FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Huyohuyo Trump anasema katika hiyo interview kuwa aliibiwa uchaguzi mwaka 2020, na kwamba kama angekuwa bado yuko madarakani, Putin asingethubutu kuivamia Ukraine. Ametumia maneno ya kumsifia Putin kama silaha dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa, Joe Biden.Trump kamsifia Putin kuwa 'namna alivyojiingiza Ukraine' katumia akili kubwa mno na katamani pia US wangetumia njia hiyo ktk kudili na sehemu za nchi inayopakana nayo upande wa kusini.
Kusifia huko kumeambatana na tukio zito na tete ambalo macho ya dunia nzima yalikuwa yakilifikiria na mataifa makubwa yalikuwa yakipiga mikwara.
Sasa wewe mjuvi weka link ya sifa alizotoa Putin kumsifu rais yeyote wa Marekani kwamba katumia akili kubwa ktk kudili na changamoto fulani nzito na tete. Sio ulete stori za marais wanatembeleana nchini mwao kisha wapiga stori za mtu na mgeni wake huku wakisifiana kinafiki.
Jitahidi kuzifahamu siasa za Marekani jinsi zilivyo!