Mkumbuke ndiyo askali hao hao wanaoweza kukunyonga akigundua una deal so muwe waangalifu nao.
Kuna basi za kampuni ya tofauti kama BM nk, haya yanakuwa na huduma tofauti ikiwepo na choo cha ndani kile choo kinasaidia sana kupunguza simama simama njiani, so basi linaokoa muda mwingi sana kuchimba mizizi nk, tofauti na zile basi zetu kina saibaba na harambee.
So ndugu trafiki hebu muingie darasani kugundua why mabasi yanawahi na mengine yanachelewa.
Muweke vituo vingi vya ukaguzi ila siyo kuzuia basi kutembea kisa muda, wenzetu huko duniani cha kwanza ni usalama siyo kwa nini umewahi.
Mombasa to Nairobi au Narobi to Kisii wengi wanasafiri usiku, na ndinga zinakata upepo kwelikweli si lelemama, tena unakuta davoo anatafuna mirungi pembeni ana bazoka na chupa ya maji, macho mekunduuu, mara paaap saa 11:43asbh mpo Tom mboya street dantown mnashuka.