuriYaMuunganoWaTanzania
#NchiKwanzaKablaYaNafsiZetu
Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app