mkuu tuna la kujifunza kupitia wewe ninaomba uweke japo kwa ufupi....sio mara 1 nimeona mambo kama hayo ndio maana vijana tabia ya kulakupa kwa wapenzi tupunguze....
Hakika nitajitahidi kujaribu,
Kwa kuwa ni tukio la nyuma sio mbele naweza kulieleza kidogo
Huyo mama yake wa hiyari wakati naanza mahusiano na BM inasemekana ndio alimpa ufundi ili nikae nitulie nisiwe na ujanja, na kweli kwa mapenzi niliyokuwa nayo kwa wakati ule hata mimi kwa sasa naona haikuwa akili ya kawaida ulikuwa ujinga mtupu, sio rahisi kwa akili ya kawaida kupenda vile na sikuwahi kabla labda nitengenezwe tena sio kwa akili hizi za kawaida
BM alipopata ajira mpango wake ulikuwa kusoma kwanza akiwa ndani ya ajira na ndio kisa cha kutoa mimba ilipoingia kwa haraka yeye alitaka asome haraka kisha airudie ndoa yake na ndio kisa cha kuniambia haruhusiwi kuhama mpaka miaka mitatu wakati huo ni utaratibu wa majeshini sio kwa sekta yake
Hata tulipokuwa mapenzini aliwahi kuniuliza ntamuendeleza kusoma? Nikakataa maana siwezi fanya ujinga huo
Kwahiyo adhima ilikuwa iko moyoni mwake kabisa
Kwahiyo alinipenda kweli lakini alikuwa na mipango yake, sasa tatizo la madawa ya mkoa huo hayamtulizi mtu yanamfanya mpumbavu, mabinti wengi wamesababisha wapenzi wao wakafukuzwa kazi maana badala mtu ampende asiwe na sauti anaharibika na kuwa mlevi hovyo asiyejali kazi.
Alipoanza kusoma huko akachanganya mambo mapenzi yakamteka huku mimi akawa hanitaki tena, na ndio pengine mapenzi hayo yalipozaa mtoto
Aliweka mategemeo kule, lakini nako aliachwa ndio akataka kupambania kurudi huku, mimi huku akili zilishanirudi maana hakuna lisilo na mwisho, miaka zaidi ya mitano naona ndumba zilikata ikawa bahati yangu.
Anafanyaje, ndio kurudi tena kwa mama wa hiyari akisingizia anafuata cheti chuoni wakati mimi najua cheti alishachukua machale yakanicheza nikajiambia nitaonana nae ili nimuone yule mtoto lakini sitakula wala "sitakula" chochote chake na kweli mkuu kwanza sikumpeleka home nilimwita eneo lingine na sio room hata pale mezani tulipokaa sikuwa nanunua maji makubwa nilikuwa nanunua madogo ili hata nikiinuka kwenda msalani namaliza maji kabisa ndio naenda, ilitokea mara moja simu ikaita nikaenda kuongea nikaacha kinywaji pale sikunywa tena mpaka akashtuka
Kwenye kikapu aliweka zawadi ya chakula fulani, haya mazao mabichi akijifanya kuniletea kama zawadi
Sikupokea, baadae nikaambiwa ile zawadi lilikuwa tego, kama ningepokea ningevurugikiwa tena, yaani angekuwa ameshikilia maisha yangu mpaka pale atakapotaka yeye.
Kwa sababu miaka kadhaa niliyokuwa napitia kadhia ya mapenzi yake sikufanya maendeleo hata kununua kijiko mkuu inasikitisha sana
Niishie hapo, uliposema vijana wasile hovyo ndio nilipojifunzia hapo tangu wakati huo, sili kwa mwanamke yeyote hasa ninayechepuka nae wala siendi kwake tunakutana juu kwa juu na huwa nawaambia kabisa usijisumbue kunipikia mimi sili, ukiwaambia hivyo wanajishtukia utasikia unaogopa ntakuwekea limbwata
Kimoyomoyo najisemea kwani mna maana nyie
BM alinikamata wakati anasoma, akija kunitembelea ananipikia hapo ndio niliponasa, hata nikikuta meseji ya mapenzi nalia mimi badala yake