Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Kigamboni kwa vibaka ndio kwenyewe!.....madenti wa IFM si wanachukuaga huko vyumba vya Bei rahisi, full kubakwa hukoo[emoji17]

Sent using Jamii Forums mobile app
Wezi wa kigamboni wakati fulani nilisikia walikuwa wanalawiti bana vija wa kiume hasa wa ifm jamaa walipochoka wanaume wakaamua kuandama kupinga hali hiyo hadi pale wizara ya elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu nimecheka sanaaa
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1990 uko katika mtaa wa Mandevu compound Lusaka nchini Zambia,tulikokuwa tukiishi baba na mama wote wakiwa wafanya biashara.

mwaka 1990 uko zambia kulikuwa na vuguvugu la mabadiliko kisiasa,wananchi walikuwa wamechoka na maisha magumu baada ya uchumi kuyumba na bidhaa kupanda bei.Zambia chini UNIP na Kaunda wananchi walikuwa wanategemea sana msaada wa serikali kuendesha maisha yao.sasa bei ya shaba ilipoporomoka serikali ilishindwa kumudu kugharamia sehem ya mahitaji ya wananchi.wananchi wakaingia mtaan machafuko yakawa makubwa kiasi cha serikali kushindwa kudhibiti.

Ikatangazwa amri ya hatari mwisho saa kumi na mbili jioni kutembea mtaani.Askali kutoka Tanzania wakashika doria mitaa mingi ya Lusaka.

siku moja muda wa saa moja usiku tukiwa ndani zikasikika risasi nje ya nyumba yetu,baba akaenda kufunga vizuri zaidi mlango wa nje,wale majambazi wakagonga kioo cha dirisha kwa kitako cha bunduki wakaingiza bunduki dirisha na kuamrisha mlango ufunguliwe na taa zizimwe.wakatoa amri kama baba akalale.

walikuwa wamevalia mavazi ya kijeshi na ya jeshi la Zambia.walionekana wanamfahamu vizuri mama shughuri zake.na walikuwa wamempania mama kwani wakati huo baba hali yake kibiashara haikuwa nzuri ilikuwa miezi michache tu imepita tangu avamiwe na kupolwa kila kitu na majambazi,kwa hiyo hawakushughulika nae.
walikuwa kama 7 hivi walioingia ndani wakadai wengine chakula wengine mmojanakatoa amri wafanye kilichowaleta.wakataka pesa mama akawapa alizotoka nazo dukan wakamwambia sio hizo hazitoshi wakaingia chumbani ambako baba alikuwa amelala baada kuamrishwa hivyo wakachukua fedha zote zilizo kuwepo.

Asubuhi yake mama akaenda kituo kikuu cha polisi kureport baada ya maelezo ikabidi liitishwe gwalide la utambuzi bahati mbaya mama hakuwatambua wale wahalifu.ikawa mwanzo wa maisha kuyumba.

wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 9 tu.mwaka ulifuata nikaja Tanzania.SIWEZI KUSAHAU KAMWE.
 
Hahaaahahaha alikuwa mbwa koko huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaaan hapa sijaelewa...ulipanda juu ya pikipiki kama Vandamme kwenye ile movie ya Hard target alivyorukia treni?[emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app

πŸ˜‚πŸ˜‚ hio movie siijui lakini ni kweli nilismama juu ya pkpk nikarukia ile gari ya pickup, yaani nimejikuta tu nimepata ujasiro wa nasmama na kuruka,
 
dooooh pole sanaa bro. kwa kumbukumbu hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…