Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbinu hii wanayoitumia imepitwa na wakati.Serikali chini ya CCM ni wajinga sana, yaani wametengeneza tatizo kisha wanalitatua ili ionekane serikali chini ya mama Samia ni sikivu, wajinga ndio waliwao wasifikiri watanzania ni wajinga kiasi hicho…
SafWaziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Agosti 31, 2021 ametia saini mabadiliko ya tozo za miamala ambapo serikali imepunguza 30% na makampuni ya simu Kupunguza 10% kutoka kwenye gharama za awali za ufanyaji wa miamala.
Sio wapunguze waitoe kabisaa,Wangepunguza 60% ikabaki 40% ingependeza zaidi.
Tafuta kitabu cha Mimi na Rais kutoka kwa Lello Mmasy, ameelezea sana kuhusu hili jambo.Serikali chini ya CCM ni wajinga sana, yaani wametengeneza tatizo kisha wanalitatua ili ionekane serikali chini ya mama Samia ni sikivu, wajinga ndio waliwao wasifikiri watanzania ni wajinga kiasi hicho…
Tumepunguza tozo ila tumeongezea kwenye mafuta yatapanda kuanzia Tarehe 1.Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Agosti 31, 2021 ametia saini mabadiliko ya tozo za miamala ambapo serikali imepunguza 30% na makampuni ya simu Kupunguza 10% kutoka kwenye gharama za awali za ufanyaji wa miamala.
Hii serikali isiyofuata sheria zake ni serikali ya ajabu sana; kama sheria ilipitishwa na Bunge iweje Waziri wa fedha aibadilishe kienyeji kwa maelekezo ya rais tu? Utaratibu ni kuwa atayarishe muswada mpya wa kuirekebisha na kuupeleka Bungeni. Halafu swala siyo kupunguza kodi tu, inabidi bajeti nzima ifanyiwe marekebisho, kwani bajeti hiyo pamoja na mambo mengine ilitegemea mapatao yatokanayo na kodi hiyo ya miamala.Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba Leo August 31,2021 ametia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021 na kupunguza viwango vya tozo za miamala kwa 30% huu ukiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia ambaye alielekeza tozo zipitiwe upya baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu tozo hizo.
Serikali pia imefanya majadiliano na watoa huduma za simu ambao na wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza katika miamala ya kutuma na kutoa fedha kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%.
Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa Tangazo la Serikali kesho September 01,2021 ambapo Serikali imesema inaamini uamuzi huo utatoa nafuu kwa Wananchi na kuiwezesha Serikali kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyokusudiwa wakati tozo hizo ziliporidhiwa na kupitishwa na Bunge la Bajeti la Mwaka 2021/2022.
#Kazi Iendelee.
Bwanku M Bwanku.
View attachment 1918384
Sheria imeweka tozo lakini haikutaja kiasi cha tozo, kanuni ndio zinazoweka viwango vya tozo, na waziri wa fwdha ana mamlaka kisheria ya kubadilisha kanuniHii serikali isiyofuata sheria zake ni serikali ya ajabu sana; kama sheria ilipitishwa na Bunge iweje Waziri wa fedha aibadilishe kienyeji kwa maelekezo ya rais tu? Utaratibu ni kuwa atayarishe muswada mpya wa kuirekebisha na kuupeleka Bungeni. Halafu swala siyo kupunguza kodi tu, inabidi bajeti nzima ifanyiwe marekebisho, kwani bajeti hiyo pamoja na mambo mengine ilitegemea mapatao yatokanayo na kodi hiyo ya miamala.