Tetesi: TTCL Kusambaza Internet Bure Majumbani na Maofisini. Bili ni kwa Mwezi

Tetesi: TTCL Kusambaza Internet Bure Majumbani na Maofisini. Bili ni kwa Mwezi

Nchi gani hapa duniani wana hiyo huduma ya unlimited internet bundle? Zitaje 3 nione
Umelala usingizi wa pono. Nilipo natumia 1000 mbps ninavyotaka. Hakuna cha kupimiana. Fiber ya kisasa kabisa.
 
Yaani hio elfu 55 kwangu haina maana maana nikijitaidi sana kufuja mb natumia za elfu 20 kwa mwezi mzima
 
Kwa bei hizo watasubiri sana!! WAtafanana na DSTV ambao wameng'ang'ania bei ya zaidi ya laki moja kwa kifurushi cha compact plus ili kuona EPL. Matokeo yake watu wamekomaa na vibanda umiza!! Wangeshusha angalau ikawa 50,000/= watu wengi sana wangenunua na wangepata faida sana.
sasa hawa TTCL wanataka sh 55,000 kwa intanenti spidi ya chini kwa mwezi, itabidi wasubiri sana! wangefanya sh 20,000/= wangepata watu wengi.
Ningekuwa wakwanza kuisubilia...
 
Wamefelije mbona bei elekezi kabisa😅 unataka ushinde instagram kwa bei gani mzee?
Kwangu mi ni nafuu kuliko utapeli wa kuuziana MB gizani
Mimi huwa nacheza na MB 22 kwa 30,000TShs kwa mwezi mzima sijui nitakwenda vp TTCL kulipa 55,000 kwa kitu ambacho ni fixed ukutani.
 
Kumekuwa ni kilio cha muda mrefu kuhusu upatikanaji wa unlimited internet kwa gharama nafuu. Ilikuwa inashangaza ni kwa nini shirika kubwa kama TTCL Customer Care haliichukui hii fursa (hata kwa kushirikiana na TANESCO ili kutumia nguzo zao). Sasa wapo kwenye right track na watasambaza internet kila kona kuanzia mwaka ujao wa fedha; unajichagulia speed yako kulingana na uwezo wa kulipia kwa mwezi. Asante Jiwe Magufuli kwa kulipa shirika uwezo wa kufanya makubwa, historia itakukumbuka daima.

Bei za vifurushi kwa mwezi:
10mbps > 55,000
20mbps > 100,000
30mbps > 150,000
50mbps > 200,000
cc C.T.U
#KaziIendelee
10mbps kwa 55,000 mbona nitaachana na haya mapaka
 
Back
Top Bottom