Tuchuguzeni kwa makini hizi kelele zinazopigwa kuhusu Ubinafsishaji Bandari, mbona kama kuna Vigogo wawili wanapigania Maslahi yao binafsi?

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Hivi,

1. Kama bandari inabinafsishwa gati na 5 hadi 8 na kuachwa gati namba 9 hadi 11 kwanini kelele ziwe nyingi kiasi kwamba ni bandari yote inauzwa?

2. Kama huyo anayekuja anakuja kuboresha miundominu na utoaji huduma sasa mbona wafanyabiashara ndio wanapiga kelele hawataki kabisa kwani si ndio hawa waligoma kabisa juzi kati sababu ya loopholes za tra kuanzia hapo bandarini na kwingineko?

Cha mwisho kila siku tunalalamika utendaji kazi wa watumishi wetu una loopholes za kutosha sasa iweje leo tubadilike na kuona kana kwamba watu wetu wanatosha kabisa ili hali tunaelewa kabisa uwezo wao autoshei kuhudumu hapo?

Mimi naona hapa kuna maslahi ya watu yanaguswa na wanatumia nguvu kubwa sana kupotosha umma kwa makusudi kuhusu uwekezaji huu na watz tusivyo na akili tunadaka kama yalivyo na kukimbiza kwenye mitandao bila ku reasoning.
 
Unaweza kuwa sahihi, hasa kwa hulka ya WaTz kutokuwa waaminifu, wao ni mchongo (deals), wizi, rushwa na uongo.
Kwa upande wangu kama kuna kelele nitapiga, ni kwa jinsi mkataba unavyoibana Tz, kiasi cha kujikuta kama tunatawaliwa na kampuni tu, ya waarabu. Ni ukoloni wa aina yake. Pili, siwaamini waarabu kuwa ndio watazuia wizi wa tra. Wataiba wao, si pesa tu, na rasilimali nyingine za nchi.
 
Yale yale ya kugawa mgodi kwa malipo ya kujengewa shule na zahanati na barabara ya lami rubish
Si afadhali hapo umeahidiwa zahanati na barabara, huu wa bandari tumeahidiwa nini?
 
Chawa duni kazini
 
Vp tukiwapa wazungu?
 
Hili swala halina tofauti na lile la Maasai Wa Ngorongoro,makelele yalitoka Kenya na Kwa vigogo waliokuwa wananufaika na maelfu ya mifugo..

Na hapa Kuna wanufaika wanaona kitumbua kinaenda kuingia mchanga ndio maana makelele yamezidi.
 
Wataje,usipowataja wewe ni mnafiki sana,hili jukuwaa ni huru sana,funguka tuiponye nchi
 


Akili huna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…