Tsh. Bilioni 3 kutumika kusaidia Samia Scholarship

Tsh. Bilioni 3 kutumika kusaidia Samia Scholarship

Jumla ya Sh3 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi katika mitihani yao ya kidato cha sita.

Ufadhili huo ambao unaanza mwaka 2022/2023 unafanyika chini ya mpango unaojulikana kama Samia Scholarship.

Akizungumza hayo leo Jumapili Septemba 25,2022, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Septemba 27,2022 wanafungua rasmi tangazo la ufadhili huo ambao utawahusisha wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha juu na kudahiliwa kusoma masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali.

“Baada ya hapo majina yao yatatanangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wamefanya vizuri sana katika masomo ambao wanastahili kupewa Mama Samia Scholarship,”amesema.

Amesema kuwa wanafunzi 640 ndio waliofaulu kwa kiwango cha juu katika masomo ya sayansi, kwa hiyo watafahamu na endapo watadahiliwa katika masomo ya sayansi watakuwa wanufaika wa ufadhili huu.

Aidha, Profesa Mkenda amesema kesho kutakuwa na mkutano wa wadau wa elimu nchini ambapo lengo likiwa ni kupitia sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na mabadiliko ya mtaala wa elimu.

“Majadiliano yatatokana na hatua iliyofikiwa kutokana na mapitio ya sera na mitaala baada ya kukusanya maoni mengi ya wadau ambayo tuliyakusanya kupitia mikutano mbalimbali na wengine wamekuwa wakituletea kimaandishi,”amesema.

Amewataja wadau watakaokutana ni wahadhiri, waajiri na wadau wa maendeleo, taasisi zinazohusihanisha na lugha, wabunge, wajumbe wa kutoka Zanzibar, jumuiya za kielimu, taasisi za tafiti za kisayansi, taasisi za umma, binafsi na dini.

Pia Profesa Mkenda amewataka Watanzania kuwasilisha rasimu za maandiko yao za riwaya na mashahiri katika kuwania tuzo za waandishi bunifu ambazo zinajulikana kama tuzo za Mwalimu Nyerere.
Hamna akili apo. Angesaidia watoto kutoka familia maskini wasiojiweza.

Unaenda kutoa schorship Kwa wanafunzi kutoka st Mary's na feza schools crazy

Ningemuona ana akili angelenga watoto kutoka shule za Kata wenye ufaulu mzuri.

This is cheap politics
 
Jambo zuri ila mchakato wa kuwapata uwekwe wazi tujue kama wanastahili .Maana hii nchi kuna majizi,mapigaji na kubebana bebana tu.
 
Jambo zuri ila mchakato wa kuwapata uwekwe wazi tujue kama wanastahili .Maana hii nchi kuna majizi,mapigaji na kubebana bebana tu.
Naamini mama atahakikisha usimamizi mzuri unakuwepo
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Hamna akili apo. Angesaidia watoto kutoka familia maskini wasiojiweza.

Unaenda kutoa schorship Kwa wanafunzi kutoka st Mary's na feza schools crazy

Ningemuona ana akili angelenga watoto kutoka shule za Kata wenye ufaulu mzuri.

This is cheap politics
Kwa hiyo wewe ulitakaje?
 
Ujinga mtupu, Profesa unakuja kutangaza upumbavu wa namna hii kwa sifa Samia Scholarship wakati Bodi ya mikopo inachechemea

Hivi waafrica akili zetu zipo makalioni?? Wasomi wa Nyumbani wana njaa kuliko mfagia mall wa Canada.

Mungj turehemu watu weusi, Tulikoseaga wapi sisi
 
Ni scholarship ya wazee wa makobasi zaidi
 
Ujinga mtupu, Profesa unakuja kutangaza upumbavu wa namna hii kwa sifa Samia Scholarship wakati Bodi ya mikopo inachechemea

Hivi waafrica akili zetu zipo makalioni?? Wasomi wa Nyumbani wana njaa kuliko mfagia mall wa Canada.

Mungj turehemu watu weusi, Tulikoseaga wapi sisi
Unaumwa saana ,yaani huoni hiyo ni motishwa wa dada zetu wa kike ? Nchi hii ina wajinga aisee, na wewe myahudi upo kwenye kundi la wajinga waliopitiliza aisee
 
Kwa hiyo wanaofaulu wasipate haki yao ya msingi kisa tu CHADEMA hawajahusishwa?
Jaribu kuwa na akili japo ya kuvukia barabara bila kugongwa na baiskeli. Unamkamua mama ntilie kumsomesha mtoto wa Mbunge anayesoma FEZA na asiyelipa kodi. Wakati unafanya hayo Bodi ya mikopo iko hoi haipati hata hela za kutosha, akili za wapi hizi?

Mama Mkapa foundation, Mama Kikwete Foundation na sasa Mama Samia Foundation! Kweli! Nchi inajengwa na wenye mioyo, inaliwa na wenye meno. Nilidhani mtaji wa awali wa Foundation yoyote ile ni hela binafsi na si za umma kutoka kwa akina mama ntilie.
 
Back
Top Bottom