Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Hii kitu sio ya kushangilia, wakati tunasema ni bora ili Serikali ijitegemea ila tuelewe sio Tanzania peke yake inayotegemea hiyo misaada, zipo Nchi zilizoathiiriwa sana na zinauhitaji mkubwa sana wa hizo dawa, so tutarajie vifo vingi vya watoto wachanga, watoto njiti na watu wenye maambukizi ya ukimwi maana imekuwa ghafla. Naamini hakuna Nchi ilitarajia hili
Ni kitu kibaya sana hiki kinaenda kuleta maafa makubwa mno
 
Utawala wa Rais Donald Trump umeamua kusitisha usambazaji wa dawa muhimu za kuokoa maisha kwa magonjwa ya VVU, malaria, na kifua kikuu, pamoja na vifaa vya matibabu kwa watoto wachanga, katika nchi zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Hatua hiyo ni sehemu ya kusimamisha kwa muda msaada wa Marekani duniani kote ili kupitia upya programu hizo. Taarifa hiyo imetolewa kwa wakandarasi na washirika wanaofanya kazi na USAID, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Chemonics, ambayo inashirikiana na USAID kusambaza dawa hizo muhimu duniani kote.
Tutazika viongozi wengi sana
 
Attachments

  • IMG-20250128-WA0054.jpg
    IMG-20250128-WA0054.jpg
    142.5 KB · Views: 4
Ni utaratibu wa kawaida kwa US Gov kama Kuna executive orders ambapo hudumu siku 90 tu raisi ana hiyo power isipopotishwa na mamlaka zao basi hiyo order inakufa.Ametoa stop order ila sio kwa kila kitu ,ARVs zipo na hajasema zisimame wapendwa watu wana interpretation zisizo na ukweli Kuna waiver zimetolewa kwenye issue za kibinadamu WAtanzania huwa hawatafuti ukweli.Halafu Serikali ya Tz hawajasema lolote kwa kuwa hii ni stop order sio closure of USAID funds
Watanzania hawatafuti ukweli kwakuwa serikali yao huwa haijisumbui kuweka taarifa bayana. Na hii inatengeneza ombwe la misinformation kama iliyopo kwenye hili suala
 
Utawala wa Rais Donald Trump umeamua kusitisha usambazaji wa dawa muhimu za kuokoa maisha kwa magonjwa ya VVU, malaria, na kifua kikuu, pamoja na vifaa vya matibabu kwa watoto wachanga, katika nchi zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Hatua hiyo ni sehemu ya kusimamisha kwa muda msaada wa Marekani duniani kote ili kupitia upya programu hizo. Taarifa hiyo imetolewa kwa wakandarasi na washirika wanaofanya kazi na USAID, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Chemonics, ambayo inashirikiana na USAID kusambaza dawa hizo muhimu duniani kote.
Duuh
 
Na badooo,
Mlimshangilia humu na kuna waswahili wengine walidiriki hadi kumtungia wimbo na kumuita mkombozi aliyetumwa na Mungu, dawa inazidi kuingia sasa
Una ukimwi!! Au kisa anawazingua ma lesbian 🤣
 
Back
Top Bottom