Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 20,877
- 43,633
Pole sana mkuuTulivamiwa Arusha Majengo ya chini, dah aise mzee alichezea visu vya kichwa, house girl kapigwa show, chumba changu kulikuwa na baiskeli ikabebwa jamani majambazi sijui roho zile wanazipata wapi Kama vile sio binadamu
Mwaka 2012/ 2013 nilimchukua Rafiki yangu kimario ambae tulikua tunasoma nae university jijini dar es salaam kwenda nae field nyumbani kwetu mwanza
Tulikata tiketi zetu vizuri Tena gari luxury na la uhakika......
Tulifika alfajiri na mapema ubungo terminal KWA ajili ya safari
Tulikua Kama na mkosi gari tulilo kusudiwa kupanda halikuwepo lilipata hitilafu mpka KUFIKIA saa 3 asbh tupo ubungo
Watu walienda kulalamika saa nne asbh ndipo IKAKODIWA Gari ingine ikaletwa Nakumbuka ilikua Ni gari KUTOKA root ya moshi itupeleke MWANZA
Rafk angu kimario alikua hajawai kusafiri safari NDEFU na tangu kuzaliwa alikua hajawai kufika mwanza
Tulifika shinyanga saa 6 Usiku na ilikua Ni sheria kuto endelea na safari muda huo....
Drevaa wetu aka force anasema lazima afike mwanza....
Tukaendelea na safari tukafika HUNGUMALWA
Njiani tuka kuta Kuna mabasi na magari madogo zaidi ya matano yamepasuliwa vioo na watu wana vuja damu..... Wakiwa waneporwa vitu vyao
Kukatokea mabishano mm nikawa kinara tusitishe safari turudi nyuma tutafute sehemu salama mpka kupambazuke....
La haula hii dunia Ina Mambo.....
Drevaa akajibu wanaotaka kushuka washuke yeye anaendelea na safari.....
Wapo walio msapoti
Hatukua na jinsi safari ikaendelea.......
Majambazi watekaji wa magari wanajua sehemu za kuteka magari
Sehemu nyembamba na zenye mabonde ndizo huweka berriear Zao
Drevaa akatamka akisema abiria tumetekwa......
Kilitokea kimya Cha gafla ndani ya basi KILA mmoja asijue Cha kufanya.....
Mm nilisema nili waambia toka mapema Sasa yametukuta....
Drevaa wetu akasimamisha gari nilichagua begi langu lenye vitu vya samani tayari kushuka chini kukimbia.....ndio akili ilivyo nituma kujiokoa......
Tukajikuta wanaume kumi tumeshuka chini KWA wakati mmoja....
Tukaona watu Kama 8 wanakimbilia vichakani wakiwa na silaha....
Kilicho saidia Ni KUA baada ya kuteka magari ya mwanzo majambazi yaliogopa yakajua TUTAKUA NA ESCOT YA MA ASKARI DATC WAY TULISHUKA CHINI WAKAKIMBIA MAPORINI
DREVA ALIRUDISHA GARI REVERSE MAANA ENEO LILE LILIKUA VERY TACTIC
Tukarudi tulipo toka Nakumbuka tuliludi mpk Kijiji kimoja
Tukasimamisha gari tukalala juu ya miti...
Nadhani KWA watu walio wai kutana na ukatili wa majambazi wanafahamu.....
Daah! Moja ya comment iliyonisikitisha Sana hasa kipande cha wife kukuita uamke. Pole na amini siku hiyo Mungu alikua side yako, hii ya kushtuka saa nane usiku nadhani inatibika na psychologist.Mwaka 2010, nyumbani tulikuwa wawili tu, mimi na mama watoto,tu na wakati huo tulikuwa hatujaanzisha familia bado.
Nilirudi nyumbani mapema Sana siku hiyo mida ya saa 12 jioni tu, baada ya kula mapema pia nikaenda kujipumzisha mapema pia, saa nane usiku nikasikia milio ya bunduki, nikahisi hapa tushavamiwa, Jana yake tu nilikuwa nimetoka kuchukua kagari Ka kutembelea( T blj), nikajua pengine ndo wanafata Hilo Gari, kwa hiyo si kuwa na idea kama wangeweza kunidhuru kwa kuiba Gari ambalo lipo nje na wangeweza kuwasha tu hata kwa funguo Malaya na kuondoka. Nyumba haikuwa na fensi
Kulikuwa na ukimya wa kama dakika moja, nikasikia tena milio mkubwa Sana maeneo mlango wa sebuleni na wa jikoni kwa pamoja! Sekunde kadhaa tu wakawa tayari wanavunja mlango wa chumba changu!
Muda wote huo wife anahangaika kujificha chini ya uvungu bila mafanikio, ni kibonge flan, so zoezi Zima la yeye kuingia huko halikuwezekana,mpaka jamaa wameingia nilikuwa Sina clue, yaan wakanza straight na mapanga mwilini,, toa pesa!toa pesa! Tunajua umezificha, chumbani walingia kama watu watano,wawili ni heavy kiasi kwamba nikahisi hapa nikijaribu kufurukuta napotea, watatu wa kawaida tu ningeweza kupambana nao kama wasingeambatana na Hao heavy duty, nikaona ni comply tu yaishe!
Mapanga yalitembea takriban dk 5 mfululizo, wife ndo alikua mtetezi wangu analia kwa kuwaambia kuwa Leo huyo baba hajaja na hela, an gekuwa nazo angewapa, kiukweli Nina kawaida ya kumkabidhi wife kila siku kile nilichokuja nacho nyumbani, na siku hiyo kweli si kuwa na pesa niliyokuja nayo nyumbani, ila kulikuwa na laki mbili tu kabatini ambayo nayo ilikuwa kama balance ya dharula, wakaichukua!
Moment ambayo Hua inaniumiza hadi Leo, ni kuna mmoja alikuwa amepania kuniua kabisa alipiga panga mbili Moja ikaingia haswa, ya pili nikasema hapana, ngoja nikinge, ikaondoka na kidole kimoja, baadaye akanitupia taulo huku akisema jifunike sasa nakata shingo hapo nadhan ufahamu wangu ndo ulifika mwisho,
Wife alikuwa anaona kila kitu, anasema baada ya tukio la kunitupia taulo alipiga panga mbili ambazo alikosa zote, ikawa wenzake wanamuita kwa code ndo ikawa pona yangu, nililala hapo chini huku nikiwa Sina fahamu, hadi nilipokuja kusikia sauti ya wife aliniambia mume wangu, kama upo hai amka wamesha ondoka,!! Ni sauti ya huzuni kabisa kuwa hi kusikia Kutoka kwa mke wangu, anasema alijaribu mara kadhaa Kuniambia hivyo, Lakin si ku respond akajua nshapotea. nadhan mungu tu alikuwa upande wangu siku hiyo.
Hawakuchukua Gari ambalo nilidhani ndo liliwaleta, kilichofata nilikimbia nyumba na kwenda kupanga Tena mana niliona haikuwa bahati yangu kujenga, ila Nilirudi baada ya kupata Familia, na nipo hadi sasa ila nina makovu kichwani na kidole kimoja Sina, plus mimi. Na wife kila ikifika saa nane usiku automatically tunakua macho, hii nadhan ni physiological toucher ambayo tutakufa nayo
User name yangu inareflect namba za Gari ambazo nadhan lilichangia pia kuniletea majanga. siku ya tukio tulivamiwa nyumba tatu mitaani, sisi tulikuwa wa mwisho kuvamiwa na Kutoka na maisha. nyumba moja walimuua baba na ya pili wakaumuua mlinzi, kwa maelezo ya wenzetu muuaji alikuwa yule yule aliyekuwa ananisulubu mie.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wangu acha kabisa sie binadamu ni viumbe wa pekee kiupekee.Aisee hawa watu sio binaadamu wa kawaida
Mtu kuchinja tu kuku unatetemeka na kusikia huruma sembuse kumpiga mtu panga? Tena unataka kumuua? Binaadamu ni kiumbe katili sana
Acha porojo weka kisa hapa2013 Dodoma hahahaa nicheke kwanza lol..nilikutana na vibaka wa4 sehemu mbaya sana aiseee siji kusahau mida ya kama saa 4-5 hivi usiku jinsi nilivyonasuka acheni tuu MUNGU aitwe MUNGU ule ni ushuhuda tosha kwangu maana wangeweza kunicheza karata zote na kuiuza roho yangu lakini niliona mkono wa Bwana wa majeshi,. ndipo ninapokumbuka neno la MUNGU lisemalo "adui zako wakikujia kukuangamiza watatawanyika kwa njia saba"...
Kumtumikia MUNGU kuna faida.
We jamaa nimekuona like[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Duh kama muvi vile.Mwaka fulani nimetoka Mbeya na Mr saa saba za usiku, Kufika maeneo fulani karibu na Morogoro kuna kona fulani hivi ya kishkaji, sijui Mr alikua na nini kichwani hakuangalia mita kadhaa mbele, mi nimelala zangu nakula usingizi kwa raha zangu, ghafla nikahisi kama gari imepaki ghafla, nikasikia ananiambia amka amka!
Kufungua macho naona malori mawili yamepaki pembeni ya njia mbele ya malori kuna gari dogo nayo imepaki halafu kuna bongee la gogo katikati ya barabarani Mr akanambia kuna tukio la utekaji hapa either linaendelea ama kimeisha muda si mrefu, Salaleee usingizi ulinitoka wote, nikakwambia Mr turudi tulikotoka akanambia No, kwenye matukio kama Haya huwa haturudi nyuma.
Nilipaniki nusu nimnase kibao nikamwambia sasa tusirudi nyuma tubaki hapa watushike na sisi? Akasema anavyoona yeye lile tukio limeshaisha na wenye magari haya either wamepaniki wamekimbilia vichakani ama watekaji wamewachukua wameondoka nao. Nililoa jasho hadi pichu, mi kwa akili yangu nilikua nafikiri wamewakusanya wenye magari wako nao mahala wanatuangalia na watajitokeza sio muda kutuchua na sisi Ndio maana nilikua namsisitiza Mr turudi tulikotoka ye anamsisitiza hakuna kurudi.
Akanambia ye anashuka ajaribu kutoa gogo tupate pakupenya, hivyo mimi nishike wheel ikitokea wakajitokeza wakamkamata mi nirudishe gari reverse vyovyote vile bora nipate ajali ila wasinikamate nikiwa mzima anasisitiza maana wanaweza kunibaka. Haya mabishano yote yalifanyika kwa dakika kadhaa, mwisho kishingo upande nikamkubalia ashuke. Akashuka nikakamata usukani, nikafunga belt nikajiandaa huku natetemeka hakuna mfano.
Ile ameshuka tu akakamata gogo naona ni zitooo hata haliwezi akatokea kijana porini amepigwa vibaya sana kumbe alikua mmoja wa madereva waliotekwa, kidogo wengine wakajitokeza wakawa wanaelezana kilichotokea, mwisho wakakubaliana watembee kwa kuongozana hadi wakutane na Barrie ya mapolisi watoe taarifa. Wale madereva na makonda wao walikuwa wamepigwa sana wanavuja tu damu, nakumbuka mmoja sikio la kulia lilikua limelegea kama linataka kudondoka na kwa wakati huo niliona kama hasens chochote zaidi ya kuona tu midamu inamvuja. Basi ndo hivyo tukaondoka kwa kuongozana tulifika Barrie ya polisi karibu kabisa na Moro tukawaacha sie tukasepa zetu, tumbo liliniuma siku hiyo sitasahau sijui ni sababu ya uoga.
Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
naona hatuelewani mkubwa nasema ilikuaje mpaka huyo kicheche akakuletea mpaka ukaingia kwenye nyumba ya watuWapi nimesema nimebaka?
like father like son, hahaha pole sana mkuu!1. Miaka ya 2000 mwanzoni, likizo time mshua katufata boarding school tunarudi home. Tulichelewa kuvuka boarder ya Mutukula tunaitafuta Bukoba. Baaasi tukakutana na bonge la road block, wazee walee na SMG zao. Wakapunga mkono style ya Traffic police wa awamu ya tano. Sijui mshua alitoa wapi confidence, ali reverse shangingi faster na kwa speed almost 40km/h au zaidi for about 10 minutes, akageuza huyooo tukarudi boarder tukala.. ndo ikawa pona yetu..
2. Wazee baba walikua wanammendea mshua kitambo, wakijua pesa pale ipo. Sehemu ya kazi ya mshua ilikua ni porini, katika ranchi za taifa. Basi siku moja mshua kapokea mishahara ya wafanya kazi, kaenda nayo porini. Majambazi yakatonywa, yakajiandaa, jioni saa kumi na mbili yakatimba home na bunduki kubwa kubwa, sisi watoto hatujui A wala B. Mshua alikua katoka kaenda kupiga maji na washakji zake. Majambazi yakatukuta sisi na step mom, yakamwambia step mom awapekele mpaka safe ilipokua, akawapeleka, sema wakashindwa kuifungua. Wakatafuta funguo wakakwama. Mama nae hajui funguo ilipo. Wakampa kipigo cha mbwa koko lakini hakuwapa walichokitaka, kiukweli hakujua funguo ilipokuwa. Safe wakaifyatulia risasi lakini haikufunguka.. walivyoona muda unakwenda, wakabeba redio, TV na jewerly wakasepa. Dingi anarudi kalewa zake, anasema funguo zilikua kwenye suruali aliyokuwa kaivaa jana yake, suruali iko juu kwenye hook.
3. Mwaka 2016 saa nane usiku natoka zangu kula bata na wana wa TIA, nina kama mwezi nimenunua mark X, nafika TAZARA taa zinawaka red, hamna magari kabisa na malori ni yakuhesabu, ile nasubiria zimulike green, akatokea mtu out of nowhere anataka nishushe kioo, ana bonge la panga.. nikajaa wenge, pombe zikaniishia. Jamaa mwingine akatokea upande wa kushoto akaanza kugonga kioo kwa kitako cha bastola... mweeee, nikakanyaga mafuta gari inaondoka kwa speed matata. Bahati nzuri nilikua sijaweka P(parking). Kuna semi trailer lilikua linavuka kwenda airport nililikosa kosa kuligonga. Nikanyoosha mijamaa nikaiacha haiamini kama nimeiponyoka. Nilipofika Buguruni sikujali kama kuna watu na magari wanavuka 24hrs. Huyooo mpaka getto Tabata.. !
Sent using Jamii Forums mobile app
hivi wolf ndio mbwa mwitu?2011, mbezi beach mida ya saa 7 usiku nimetoka samaki samaki mbezi ninaelekea home nilitoka kuangalia mpira, ninapiga moja moja, kona ya kwanza ya pili naona jamaa wawili wananifuata, nikavuta kisu changu cha kiunoni nikakiweka sawa mkononi ghafla jamaa mmoja akaanza kutembea kwa kasi mpaka akanifikia, kama anataka kunipita akataka kunipiga kikumbo nikamkwepa kadondoka jamaa wa nyuma kaja anataka kunitia kabali nikampa ki “pepsi” hatari nikamsokomezea na kisu cha usoni, kilimchana mdomo, jamaa wa chini nikamshushia visigino, vya kufa mtu nikamuongeza jamaa kisu cha mgongo nikakimbia nakuomba msaada, kumbe ni majamaa wa pale mtaani hawakufa ila mpaka kesho wakiniona wanabadili njia
hata Yesu alisema atakuja kama mwizi. it means ya mwizi hayajulikani lini yanatokea mkuuUSIKU HAUSHONI NGUO, ILI KUEPUKA YOTE HAYO EPUKA KUTEMBEA USIKU KAMA UNATEMBEA JITAHIDI KUWA NA PESA YA KUKUSAIDIA USAFIRI KAMA NI DHARURA CHUKUA TAHADHARI NYINGINE KAMA KUWA NA SILAHA UTAKAYOWEZA KUTUMIA VZR, KAMA VP RUDI NYUMBANI MAPEMA.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah nimecheka mmpaka mchozi2016 enzi hizo nasoma chuo.. tulikuwa ghetto watu watatu yaani mimi na rafki zangu wawili.. Tulikuwa tunapiga story mara ghafla usingizi ukatupitia bila kuzima taa na dirisha lipo wazi so tulikuwa tunaonekana tulivo lala na watu wanaopita nje..
Kumbe wizi wakatuchora wakuruka geti la nje na kusogelea chumba chetu na kufungua mlango taratibuuu aiseee kulikuwa kuna smart phone 3 zipo chaji na laptop 1 jamaa alikuwa anachek movie kabla hajapitiwa na usingizi..
Mi nlikuwa nimelala huku nimeupa mgongo mlango so mwizi aliingia kwa nyuma yangu..
Nikawa kama naota kuna watu wameingia chumbani nikageuka kuelekea upande wa mlangoni yaani nikawa kawa kama nimegeuka kumuangalia mwizi anavotuibia..
Yaani nilikutana na jitu jeusi tiii alafu lina miguu mikubwa kama ya tembo alafu lipo uchi wa mnyama limejipaka mafuta mengi yaani linateleza tu aiseee wizi wanatisha jamani..
Nikapiga kelele na kumrukia maana hakuwa na silaha yoyote alinipiga na laptop usoni mpaka ikapasuka wale wenzangu kukurupuka mmoja akala teke la uso na kuzimia palepale.. Mimi kile kichapo cha laptop usoni kilinifanya nianguke kitandani mpaka nikavunja chaga za kitanda.. jamaa ndo kukimbia na kuruka ukuta na kusepa mazima ila akuiba chochote ila alikuwa na wenzake nje... sitasahau kabisa
Mkuu kilichotokea huwezi amini kilichotokea. Hii kitu ukijua kuitumia aisee labda waje na chuma.hahahaha malizia
Daaah we jamaaaa umenichekesha hatariNakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.
Sent from my iPhone using JamiiForums