Trafiki aliyekataza mabasi ya Dar kuingia Same kabla ya saa bado yupo ofisini? Kwanini kizuizi kiwe Same na sehemu nyingine?

Trafiki aliyekataza mabasi ya Dar kuingia Same kabla ya saa bado yupo ofisini? Kwanini kizuizi kiwe Same na sehemu nyingine?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kuna taarifa zinasambaa Kwenye mitandao ya kijamii Kwamba Trafic wa Wilayani Same wamekataza mabasi yanayotoka Dar kuwahi kufika Same kabla ya saa Saba. Matokeo yake mabasi yakikaribia same yanapaki barabarani yakisubiri ifike saa Saba yaingie mjini.

Wakati huyu trafic anafanya haya naamini viongozi wa Wilaya na Mkoa wapo wamekaa kimya, tujiulize kutoka Dar Hadi Same Kuna vituo vingapi vya ukaguzi inavyosimamiwa na trafic?

Kama huko kote wameruhusiwa kupita means speed Yao inakubalika, unajiuliza hawa trafic wa Same Wana utaalamu Gani wa ziada? Unajiuliza Same ipo Tanzania au ipo nchi nyingine? Wana Sheria yao ya usalama barabarani?

Ningekuwa Mhe. RAIS watu kama hawa ningewarudisha nyumbani wakajifunze kutumia akili kutenda kazi. Kumsimamisha abiria Same akumwepushi na ajali kwa sababu wapo watu wanatoka Same Wanapata ajali mita chache. Lakini lazima Polisi iwe na unifomity iache generalization, mtu Mmoja awezi kujitungia sheria zake Ndani ya nchi.

Wafuatilie wanaovunja sheria then wawachukulie hatua wawache madreva wafanye kazi Yao Kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Hata singida Kuna muda wa kuingia kama basi limetoka dar,kama nakumbuka vizuri ni saa 10!So madereva walikuwa wakiwahi basi wakikaribia wanaenda kama wanasindikiza harusi au msiba!
Kabla ya hapo,Kuna bus kama Ally's kipindi hicho 12 ziko Kahama,Kuna siku tuliwahi fika Kahama saa 11:30 jioni kutokea Dar!
 
Huu ni upuuzi, basi likimbie kite huko lilipotoka halafu lilikaribia Same lioaki sehemu au lianze kwenda polepole, hii sio njia nzuri ya kuepusha ajali.
 
Hata singida Kuna muda wa kuingia kama basi limetoka dar,kama nakumbuka vizuri ni saa 10!So madereva walikuwa wakiwahi basi wakikaribia wanaenda kama wanasindikiza harusi au msiba!
Kabla ya hapo,Kuna bus kama Ally's kipindi hicho 12 ziko Kahama,Kuna siku tuliwahi fika Kahama saa 11:30 jioni kutokea Dar!
Kufika Kahama 17:30 toka Dsm huo muda si ndio unatakiwa muwe Igunga!, hiyo Ally's ilikuwa hatari.
 
Kwa ushauri ungepaswa kuomba kuwa waongeze Wasimamizi wengine kwenye kila kituo watakao simamia muda wakufika sehemu husika .
Mfano Segera, korogwe nao wasimamie kama anavyosimamia huyo.

Huyu unae mtaja niwakusifia anasimamia kazi yake ipasvyo. Sasa kwa vile wengine hawatimizi wajibu wao ndo unataka nae asitimize?
Au kama utaratibu ni muda upi gari lifike same , yaezekana ndo sehemu walotenga, Japo kweli inapaswa vizidishwe vituo vya usimamizi huo ili kuzuiya mwendo kasi kila hatua.

Jambo ni moja MWENDO KASI UNAUWA. Hasa hizi nchi zetu ambazo miundo mbinu ndo hivyo bado magari yenyewe haya tea tea

Hata kama sinaga imani na mapolisi ila huyu kwa hili yuko sawa

Tusije rudi ile miaka ya "Ajali ya Uwa watu 30+ na majeruhi 20+.
 
Kuna taarifa zinasambaa Kwenye mitandao ya kijamii Kwamba Trafic wa Wilayani Same wamekataza mabasi yanayotoka Dar kuwahi kufika Same kabla ya saa Saba. Matokeo yake mabasi yakikaribia same yanapaki barabarani yakisubiri ifike saa Saba yaingie mjini.

Wakati huyu trafic anafanya haya naamini viongozi wa Wilaya na Mkoa wapo wamekaa kimya, tujiulize kutoka Dar Hadi Same Kuna vituo vingapi vya ukaguzi inavyosimamiwa na trafic? Kama huko kote wameruhusiwa kupita means speed Yao inakubalika, unajiuliza hawa trafic wa Same Wana utaalamu Gani wa ziada? Unajiuliza Same ipo Tanzania au ipo nchi nyingine? Wana Sheria yao ya usalama barabarani?

Ningekuwa Mhe. RAIS watu kama hawa ningewarudisha nyumbani wakajifunze kutumia akili kutenda kazi. Kumsimamisha abiria Same akumwepushi na ajali kwa sababu wapo watu wanatoka Same Wanapata ajali mita chache. Lakini lazima Polisi iwe na unifomity iache generalization, mtu Mmoja awezi kujitungia sheria zake Ndani ya nchi. Wafuatilie wanaovunja sheria then wawachukulie hatua wawache madreva wafanye kazi Yao Kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Spidi inaua wewe endelea kumshangilia drreva mwenye mbio.
 
Hao Ally's bus kipindi hicho ilikuwa hatari tupu, nshawahi ingia Shinya ga stand saa 11.00 jioni from DSM.
 
Kufika Kahama 17:30 toka Dsm huo muda si ndio unatakiwa muwe Igunga!, hiyo Ally's ilikuwa hatari.
Ilikuwa balaa kipindi hicho,na ndio walikuwa wameshika njia ya Dar-kahama kipindi hicho!Baadaye wakaja Princess Muro,Leina,City boy NK!
 
Hao Ally's bus kipindi hicho ilikuwa hatari tupu, nshawahi ingia Shinya ga stand saa 11.00 jioni from DSM.
Ilikuwa balaa sana,ila bus za kutoka Dar-Kahama hazipiti shinyanga mjini!
 
Ebwana eeh niko na kondakta wa tilisho hapa nyumbani kwangu amedhitisha hili kuwa siyo trafic anyefanya hvyo Ni latra ndio wanafanya hvyo na kupelekea kuficha mabasi vichakani wakisubiria ifike saa Saba dkk 35 HV
 
Tatizo sio speed,tatizo ni barabara ni mbovu,Dar to Arusha no kama 650kms huu ni mwendo wa saa 8tu kwa bus!watanzania tusiwe tunaangalia tulipoangukia!barabara zetu bado sana!!
 
Sijui kama nimeelewa tofauti hii mada.... kinachotakiwa ni vituo vingine vyote visimamie kuhakikisha kuwa mabasi yanafika kila kituo kwa muda sahihi uliopangwa.....hao wa Same ni wa kupongezwa.
Ila tatizo kubwa ninaloona ni jamii zetu kuridhika na vitu duni mno! Barabara zetu ni za hovyo mno.....Dar-Same katika karne hii kuchukulia watu masaa saba na zaidi ni uzembe uliopindukia, na hii inasababishwa na barabara feki tunazojenga.
 
Ni upumbafu tuu maamlaka husika kuweka muda wa kufika stendi na baadhi ya vituo inachosha sana abiria.

Mfano mtu igunga ilikua saa 12 unapita kutokea dar saa hivi hadi saa 1 hadi saa 2 kudadek
 
Ebwana eeh niko na kondakta wa tilisho hapa nyumbani kwangu amedhitisha hili kuwa siyo trafic anyefanya hvyo Ni latra ndio wanafanya hvyo na kupelekea kuficha mabasi vichakani wakisubiria ifike saa Saba dkk 35 HV
Mkuu na wewe bana yani kukuthibitishia tu umeshakimbia jamvini kujulisha. Yani ulivyoniambia unaenda uwani kidogo unarudi kumbe ulikuwa unaposti hii comment
 
Hayo ndio matokeo ya kuacha Form Four Failure waongoze nchi kwenye msafara wa maendeleo
 
Back
Top Bottom