TPA: Ni kweli Mizigo imepungua Bandarini

sasa gari la milion 5 ushuru wake milion 7 ?? yaana ushuru unabei kubwa kuliko gari bora upitishie msumbiji
 
Upinzani walilalamika Sana hili la bandari na utalii lakini jamaa akasema yeye Ni baunsa WA njaa, njaa ikimuona inakimbia nasubiri mwisho wa mpambano nani ataibuka kidedea ingawa mmoja kaanza kulalamika uchumi umechoka kisa watu wameficha noti
Kuficha noti nayo ni single kama ile ya wafanyakzi hewa na ajira mpya. Tusubir kidogo hiyo nayo ikichuja kwa vyovyote vile kuna nyingine jikoni.
 
Hapana tusijipe mda tuamke sasa maana mda tukiamka Beira Durban na Mombasa zitakuwa mbali hatutakuwa na uwezo tena wa kuvutia wateja hivyo watakuwa na sauti
lakin mbona IMF wametuambia kwamba ni nchi inayokua kwa kasi snaa kiuchumi
 
We kumbe kuna muda hua unaongea points? Usipende kujifunika kitambaa cheusi muda mwingine.
 
Hii kamati ya bunge nayo si lolote na pengine hapa wanaendeleza tu siasa zao, binafsi nilimsikia na kumuona Bw. H.Pope akiwawakilisha wasafirishaji takribani mara mbili na kueleza hatari ya kupoteza wateja, lakini pia walifikisha malalamiko yao kwny kamati ya bunge kabla ya kupitisha sheria hiyo ya kodi hakuna kilichobadilishwa,sasa najiuliza hapa hizo sheria za kodi si zilipitishwa huko bungeni??? Kwa nini hawakuhoji na kuibana TRA na Bandari??? Au walikuwa wapi wamelala au kama kawaida uCCM na kujipendekeza Kwa serikali badala ya kuisimamia???

Hawa wabunge wetu hawafanyikazi zao, anayetakiwa kuishauri na kuisimamia serikali namba moja ni wao, lakini hawafanyi hivyo kazi kugonga meza halafu mambo yakiharibika wanatumia tena fursa hiyo kujipatia umaarufu Kwa wanahaingikia tatizo, najiuliza sana huu muda wa kupitisha vitu hovyo halafu wao wao tena wanarudi kujionyesha wanaguswa na matatizo ili kila mtu awapigie makofi ni ujinga mkubwa hapa Tanzania.

Mlikuwa wapi??????????? Hawa ni wakukamata na kuwafunga kifungo kirefu.
 
Walau umeleta wazo mbadala. Linachangamsha ubongo hili
 
Yaaan hali ni tete kyanan. Bila kubadlshia gia angani na bandari
itageuza uwanja wa mpra kyanan.
 
Kwenye huu uzi wale buku7 wa lumumba huwezi kuwaona..
Fatilia
 
Huwa najiuliza sana wataalamu wengi wa nchi hii sijui kwa nini hawataki kusaidia hii nchi?? Mfano nyinyi wataalamu wa kodi hasa to waziri mwenye dhamani hivi ile sifa ya kodi iwe fair na convenient hukuwai soma hata siku moja???
Kodi inatakiwa iwe ya gharama ya kawaida kwa kila mlipaji aweze kulipa na asione kama ni mzigo kwake, sasa hivi sisi walipa kodi tumezidiwa, kodi zimekuwa kubwa mno tunachofikiria kwa sasa ni kujipanga namna za kuikwepa na si kulipa ili kufikia malengo yenu, tunatafuta njia mbadala kuepukana na kodi zenu (bila kuvunja sheria) na hili ndani ya muda mfupi litaonekana.
Kodi inatakiwa kuwa ya kiasi cha kawaida kwa mlipaji wa mwisho ili kumuwezesha rais wetu kufikia malengo.
Kumbukeni tuna imani sana na Rais huyu ambaye anachukua hatua za kimaendeleo ambazo zinaonekana kila uchao, tatizo mnatuumiza sisi walipa kodi kwa mzigo mkubwa wa kulundika kodi zote.

USHAURI.
Wawezesheni wafanyabiashara wa chini, kati na wafanyakazi ambao ni walipaji wakuu wa kodi kwa kuwapa mazingira yenye kodi za wastani chache zenye kiwango cha kati, vile vile mikopo yenye gharama na mashariti nafuu hii itatia chachu na kuhamasisha biashara kukua hivyo kuwa na uwezo wa kulipa kodi kwa wingi bila manung'uniko au kukwepa.

Yote haya wataalamu wanayajua vizuri ila ubinafsi na viburi vimewajaa, kwa kuwa tu wao wanalipwa vizuri, LAKINI amkae mkijua MUNGU HUYU HUYU ANAWAONA.
 
Mkulu anastahili kulaumiwa kwa hili sababu siku zote alijinasibu kuwa hakuna tatizo bandarini sasa sasa kaumbuka sijui atakuja na utetezi upi au ndiyo atatumbia wafanyabiashara wameficha mizigo
 
Kodi ipo kwa ajiri ya wenyewe kama wenyewe wametosheka inatosha nyie fanyeni kazi tu, na mlipe kodi yake.
 
bosi wa TPA najua atakanusha
Hana uwezo wa kukanusha hili. suala lipo wazi bandari sasa inaweza kugeuka uwanja wa mpira, mizigo hamna. Wafanyabiashara wamehamia bandari ya Beira.
 
DG WA TPA LAZIMA AWE MFANYA BIASHARA MZURI NA AWE NA LUGHA YA BIASHARA SIO YA KIJESHI......HII NI MUHIMU KWA TAIFA. ....MFANYA BIASHARA ANA CREATE NEW IDEAS EVERY SECOND KATIKA UBONGO WAKE. .TOFAUTI NA WATU WENGINE AMBAO MIND ZAO ZIKO CONTROLLED....Nasisitiza. ...have a blessed Sunday!
 
Kufika mwakani tarehe kama za leo kule itakuwa inatamba mv kilimanjaro pekee
Mkuu mpaka asaiv ndo anaetamba mule majini kuna meli mbili tu zinangoja kushusha nimetoka zenji jana tu nimeliona hilo
 
Rais wa chama cha mawakala aliwahi kusema serikali inadanganya wananchi lakini ipo siku itakuja kuumbuka. Sasa yametimia
 
hii habari ya kijumla sana, yamepungua kutoka mangapi hadi mangapi? mapato je? kama urasimu umeondolewa makontena yanaondolewa kwa wakati je? bandari sio yard wala stoo kama hayapo wenyewe wameyachukua.
Tan 40,000 hadi tan 1000, uko wapi wewe bandari unajua ilipo? Pita ujionee..............
 
TRA wanatoa taarifa za kupika juu ya kuongezeka mapato nchini, ki uhalisia unaweza kukuta wanakusanya chini ya 500B kwa mwezi
Mbio za sakafuni tu ngoja stock za bidhaa muhimu zinazoagizwa na serikali ziishe ndio watasema wenyewe hakuna hela ya kuagiza nyingine
 
Ni mtego Mzuri sana. Inaonyesha hawawezi Ku deliver good results . Liko wazi, hakuna mizigo maana yake hakuna mshara . kazi oliuombele yao inajulikana . Waliajiliwa Ku deliver good results.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…