Bwana Mrefu
JF-Expert Member
- Jul 17, 2018
- 417
- 1,012
Kwa sasa Hiki ndo kisa cha kuchekesha kuliko vyote humu[emoji23][emoji23]Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.
Sent from my iPhone using JamiiForums
kabla ya hayo mabalaa tulikuwa na maisha mazuri ya wastani kiasi kwamba watanzania wengi hasa kutoka Rungwe vijiji walivyokuwa wanatokea wazazi na vya jiran wengi wao walikuwa wanakuja kuanza maisha Lusaka walikuwa wanafikia kwetu.Nilikuwa na akina shsngazi wengi,akina mjomba ,ba mdogo au ba mkubwa na akina ma mdogo.
Jamaa alituchezeshea kichapo kikali mnoo alafu lipo uchi kabisa yaani..😂😂STUNTER said:[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nimecheka saaaana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Walokole bhana hamwishi vituko,badala ya kutupa mkasa unaanza kutupa vifungu vya biblia..2013 Dodoma hahahaa nicheke kwanza lol..nilikutana na vibaka wa4 sehemu mbaya sana aiseee siji kusahau mida ya kama saa 4-5 hivi usiku jinsi nilivyonasuka acheni tuu MUNGU aitwe MUNGU ule ni ushuhuda tosha kwangu maana wangeweza kunicheza karata zote na kuiuza roho yangu lakini niliona mkono wa Bwana wa majeshi,. ndipo ninapokumbuka neno la MUNGU lisemalo "adui zako wakikujia kukuangamiza watatawanyika kwa njia saba"...
Kumtumikia MUNGU kuna faida.
Lete ya kwako ambayo ina vitafunwa kabisaKaka Galadudu,,hii ya 2007 km chai vile[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Sana mi mtu wa usiku sana...toka nimesoma huu uzi nimebadilika mnoohahahah.... asante mkuu nimeona sehemu umeandika kuwa unasafirigi sana usiku kuwa makin mkuu usiku una mengi sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Haaaahaaaa...unajua wanawake sisi huwa ni wepesi sana mdomoni but sikusikia kabisa[emoji16][emoji16]mkuu ulitaka kusikia wanapiga story za kutembezewaa mjurubeng na vibaka [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
ila usiogopa... kuna njia na njia ndio hatari kwa usiku kuna njia nyingine zipo safe hazinaga matukioSana mi mtu wa usiku sana...toka nimesoma huu uzi nimebadilika mnoo
Sent using Jamii Forums mobile app
hahaha... ni wepesi ndio ila suala la kubakwa na kulawitiwa ni exeptional [emoji23][emoji23][emoji23]Haaaahaaaa...unajua wanawake sisi huwa ni wepesi sana mdomoni but sikusikia kabisa[emoji16][emoji16]
Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa ...hilo haliongelewi [emoji16][emoji16]hahaha... ni wepesi ndio ila suala la kubakwa na kulawitiwa ni exeptional [emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
hahaha... nililisikiaga tu kwa watu na kwenye habari....
Aaah wapi walimbwela mbwela hivo hivo tu[emoji16][emoji16]hahaha... nililisikiaga tu kwa watu na kwenye habari....
vipi sasa baada ya habari kutoka mlivyowauliza kuna hata mmoja alikubali kuwa kapitiwa na jambaz [emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mimi ningejiongeza tu ningefanya ana anado ya nani kabakwa nani hajabakwa
Ni hatari,huwa wanachukia sana.
Bila shaka ulisoma Majengo sec. wewe jamaa.hahahahaMwaka 2012
Joka ndio nilikuwa moto kwa watoto warembo nikiwa kidato cha sita huko Kilimanjaro.
Nilitoka na manzi mmoja mkali mtoto wa Kigogo wa Chuo cha Polisi pale Moshi. Rafiki zangu walinionya kuwa niachane na Shani lakini Joka nilikuwa nimeshakolea.
Dogo alikuwa Mawenzi kidato cha tano Boarding. Kila ijumaa alikuwa akija Ghetto Na kurudi Jumapili. Kama unavyojua ujana basi nikawa najiona bonge la mjanja nikiwaoshea Washikaji. Manzi alikuwa amesimama haswa.
Siku moja tuliamua kwenda Waterfall ya Marangu. Na hapo ndipo nilipoonja Joto ya jiwe. Tuliondoka pale mjini mimi Na Shani. Tukafika Marangu Mtoni. Tukashuka. Tukaenda kuchukua Room kwenye hotel ya Kill Hotel kama unaenda kupanda Mlima Kilimanjaro kule.
Hao tukatoka. Tukachukua boda boda mpaka Waterfall ya Marangu. Ilikuwa mida ya jioni watu walikuwa wachache kama kumi na tano hivi.
Tukasaura nguo watu ndani. Punde walikuja washikaji wanne vijeba haswa. wakawaweka chini ya Ulinzi Wale waliokuwa nje ya maji. Walitoa Bastola na kutoa amri ya sisi kutoka ndani ya maji.
Nilikuwa mbishi. wakapiga Risasi moja juu ndipo nikaona hapa hawatanii. Tukatoka Mimi na Shani. Nilipigwa mitama nikahisi kiuno kimevunjika. Shani alipiga makelele tuu. Walipoona Shani anazidisha Kelele walimzaba Kofi akapoteza fahamu hali iliyonifanya nidhani Amekufa. Niliwabwatukia nikitumia nguvu kumfuata aliyempiga Shani. Ghafla nilihisi kitu kizito kichwani na papo hapo nilipoteza fahamu.
Nilikuja kuzinduka Asubuhi nikiwa kando ya Mto Karanga. Nikiwa sina nguvu kabisa.
Sitokuja kisahau. Mapenzi yaacheni tuu
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1990 uko katika mtaa wa Mandevu compound Lusaka nchini Zambia,tulikokuwa tukiishi baba na mama wote wakiwa wafanya biashara.
mwaka 1990 uko zambia kulikuwa na vuguvugu la mabadiliko kisiasa,wananchi walikuwa wamechoka na maisha magumu baada ya uchumi kuyumba na bidhaa kupanda bei.Zambia chini UNIP na Kaunda wananchi walikuwa wanategemea sana msaada wa serikali kuendesha maisha yao.sasa bei ya shaba ilipoporomoka serikali ilishindwa kumudu kugharamia sehem ya mahitaji ya wananchi.wananchi wakaingia mtaan machafuko yakawa makubwa kiasi cha serikali kushindwa kudhibiti.
ikatangazwa amri ya hatari mwisho saa kumi na mbili jioni kutembea mtaani.Askali kutoka Tanzania wakashika doria mitaa mingi ya Lusaka.
siku moja muda wa saa moja usiku tukiwa ndani zikasikika risasi nje ya nyumba yetu,baba akaenda kufunga vizuri zaidi mlango wa nje,wale majambazi wakagonga kioo cha dirisha kwa kitako cha bunduki wakaingiza bunduki dirisha na kuamrisha mlango ufunguliwe na taa zizimwe.wakatoa amri kama baba akalale.
walikuwa wamevalia mavazi ya kijeshi na ya jeshi la Zambia.walionekana wanamfahamu vizuri mama shughuri zake.na walikuwa wamempania mama kwani wakati huo baba hali yake kibiashara haikuwa nzuri ilikuwa miezi michache tu imepita tangu avamiwe na kupolwa kila kitu na majambazi,kwa hiyo hawakushughulika nae.
wakikuwa kama 7 walioingia ndani wakadai wengine chakula wengine mmojanakatoa amri wafanye kilichowaleta.wakataka pesa mama akawapa alizotoka nazo dukan wakamwambia sio hizo hazitoshi wakaingia chumbani ambako baba alikuwa amelala baada kuamrishwa hivyo wakachukua fedha zote zilizo kuwepo.
Asubuhi yake mama akaenda kituo kikuu cha polisi kureport baada ya maelezo ikabidi liitishwe gwalide la utambuzi bahati mbaya mama hakuwatambua wale wahalifu.ikawa mwanzo wa maisha kuyumba.
wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 9 tu.mwaka ulifuata nikaja Tanzania.SIWEZI KUSAHAU KAMWE.