Mkuu ukiwa ndani ya Kristo hakuna tofauti kati ya jumatatu, alhamisi na jumapili, Mungu anaabudiwa katika roho na kweli. Katika muktadha huu unaweza kufanya ibada wakati wowote na siku yoyote. Mitume walikuwa wanakutana siku ya kwanza ya juma. Biblia imesema waamini wasiache kukutana ila haijasema wasiache kukutana siku fulani.
Halafu Christmas ni siku kama nyingine tu, mimi naungana na wale wanaosherehekea kuzaliwa kwa Yesu (kumbuka hatusherehekei birthday maana hakuna anayejua tarehe sahihi). Kwahiyo unaweza kusherehekea siku hiyo au ukachagua yakwako ukasherehekea kuzaliwa kwa Yesu.
Easter nayo ni kukumbuka ufufuko wa Yesu Kristo na sio kukumbuka exact date. Haisherehekewi siku bali kinasherehekewa kile kilichotokea. Kwahiyo mtu anaweza kuamua kusherehekea wakati wowote au akaungana kwenye siku ambayo wengi wanasherehekea.
Dah,siku zote si sawa mkuu?Hapana,si sawa ni udanganyifu wa Shetani na wanaojiita watumishi.Ni siku moja tu ambayo Mungu aliitakasa na kuibariki,nayo ni siku ya Saba tu,ambayo ni Sabato.Siku zote zitakuwaje sawa wakati ni siku moja tu Mungu aliyoibariki?
Mwanzo 2:3 inasema,
3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Naomba nikukumbushe kwamba wana wa Israel walipokuwa wanakwenda Kanani,Mungu aliwakataza wasiokote Mana siku ya Sabato,ambayo ni siku ya saba ya juma.Kama siku zote zingekuwa sawa,Mungu asingewakataza,so obviously siku zote sio sawa!
Kutoka 16:22-28
22 Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.
Kutoka 16:22
23 Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi.
Kutoka 16:23
24 Basi wakakiweka hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza; nacho hakikutoa uvundo wala kuingia mabuu.
Kutoka 16:24
25 Musa akasema, Haya, kuleni hiki leo; kwa kuwa leo ni Sabato ya Bwana; leo hamtakiona nje barani.
Kutoka 16:25
26 Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana.
Kutoka 16:26
27 Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione.
Kutoka 16:27
28 Bwana akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?
Kutoka 16:28
Naomba nikumbushe kwamba Mungu habadiliki,ni Yeye yule,jana leo na milele.Akishapanga jambo lake,linadumu milele.
Nikukumbushe pia kwamba ni Ceremonial Laws tu zilizo ishia msalabani pamoja na sehemu ya zile Sheria nyingine ndogo ndogo 613,lakini moral laws zote ambazo ni zile Amri Kumi za Mungu zilipita.
Notice God says,
"15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
Yohana 14:15
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Yohana 14:16"
Tatizo ni kwamba tunachagua Sheria au Amri tunazotaka,zingine tuna acha,lakini Mungu anataka tuzishike zote!Mtu akizini anatengwa,uongo hapana,Sabato ndio kabisa imewekwa pembeni.Haifai mambo kuwa hivyo.Mungu anasema mkinipenda mtashika Amri zangu,zote without exception.
Naomba nirudie,Sheria zilizoishia msalabani ni za sherehe tu,za maadili zote zilipita,zile kumi,ikiwa ni pamoja na Amri ya nne ya kuishika Sabato.Notice kwamba Mungu "anawakubusha" tu wana wa Israel kwamba waishike Sabato kwa kuwa ilishakuwepo tangu mwanzo kabla Musa hajapewa hata Amri Kumi.
Kutoka 20:8
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Kutoka 20:8
Notice the word "Ikumbuke,"showing that tayari ilishakuwepo wanajuwa, wanakumbushwa tu.Mkuu naomba niseme hivi,Sabato ni Agano la milele kati ya wanadamu na Mungu,ndio maana hata katika nchi npya na nchi mpya,tutakwenda mbele za Mungu siku ya Sabato.Soma Isaya 66:22-23
Isaya 66:22-23
22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.
Isaya 66:22
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
Isaya 66:23
Swala la mbingu mpya na nchi mpya tunaziona katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 21:1-2
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufunuo wa Yohana 21:1
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Ufunuo wa Yohana 21:2
Yapo mawazo ya kushangaza kwamba watu hawawezi kujua siku ya Saba ya juma ni ipi,that is nonsense.
1.Biblia inaweka wazi kwamba siku ya Kwanza ya Juma ni Jumapili.Ukianzia hapo unaona wazi kwamba siku ya Saba ni Jumamosi.
2.Mungu hawezi kuwaambia watu wamuabudu siku ya Sabato huku akijua hawataijua siku yenyewe.Atakuwa Mungu wa ajabu sana huyo.
3.Clip ya "Historia ya majina ya siku za juma" below keeps to rest mawazo kwamba siku ya saba ya juma ambayo Biblia inaiita Sabato haifahamiki.
View: https://youtu.be/oVbXcwvvVDs?si=AYupAs8cXHroS3Ux