Mama Sabrina
JF-Expert Member
- Jul 30, 2016
- 16,607
- 27,607
Mtaniua jamani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Weweee utatuuaa mpaka nimeliaaYaani nilikua nakimbia huku nawaza ni bora ningebaki kwa majambazi kuliko kwenda kukutana na ule mzuka, kumbe alikua mhanga mwenzetu bhana
Sent from my iPhone using JamiiForums
Haaahaaa [emoji1787]We jamaa mchele mchele sana,,,,,hahahahaa yan unajificha unamuacha wife
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mheshimiwa ni maarufu bongo?1. 2007(TARIME VIJIJINI) niko kidato cha kwanza majira ya saa10 usiku nikiwa na bro tunaenda shule ghafla kwenye kona tunakutana na wezi wa mifugo kama 7 wakiwa na bunduki tukaambatana nao, ikafika mahali wao wakaenda kivyao nasi kivyetu. MUNGU saidia hawakutudhuru wala kutuhoji.
2. 2011-2013 (MKOA Z). Nimekaa na majambazi nyumba jirani, mara nyingi nikitoka usiku kwenda uani nilikuwa nikiwakuta wanagawana bidhaa walizopora kama TV, PC, masufuria, bufa, simu, vocha za jumla, malobota ya nguo, viatu nk. Nawapita nazama uani kisha narudi kulala. Hawakuwa na noma na watu wa kitaa, tena tulikuwa tunapiga nao stori tu kama kawaida na ukiwa na shida wanakusaidia. Watamletea noma yule tu atayetaka kuwachomesha. Vibaka walijaribu kuvunjia watu maduka na nyumba, wakawafata wakawapa onyo wasitake kuwaharibia sehemu za maficho yao na walitii. Za mwizi ni 40, ktk majukumu yao ya usiku walikutana na mheshimiwa(jina na cheo kapuni) wakamuua bila kujua walomuua ana cheo gani. Wote walikamatwa, kwa sasa wananyea ndoo.
Matukio yao ni yapi mkuu ili tujihadhari??Aisee kama uko maeneo ya mtongani kwa azizi ally na umepata breakdown au unapancha tembea ivo ivo kwasababu yatakayokukuta utasimulia kwanzia saa23;00hrs
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata nikiwa nayo sitaweza kuitumia[emoji848][emoji848]...mmmh!usiogope sasa...wewe jiandae tu kwa lolote, usisahau kuweka sime pembeni kwenye mlango wa gari.
Kwahiyo we ni jambazi mstaafu???[emoji848][emoji848]Ni gari Za NMB sio crdb, ilikua Saa 6 mchana.
Ngoja ntaanzisha thread yng nielezee matukio tulopiga japo kwa kifupi nilikuja kunasa maeneo ya nkuhungu Dodoma nikanusurika kuchezea moto lkn mguu walivunja na jicho wakatoa!!sshv nimekua raia Mwema na ibada nafanya Pia.
Sent using Jamii Forums mobile app
kwanini?
Hiyo mtego mara mbili ikuwaje mkuu??Miaka hiyoo... Kuna siku nimetoka kutoa hela benki, kuna gari likanichomekea na kunipiga block... Wakatoka njemba nne, watatu wana bunduki mmoja sime.. Wakaja hadi kwenye milango wakagonga na vitako vya bunduki wakitaka niwape hela... Ile wenge na panic nikashindwa kujiokoa..
Nikaona bora kuokoa uhai, pesa makaratasi.. Nikawatolea pesa, wakabeba na kusepa..
Ila baadae tuliwawekea mtego wakanasa, walikufa na hela zilirudi mara mbili..
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28]...mi muoga mnoo siwezikwanini?
Angepigwa shaba ya tako sasa si ndio uboya wenyewe huo...
Unafika sehemu unasikia harufu ya damu mbichi,harufu ya risasi alafu unashuka kwenye gari kwenda kutoa gogo barabarani kisa huwezi kufa kiboya wakati huo huna uhakika kama wazee wa kazi wameshaondoka au laah..
Bora angepiga uturn arudi alikotoka kuliko kujidai shababi kwenye kutoa gogo
Kifungo Cha Maisha???1. 2007(TARIME VIJIJINI) niko kidato cha kwanza majira ya saa10 usiku nikiwa na bro tunaenda shule ghafla kwenye kona tunakutana na wezi wa mifugo kama 7 wakiwa na bunduki tukaambatana nao, ikafika mahali wao wakaenda kivyao nasi kivyetu. MUNGU saidia hawakutudhuru wala kutuhoji.
2. 2011-2013 (MKOA Z). Nimekaa na majambazi nyumba jirani, mara nyingi nikitoka usiku kwenda uani nilikuwa nikiwakuta wanagawana bidhaa walizopora kama TV, PC, masufuria, bufa, simu, vocha za jumla, malobota ya nguo, viatu nk. Nawapita nazama uani kisha narudi kulala. Hawakuwa na noma na watu wa kitaa, tena tulikuwa tunapiga nao stori tu kama kawaida na ukiwa na shida wanakusaidia. Watamletea noma yule tu atayetaka kuwachomesha. Vibaka walijaribu kuvunjia watu maduka na nyumba, wakawafata wakawapa onyo wasitake kuwaharibia sehemu za maficho yao na walitii. Za mwizi ni 40, ktk majukumu yao ya usiku walikutana na mheshimiwa(jina na cheo kapuni) wakamuua bila kujua walomuua ana cheo gani. Wote walikamatwa, kwa sasa wananyea ndoo.
Fanya hivyo mkuuNi gari Za NMB sio crdb, ilikua Saa 6 mchana.
Ngoja ntaanzisha thread yng nielezee matukio tulopiga japo kwa kifupi nilikuja kunasa maeneo ya nkuhungu Dodoma nikanusurika kuchezea moto lkn mguu walivunja na jicho wakatoa!!sshv nimekua raia Mwema na ibada nafanya Pia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii sasa nilisimuliwa tu hivyo sijui kama ni chai ama kweli.
Kuna siku majambazi walivamia nyumba yenye familia, walipofika wakaamuru watu wote walale chini kifudi fudi, baada ya raia kulala wote jamaa wakakomba kila kitu chepesi kubebeka kisha mmoja wao akawasha redio kaseti iliyokuwemo humo ndani halafu akaweka tape/kanda-(samahani watoto wa 2000) waliojirekodi wakipiga mikwara ya kufa mtu humo ndani akaplay kisha wakasepa, sasa familia kutoka saa tisa usiku wakawa wanaamrishwa na redio mpaka asubuhi wakawa bado wamelala kifudi fudi na majambazi kitaaambo yameshaondoka
Sent from my iPhone using JamiiForums