TUJIKUMBUSHE: Timu Maarufu za Ndondo kutoka mitaa yetu

TUJIKUMBUSHE: Timu Maarufu za Ndondo kutoka mitaa yetu

Kagera rangers, faru dume, Sinza stars, Linea Messina, afc leopard, nyarugusu, milambo ya Mburahati, Oman,
Milambo mshindi wa kombe la ishi ile kampeni ya ukimwi na kondom 2022.
Hiyo timu ilianza kupotea baada ya wacheza ngumi kuwa wapanga first eleven hahaaa
 
Wewe ndio age mate wangu humu. Kulikuwa na Msako FC, Mfano FC [hii alicheza Mtwa Kihwelo],

Ngurumo FC, Yetu Afrika, Manta Line [zote Mburahati/Kigogo/Luhanga/Mabibo]. Kulikuwa na Kiboko Msheli [Magomeni], Kagera Shooting aka Kombo Ulaya. Jahazi ya Ilala, Mogo FC ya Ukonga, Vita FC, Magomeni Mapipa. Sifa United na Faru FC za Manzese.

Enzi hizo ilikuwa ubabe ubabe, baada ya mechi lazima vurugu zitokee.

Vv
Wa kina Dame wamepiga sana watu sana ktk mechi miaka hiyo
 
Wa kina Dame wamepiga sana watu sana ktk mechi miaka hiyo
Kipindi hiko ngumi zilikuwa zinawaka muda wowote. Nakumbuka kuna mechi moja ya ndondo huku Morogoro Vijijini Kati ya vijiji vya Hembeti na Kijiji kimoja cha wamasai kinaitwa Kambala. Hahaaa zikaanza kuchapwa, masai wakala kichapo wakaanza kukimbia na wakifika kwenye majumba ya wenyeji wa Hembeti wanawafukuza.
Mabifu ya Mpira yalikuwa yanaenda hadi kijiji kwa kijiji. Vijiji vikipigana na kijiji kimoja kikipigwa na kama kinatakiwa kupita kijiji walichopigana nacho kwenda mjini au sehemu nyingine, wanashushwa kwenye gari na kupigwa.
 
Hatari sana hao watu kuna ile White yakina mbamba mwishoni ya miaka ya 90 inachukua ubingwa pale uwanja wa kinondoni shule ya msingi kabla kambangwa haijajengwa ilikua hatari,shule ya kambangwa imesaidia kuleta elimu ila imeua elimu kata ya mwananyamala maana ule uwanja ndio ulikua uwanja mkubwa wa kucheza kwa gozi viwanja vya kule msisiri vyote vidogo na vyakuchezea chandimu

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
White star ilikuwa igumila kama nakumbumbuka vizuri, kina SHABANI KICHUYA NA SHABANI MANUPA ilikuwa hatari.......

Kina mbamba kule ni CHAUKUCHA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa kopa ile aseeeehhhhh ilikuwa ni kwikwi
 
Na jamaa yao anaitwa KIWIKU.
Hawa jamaa ndio waliosababisha lile vagi kule Ukombozi manzese mpaka kuna jamaa akauawa uwanjani kwa kupigwa na kitu kizito watu wakakimbia na na nondo ikavirugika....wakaja kina Jonas mkude wakajitahidi kuirudisha lakini wapi
 
Wakati hata sekondari ya kambanwa haijajengwa, uwanja ulikuwepo pale ilipojengwa ile ghorofa.Timu ilikuwa ya pascal ambae ni padri mtoto wa mama bahati.
Uwanja naukumbuka na sana maana mi nmesoma pale pale shule ya Msingi na nimekaa maeneo yale yale ya mahakamani kwa juu kidogo

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Kama Mada Inavyosema.

Mimi nimekulia Morogoro na nimecheza sana ndondo miaka ya late 1990's na 2000's nikitokea timu ya Ghetto Boys ya Mvomero.

Katika makuzi yetu tulikuwa tunacheza sana ndondo huko Mvomero na Moro kwa Ujumla na katika mashindani ya Kiwilaya na Mkoa tulikuwa tunakutana na timu za Wilaya nyingine au mikoa mingine pale uwanja wa shujaa Morogoro Mjini.

Timu nyingi zilitoa wachezaji wa iliyokuwa ligi daraja la Kwanza sasa Ligi Kuu mfano Reli, Moro United, Mtibwa Sugar n.k za Moro na nyingine nyingi za nje ya Moro kama Prisons, AFC, Simba na Yanga n.k.

Wachezaji maarufu wa Ndondo ambao binafsi nimewashuhudia na kimsingi walikosa njia nzuri tokana na "Zama za giza tulizokuwa tunacheza na kizazi," ila wangekuwa wachezaji bora nchini na duniani kama wangecheza sasa ni kama wafuatao:

1. David Izengo-Toka timu ya Magereza huyu kwangu mimi ni mchezaji bora kumshuhudia kwa macho yangu nchini sema zama alizokuwa ziliua kipaji chake akaja cheza Prison. Hapa "Triple C" hamfikii.

2. Paul Mokiwa alicheza reli Morogoro na baadaye Prison ambapo alipata majeraha na kuacha kucheza Mpira.

3. Ramadhani Lundenga. Alikuwa ndugu na Hashimu Lundenga na alikuja chezea Yanga B.

4. Abu Ramadhani alikuja chezea Yanga.

5. Salum wa Gheto Boys ya Mvomero

6. Mimi Jimmy Gatete a.k.a mungu ya Magoli toka ghetto boys ya Mvomero.

7. Kipa Maarufu wa Ndondo Yusuph Dezo toka Timu ya Kishingo ya Dakawa pale alikuwa anampiga mikwara Kaseja kuwa yeye Kaseja ni "Tanzania 2" mbele yake naye ni "Tanzania 1" ila mfumo tu umembeba.

Timu maarufu za Ndondo Moro ninazozifahamu na tulizokutana nazo kwenye michuano mbalimbali ni:

1. Jamaica ya Moro Mjini.
2. Young Boys ya Mikese.
3. Jiwe ya Dumila.
4. Ghetto Boys na Asec za Mvomero.
5. Burkina ya Moro Mjini.
6. Kulikuwa na timu moja ya Kihonda waliyokuwa wanachezea akina Ulimboka Mwakingwe, Jumanne Shengo Tondoro na akina Kaseja siikumbuki vizuri.
7. Kulikuwa na timu moja toka turiani iliyokuwa ina wachezaji toka mtibwa kipindi hiko akina Mkangwa, salhina mjengwa, Zuberi Katwila, Mecky n.k

Je, wewe unaikumbuka timu gani maarufu ya ndondo ya mtaani kwenu na wachezaji maarufu waliokuwa wanaichezea?

Nakumbuka Dar walikuwa na Abajalo ya Sinza waliyocheza akina "Kali Mangonga Ongara Mbele kwa Mbele."
Hao Young Boys walikuwa wanapiga mpira hatari. Niliwashuhudia siku moja. Anyway, nilipenda battle la Bomu na Ashanti japo mi nilipenda siku ikicheza Sifa Politan na Kagera Rangers.
 
Aisee hapo kiluvya kwa Komba alikuwepo fundi wa mpira wa miguu(ndpndo) anaitwa Atakiwi.

Mungu aendelee kumpumzisha huyu mwamba.
 
Mtaa wa likwati temeke wailes imewatoa hawa wachezaji

1.Ramadhan leny
2.Edward Chumila
3.George Masatu
4.Mohammed Mwameja
5.Issa manofu

Na wengineo wengi temeke wailesi imewatoa
 
Hawa jamaa ndio waliosababisha lile vagi kule Ukombozi manzese mpaka kuna jamaa akauawa uwanjani kwa kupigwa na kitu kizito watu wakakimbia na na nondo ikavirugika....wakaja kina Jonas mkude wakajitahidi kuirudisha lakini wapi
Akina mkude wenyewe wakawa walevi, wakawazaa watoto kama akina Amani george, kina lau wakaanza toka.Sema msisiri walipokulia malaya, pombe, kamari vikawapoteza.
 
Abajalo vs Faru dume

Uwanja wa Makurumla, magomeni mwembechai late 90's....hatari hiyo
 
Nondo, aiseeeehhh kulikuwa na Kiwiku na Kibesi bila kumsahau Maswini mwamba alikuwa kuvua nguo na kukimbia uchi ground wakati ball linatembea ni kawaida tu.....

Alafu kulikuwa na Shoka ya msufini magengeni kule msisiri dah
Kibesi bado ana urefa urefa ni swala tano sana, maswini ni kama kichaa tu, Kiwiku toka ile ishu ya kinu alitulia.Naona na uzee.
 
Back
Top Bottom