Tuache kumuita Rais Samia Suluhu Hassan 'Mama'

Tuache kumuita Rais Samia Suluhu Hassan 'Mama'

Ninyi Chadema gang mnateseka sana, ninyi hata mumuite Bibi kipigo na kubano kiko palepale,hakuna katiba mpya ,hakuna mikutano ya siasa na mwisho hakuna mbuge kufanya siasa nje ya Jimbo lake.

Mtajua hamjui ninyi viwavi wa chadema,mwacheni rais apige kazi na kamwe hawezi kutekeleza majukumu kwa kufuata vitisho vya DJ wa club moja pale Dar.
 
John Heche ni mkurya mtu wa bara huko, asitupangie namna ya kukitumia Kiswahili kwa sababu yeye hajui kwa nini tunamuita Samia mama.

Samia ni mwanamke na kwa heshima hasa ya watu wa mwambao huita mama mwanamke yeyote hata akiwa mtoto mdogo kwa sababu ya jinsi yake. Hatumuiti Samia mama kwa kuwa sisi ni wanae hapana ila ni kwa kuwa yeye ni mwanamke. Ni heshima kumuita mwanamke mama.

Nje ya mada, mbona Nyerere aliitwa Mwalim je sisi sote ni wanafunzi wake. Au tukimuita mtu fulani Daktari ina maana sisi sote ni wagonjwa wake?
 
naunga mkono hoja.

haya mambo ya kuitana mama mama hayapendezi.

asije akajisahau akapractice umama kwenye mambo ya nchi.

yani haipendezi kabisa asante Heche una akili sana.
 
John Heche ni mkurya mtu wa bara huko, asitupangie namna ya kukitumia Kiswahili kwa sababu yeye hajui kwa nini tunamuita Samia mama.
Samia ni mwanamke na kwa heshima hasa ya watu wa mwambao huita mama mwanamke yeyote hata akiwa mtoto mdogo kwa sababu ya jinsi yake...
kwa hiyo mnafata mambo ya mwambao? Hakika Taifa la Tanzania limevamiwa Mungu tusaidie
 
Samia nataka sasa atuonyeshe yeye ni raisi sisi tutaandamana kama kawaida ingawa sio mfuasi wa chadema alimuona Magufuli mjinga alivyokua anadeal na hawa watu sasa na yeye aanze kuua na kupiga risasi kama walivyomtuhumu Magufuli ndio ajue kupractice democrasia kwenye nchi maskini.

kama hizi ni ngumu usione raisi mpaka anachukua maamuzi ya kumpiga mtu bomba za risasi ni mjinga hawa watu wanachukua pesa nyingi abroad kuvuruga aman sasa wameanza na KATIBA kesho watataka maelezo wakina SETH mafisadi wa IPTL walitokaje jela na VIONGOZI WA UAMSHO walitokaje jela na wakati walikua na kesi za kujibu?

#mwendazakehakuampumbavuaumjingakufanyamaamuzialiyofanya
 
"Ni lazima tuanze kumzoesha Raisi kujua yeye ni Raisi tukiendelea kumuita mama anajua sisi wote ni watoto wake kwa hiyo mtoto kwa mama huna sauti." - John Heche

Sauti imesikika vyema brother!!

Aitwe Rais, na sio Mama? au vyote?
Nikumbushe ni nchi gani bara la africa iliwahi kumchagua mama kupitia box. Nimeuliza tu.
 
Samia ni Rais wa nchi ya Tanzania na lazima awajibike kulingana na nafasi yake ki katiba.

Suala la kuwatisha wakosoaji wake huku akiwatabiria laana ya kupambana na mwanamke si jambo la kuvumilika hata kidogo!

Urais haufungamani na u-mama wake ni kwa watoto wake pekee; ndiyo na hii ni kwa sababu si kila awaye hapa Tanzania ni mwanaye kama anavyotaka kutuaminisha.

Rais Samia asilete u-mama kwenye wajibu.
 
Daily Mama Samia Mama Samia unafaidika na lipi?huna uwezo wa kushindana na Mkuu wa nchi endelea na vibarua vyako maisha yaende
 
Back
Top Bottom