TUJIKUMBUSHE: Timu Maarufu za Ndondo kutoka mitaa yetu

Kagera rangers, faru dume, Sinza stars, Linea Messina, afc leopard, nyarugusu, milambo ya Mburahati, Oman,
Milambo mshindi wa kombe la ishi ile kampeni ya ukimwi na kondom 2022.
Hiyo timu ilianza kupotea baada ya wacheza ngumi kuwa wapanga first eleven hahaaa
 
Wa kina Dame wamepiga sana watu sana ktk mechi miaka hiyo
 
Wa kina Dame wamepiga sana watu sana ktk mechi miaka hiyo
Kipindi hiko ngumi zilikuwa zinawaka muda wowote. Nakumbuka kuna mechi moja ya ndondo huku Morogoro Vijijini Kati ya vijiji vya Hembeti na Kijiji kimoja cha wamasai kinaitwa Kambala. Hahaaa zikaanza kuchapwa, masai wakala kichapo wakaanza kukimbia na wakifika kwenye majumba ya wenyeji wa Hembeti wanawafukuza.
Mabifu ya Mpira yalikuwa yanaenda hadi kijiji kwa kijiji. Vijiji vikipigana na kijiji kimoja kikipigwa na kama kinatakiwa kupita kijiji walichopigana nacho kwenda mjini au sehemu nyingine, wanashushwa kwenye gari na kupigwa.
 
White star ilikuwa igumila kama nakumbumbuka vizuri, kina SHABANI KICHUYA NA SHABANI MANUPA ilikuwa hatari.......

Kina mbamba kule ni CHAUKUCHA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa kopa ile aseeeehhhhh ilikuwa ni kwikwi
 
Na jamaa yao anaitwa KIWIKU.
Hawa jamaa ndio waliosababisha lile vagi kule Ukombozi manzese mpaka kuna jamaa akauawa uwanjani kwa kupigwa na kitu kizito watu wakakimbia na na nondo ikavirugika....wakaja kina Jonas mkude wakajitahidi kuirudisha lakini wapi
 
Wakati hata sekondari ya kambanwa haijajengwa, uwanja ulikuwepo pale ilipojengwa ile ghorofa.Timu ilikuwa ya pascal ambae ni padri mtoto wa mama bahati.
Uwanja naukumbuka na sana maana mi nmesoma pale pale shule ya Msingi na nimekaa maeneo yale yale ya mahakamani kwa juu kidogo

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Hao Young Boys walikuwa wanapiga mpira hatari. Niliwashuhudia siku moja. Anyway, nilipenda battle la Bomu na Ashanti japo mi nilipenda siku ikicheza Sifa Politan na Kagera Rangers.
 
Aisee hapo kiluvya kwa Komba alikuwepo fundi wa mpira wa miguu(ndpndo) anaitwa Atakiwi.

Mungu aendelee kumpumzisha huyu mwamba.
 
Mtaa wa likwati temeke wailes imewatoa hawa wachezaji

1.Ramadhan leny
2.Edward Chumila
3.George Masatu
4.Mohammed Mwameja
5.Issa manofu

Na wengineo wengi temeke wailesi imewatoa
 
Hawa jamaa ndio waliosababisha lile vagi kule Ukombozi manzese mpaka kuna jamaa akauawa uwanjani kwa kupigwa na kitu kizito watu wakakimbia na na nondo ikavirugika....wakaja kina Jonas mkude wakajitahidi kuirudisha lakini wapi
Akina mkude wenyewe wakawa walevi, wakawazaa watoto kama akina Amani george, kina lau wakaanza toka.Sema msisiri walipokulia malaya, pombe, kamari vikawapoteza.
 
Abajalo vs Faru dume

Uwanja wa Makurumla, magomeni mwembechai late 90's....hatari hiyo
 
Nondo, aiseeeehhh kulikuwa na Kiwiku na Kibesi bila kumsahau Maswini mwamba alikuwa kuvua nguo na kukimbia uchi ground wakati ball linatembea ni kawaida tu.....

Alafu kulikuwa na Shoka ya msufini magengeni kule msisiri dah
Kibesi bado ana urefa urefa ni swala tano sana, maswini ni kama kichaa tu, Kiwiku toka ile ishu ya kinu alitulia.Naona na uzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…