Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Mpande kala chumvi hatari. Akisema akusanye chumvi yote aliyokula anaweza fungua duka la jumla la chumvi. 😄
 
Huu mwaka ndo Lemutuz anazaliwa. Jomba umetisha sana. Dingi shkamoo
 
Nalimi a.k.a kocha wa Ifunda Tech Sec School
Mwakalindile a.k.a Brigedia Ifunda Tech Sec School

Hawa jamaa, inapokuja wakati wa wao kuwa walimu wa zamu, ni kwamba assembly hakuna kuchelewa..!! Ole wako
Ifunda kulikuwa na mwalimu mmoja ana jina la kichaga.. hakuwa mnoko sana ila ukisema umpe pocket money akuwekee ndo IMEISHA HIYO.
 
Lubida nguli wa physics kutoka UDZUNGWA SEC SCHOOL
 
Nawakumbuka kwa majina yao tuliokuwa tukiwatania kuna Pokati kajamaa kalikua kimbaumbau alikua anafundisha history na Bwana mzee huyu alikua na kasauti flani kenye lafudhi ya kihaya alikua anafundisha math pia alikua ni academic master pande za Nyakato boys
 
Mwalimu Itambu,Mwenge boys.
 
Mtui nilikuta historia yake pale 1996
 
Wibonele alikuwa maarufu kwa Physics from Mzumbe sec. Tulikuwa tunamsikia sana.
 
Tosa boys, PCB Mzena alikua balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…