Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Umenikumbusha mbali. Nilikuwa pale 1981 mpaka 1984. Mpande namkumbuka sana kwenye mchakamcha saa 11 asubuhi.
Waalimu wetu wa miaka ile- Michael Malale, headmaster; Kasenge, secondmaster; Isack Malisa, academic master, Nzohi, maths, baadae secondmaster; Bhatia & Mikhailov, Engineering science; Mama Mayasa, chemistry, etc
Mpande kala chumvi hatari. Akisema akusanye chumvi yote aliyokula anaweza fungua duka la jumla la chumvi. 😄
 
Sir Lighfoot Stonebridge Henry

Tabora Boys mwaka 1962

Huyu mwamba ilikuwa ukifanya kosa anakupa wosia mpaka analia yaani. Tulikuwa tunaogopa kumuudhi kwa jinsi alivyokuwa anasikitika. Anakufanya ujifeel guilty na kuwa na sympathy. Ndivyo alivyofanikiwa kubadili maisha ya baadhi yetu...
Huu mwaka ndo Lemutuz anazaliwa. Jomba umetisha sana. Dingi shkamoo
 
Nalimi a.k.a kocha wa Ifunda Tech Sec School
Mwakalindile a.k.a Brigedia Ifunda Tech Sec School

Hawa jamaa, inapokuja wakati wa wao kuwa walimu wa zamu, ni kwamba assembly hakuna kuchelewa..!! Ole wako
Ifunda kulikuwa na mwalimu mmoja ana jina la kichaga.. hakuwa mnoko sana ila ukisema umpe pocket money akuwekee ndo IMEISHA HIYO.
 
Lubida nguli wa physics kutoka UDZUNGWA SEC SCHOOL
 
Nawakumbuka kwa majina yao tuliokuwa tukiwatania kuna Pokati kajamaa kalikua kimbaumbau alikua anafundisha history na Bwana mzee huyu alikua na kasauti flani kenye lafudhi ya kihaya alikua anafundisha math pia alikua ni academic master pande za Nyakato boys
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
8. Mwalimu Masatu na Mgimwa - Mkwawa High School (complex)
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Mwalimu Itambu,Mwenge boys.
 
Old moshi Sekondari - Huwezi kuitaja hiyo shule ukamuacha Headmaster aliyejulikana kama - Mtui (Mr)
miaka ya 1990- Alibadilisha Shule ikawa inafaulisha kama special school. Nafikiri yule alikuwa mwanajeshi
Kusimamia nidhamu ya wanafunzi wa kiume zaidi ya 1200 wote wa bweni (o-level & A-level) sio mchezo
Mtui nilikuta historia yake pale 1996
 
Wibonele alikuwa maarufu kwa Physics from Mzumbe sec. Tulikuwa tunamsikia sana.
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
8. Mwalimu Masatu na Mgimwa - Mkwawa High School (complex)
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Tosa boys, PCB Mzena alikua balaa
 
Back
Top Bottom