Tukubali tukatae, mtu kuwa na Tattoo ni kielelezo cha malezi mabovu

Tukubali tukatae, mtu kuwa na Tattoo ni kielelezo cha malezi mabovu

Baaada ya muda tattoo itakua jambo la kawaida tu kama wenzetu. Unakuta mfanyakazi wa umma na ana tattoo yake wala hana wasiwasi.

Kuna wanaochora kutopitwa na fashion hata ukimuuliza maana ya hiyo tattoo hawez kukupa jibu. Na mwingine anachora kwa kitu ambacho hataki kukisahau maishani mwake.

Kila mtu na mwili wake ya nini kupangiana na kunyoosheana vidole
 
Mkuuu kuna wengine wamezichora kutokana na matakwa ya kazi wanazofanya hivyo tusiwahukumu wooote tutakuwa tumefanya FALLACY OF GENERALIZATION. Lkn kwa wengineo aina hiyo ya Urembo kwakweli haifai kwa vyovyote.
Mfano kazi gani?
 
Hili liko wazi na wala halina ubishi, mtoto hadi anathubutu kujiweka maandishi mwilini mwake chini ya uangalizi wako?!
 
28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.
Mambo ya Walawi 19:28
Kwa ajili ya wafu manaake ni nini? Mie nataka niandike jina la mama yangu na ndugu yangu wa damu waliokufa tayari kama kumbukumbu!

Ndio bibilia haitaki hivyo?
 
Mambo ya Walawi 19:28
[28]Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
Ye shall not make any cuttings in your flesh for the dead, nor print any marks upon you: I am the LORD.
Huu mstari wa Biblia una historia nyuma yake, watu tunautafsiri kama ulivyo, sina maana ya kutaka kuwaaminisha ninavyoamini mimi ila natoa hoja yangu tu.

Kipindi hicho kulikua na miungu kwenye jamii nyingi, jambo lililomchukiza Mungu, msichanje kwa ajili ya wafu, means kulikua na hiyo tamaduni watu kuchanja kwa ajili ya wafu sijajua nini walikua wanapata baada ya hapo, wala msiandike ALAMA mwilini mwenu ( kwa ajili ya wafu pia). Bible ni historia za kale na future.

Tumepewa Historia zilizofanyiwa summary tu, nyama nyingi zimetolewa na yamebaki mafumbo ambayo kuyategua tunajikuta tupo wrong au tupo right.

Tusimhukumu yeyote kwa kutumia Mistari ya Bible, tunaweza kuwa sahihi au tusiwe sahihi, Kikubwa tuangalie kilicho sahihi kwa ajili ya JAMII zetu.

.....!





Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tukubali tukatae, ukiona mtu ana tattoo yoyote ujue ni matokeo ya malezi mabaya.

Tattoo ni ishara ya mtu kutokujijali, kutojali afya wala thamani ya mwili wake na pia kutokutumia akili sawasawa.

Ndio maana China kwa ajili ya kulinda kizazi cha sasa na kizazi cha baadae imepiga marufuku ukengeufu na kuzuia watu kutokuchora tattoo. Sio China tu, nchi nyingi sasa zimeshaanza kuona kwamba tattoo ni mwenendo mbaya kwa jamii hivyo kuanza kuzipiga marufuku.

Ukiangalia, huwezi kukuta familia zinazojielewa na zenye heshima katika jamii kama wanasiasa, wafanya biashara wakubwa, wanasayansi, wasomi nk watoto wao ama wao wenyewe wamechora tattoo. Na hata kama ikitokea alichora kwa bahati mbaya akiwa mdogo, lazima utakuta anaificha sana isionekane katika jamii. Sababu ya kufanya hivyo ni moja tu kwamba tattoo ni ishara ya malezi mabaya ama tabia mbaya.

Huku Afrika hasa Tanzania ambako usimamizi wa maadili na mwenendo mwema katika jamii imeachwa kwa mtu binafsi, vijana wengi huona kuchora tattoo ni ufahahari kua kama Messi ama 50 Cents.

Tulinde kizazi chetu cha sasa na cha baade kutoka kwenye uharibifu huu wa Tattoo, tueleze vijana tattoo sio jambo jema na sio ufahari, ni ujinga.

Tatoo ni dalili pia kwamba huyo mtu anatawaliwa na Shetani mkuu,it is a sign of demon possession!
 
Mambo ya Walawi 19:28
[28]Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
Ye shall not make any cuttings in your flesh for the dead, nor print any marks upon you: I am the LORD.
Bujibuji uko vizuri na nafurahia comments zako uko balanced! Ukiwa kwenye MMU uko vizuri pia huku kwenye Biblia vivyo hivyo!
 
Lkn kwa wengineo aina hiyo ya Urembo kwakweli haifai kwa vyovyote.
Ni suala la Muda tuu, haya mambo yatakuja kuwa common kabisa kwenye jamii; Mambo kama Uvaaji suruali kwa, Unywaji pombe, Uvutaji sigara, uvaaji nguo fupi etc. There was a time kufanya mambo kama hayo ilikuwa ni ishu kweli kweli, kwanza mtu anaanzia wapi??
lakini in now days ni ishu ya kawaida tuu. Hata kwenye vizazi 10 vijavyo ila amini itakuwa common katika jamii.

There was a time baadh ya Imani hazikutaka Elimu hizi za dunia, ila baada ya miongo mingi tunaona now zinaenea vizuri tena kwa speed. Cultural ni kitu kinakuja na kinasambaa kwa speed;

Ila ninachofahamu bado pamoja na kuenea sana Bado inabaki Personal commitment kuipokea au kuikataa, nami ndio nasimamia hapo.
 
Baaada ya muda tattoo itakua jambo la kawaida tu kama wenzetu. Unakuta mfanyakazi wa umma na ana tattoo yake wala hana wasiwasi.

Kuna wanaochora kutopitwa na fashion hata ukimuuliza maana ya hiyo tattoo hawez kukupa jibu. Na mwingine anachora kwa kitu ambacho hataki kukisahau maishani mwake.

Kila mtu na mwili wake ya nini kupangiana na kunyoosheana vidole
wanawake wengi mnaochora tattoo mnatoa ndogo,

aliskika akisema mtifua tope maarufu.
 
Nachoelewa tatoo ni uhuni kama huna hela tu ila ukiwa kama Carlito wa Samaki Samaki pale kajichora mwili mzima huwezi sikia kelele zozote
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mambo ya walimwengu ukiyatilia maanani mbona hutofanya jambo la kufurahisha nafsi yako. Zamani ilikua msichana ukivaa suruali ya kubana tulikua tunaitaga 'm-bato' unaonekana muhuni. Kiko wapi sasa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mambo ya walimwengu ukiyatilia maanani mbona hutofanya jambo la kufurahisha nafsi yako. Zamani ilikua msichana ukivaa suruali ya kubana tulikua tunaitaga 'm-bato' unaonekana muhuni. Kiko wapi sasa
😅😅😅😅😅😅😆 amevaa mmbato mtoto wa mama Jeni hana adabu kabisa anaonesha maumbile yake😅 leo zinavaliwa za kuchanika kama dekio na hamna mtu anaongea.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji38] amevaa mmbato mtoto wa mama Jeni hana adabu kabisa anaonesha maumbile yake[emoji28] leo zinavaliwa za kuchanika kama dekio na hamna mtu anaongea.
Yaani zipo za aina tofauti zenye kuvutia kwa wembamba na wanene. Unaweza vaa casual au official. Kila zama na kitabu chake
 
Back
Top Bottom