TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

Bora Bandarini kontena libaki moja lakini kodi ilipwe
 
mizingo hiko ming maana tunakusanya matrilion kila mwezi,hahahahahahaahahahahhahah
Na kama hawataki kufuata amri zetu na wasije sasa hawaji na hsyo matrilion mbona yanaendelea kukusanywa hapa pana kiza kinene mimi wasiwasi wangu ni kuwa makusanyo yameshukabkwa asilimia kubwa kama sio nusu na ndio maana mkuu anasema watu wameficha fedha kwenye magodoro sasa ni wakati wafunguke tu bila aibu waseme kweli wanachokusanya wawezekana august wasitaje kabisa maana ni aibu
 
Wenye mamlaka TPA ni pamoja na Kamati ya bunge...Na hiyo ndio taarifa wameitoa
Wewe uliyeangalia hiyo taarifa hebu tupe basi japo data kwa summary tujue kweli mizigo imepungua!!!
 
Sasa kama takwimu hatu zijui kwa kutangazwa, unamaanisha kuna namna nyingine ya kuzijua?

Au mwenzetu unaweza kuangalia moja kwa moja kwenye akaunti za nchi
Sehemu yenye Hela inajulikana....au hukumsikia mtukufu alivyotoa povu kwamba....hela hakuna...
 
Nimeiona hiyo.

Kuna umuhimu wa wadau kukutana na kupatia ufumbuz suala hili. Bandari ya Dar ndiyo roho yetu kuu ya uchumi. Inapoonyesha kutetereka lazima juhudi za makusudi zifanyike kunusuru hali.
Mdau ni mmoja tu.....
 
Kuna clip ilikua inasambaa sana kabla na hata baada ya uchaguzi. Ina maneno '... kwangu mimi watalimia meno ...'
 
Kamati ya bunge imesema mpaka sasa mzigo uliopokewa ni tani 1000 badala ya 40000 kama ni hivyo basi ni sawa na bandari kupokea fuso mia za tani kumi au mzigo unaotosha fuso 100 za tani kumi.

Na hii ni hatari,upungufu wa tani 39000,,
 
Sehemu yenye Hela inajulikana....au hukumsikia mtukufu alivyotoa povu kwamba....hela hakuna...
kumbe na wewe unasikia tu, vithibitisho huna..

na hayo mapato huwa wanasema hivyo hivyo...
 
Akili zingine full majanga...wakati wengine wakinyooshwa wewe utakuwa wapi....!! Huyo mkwere unaemtukuza kuna lipi la maana amefanya au nikuruhusu Watu kugawana Hela kwenye viROBA!

Unauliza aliyofanya Jk?!

1) Ukiona tunajadili kupungua Mizigo bandarini ujue tunalinganisha na Wakati wa Jk.
2) Ukiona Kuna UKUTA ujue wanapigania uhuru Urudi Kama wakati wa JK
3) Ukiona Rais analalamika Mzunguko wa Fedha umepungua ujue analinganisha na Wakati wa Jk
4) Ukiona Hotel kubwa Kama Mount Meru inatangazwa kuuzwa ujue Biashara sasa hivi ni tofauti na Wakati wa Jk
5) Ukiona watu wanalalamika kupandishwa Passmark kuingia Vyuoni ili kupunguziwa mzigo Loan Board ujue wanalinganisha na Wakati wa Jk
6) Ukiona watu Wanalalamika kuropoka ropoka kwa Pombe Jua wanalinganisha na busara na hekma za Jk.
7) Wabunge waliokufundisha kushangilia Ziara za kustukiza Bandarini na kuwatimua Wateule wa Jk ndio Leo wanakufundisha ustuke Hali ya Bandarini ni zaid ya Hatari kutokana na fukuza fukuza na uvamizi ule.
8) Kama ulimuona Msigwa Ikulu kwny kugawa Madawati Jua anayapeleka kwny Madarasa yaliyojengwa wakati wa Jk sio anapeleka chini ya Mwembe!

Unaniuliza watu wakinyooshwa mie ntakuwa wapi Kwan nimekwambia Mie nitakwenda kuandamana kwny Ukuta? Mie sihitaji ajira Serikalini zilizozuiwa, sihitaji Promotion ya Mishahara iliyozuiwa, Sihitaji Bunge Live, Sitegemei kuja Kutumbuliwa kwa kuwa sio Mtumishi wala Mteuliwa, Shughuli zangu hazihitaji Ziara za kustukiza wala Maelekezo ya Wanasiasa. Tambua Mnyoosho huu unawahusu Watanzania Wengi ila si wote

Kumtukuza Jk sijaanza Mie wameanza wale waliokufundisha Kumchukia, hujamsikia Godbless Lema aliefikia hatua ya kupiga Marufuku Amiri Jeshi asikanyage Jamhuri ya Kaskazini yeye na Joshua Nasari wakajitangaza ndo Rais na PM wa Kaskazini lakin hata Onyo hawakupewa lakin Juzi Kati kamtukana Mrisho Gambo tu RC wake Maisha Lupango mpaka kasusa Kula ndio kapewa Dhamana? Hujamsikia Tundu Lissu? Jee nao akili zao Full Majanga kwa kuwa tu wamemtukuza Jk?
 
Juzi kaja na sera mmeficha pesa ndani leo bandari wamekili mambo magum kama yeye ndoo mwenye hakili tanzania nzima unamshauli nini atanyooka 2 maana kazungukwa na watu wanafiki qmbao kazi yao kumsifia 2
 
Wewe jamaa uko Siriaz kweli?
 
Kuna haja ya kuwafahsmu wanaomshauri rais.
Tazama yanayoendelea bandarini
Tazama yanayoendelea katika hotuba zake.
Tazama yanayoendelea bungeni
Tazama yansyoendelea kuhamia Dodoma

na mengine mengi sn.


wananchi tunahaki kuwajua washauri wa raisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…