Tukutane wanaume tuliowahi kupata “wife material” mpaka leo tunajuta baada ya kuleta wenge

Mauno [emoji16][emoji16]
 
Kosa lilikuwa nini mkuu...
 
Aisee usinikumbushe machungu ya yule mrembo wangu. Yaani bonge la wife material sasa bwana kweli ujana maji ya moto.
 
Si wengine hatuna ex wa maana wote vichomi, mmoja alivyoenda kusoma nikala kibuti mwingine nilikuwa nae kumbe mwenzangu anamapenzi na ex wake.

Basi tena siku hizi nadate kimitego na sio king'ang'anizi kama zamani sijawahi kukutana na ke yoyote wa kusema huyu wife material, wengi ni block 41 kikosi.
 
Block 41 kikosi ndiyo nini mkuu?
 
Pole sana Chifu.

Usiendelee kuwapenda maana tayari wajanja tushajinyakulia shilingi uliyoichezea chooni...[emoji124]
 
Mnara wa voda au sioo..
 
Single mother wengine wanashawishi
 
daaah pole sana
 
Mi title ya uzi iko tofauti kwangu 😀 yaan nilioa kicheche baadae nikaangukia kwa wife material hadi sasa niko nae.
Picha linaanza baada ya kumaliza f6 nikaenda kwa anko, pale kwa anko alikuwa na jirani yake na huyo jirani yake alikuwa anaishi na mtoto wa dada yake aliye mlea tangu kachanga maana dada ya huyo jirani wa anko alifariki akaacha kadogo sana ilikuwa ngumu sana kujua sio binti wa kuzaa wa huyo jirani ya anko maana kalikua kanamwita baba badala ya anko.
Anko na huyo jirani yake walikuwa wasabato kamili kwa hiyo na kabinti kenyewe kalikuwa kasabato kalikoshika dini balaa na kalikuwa form 4 pindi hiyo kitabia kweli kalikuwa kamelelewa kakaleleka sasa wazo langu nikawa nataka nichape nitembee siku moja wameenda church miji yote kakabaki home mzee, nikafanya mambo siku hiyo kumbe kalikuwa bikra ... basi roho ya kukaoa ikawa inanitembelea sana ugumu ukawa dini ... matokeo ya six yalipotoka nikaendelea na chuo na mambo mengine miaka ikapita sana kila nikipiga simu kwa anko naogopa kuulizia habari za dogo kwamba anko angestuka..
Nikaja kuoa mwl mmoja hivi dahh alikuwa fresh kimwonekano rangi, sura, tako nikaona dhahabu nikaweka ndani hakuna rangi niliacha kuona demu kumbe kicheche....
Siku moja nikampigia mke wa anko katika kuwajulia hali nikauliza vp fulani ... ooh pale tulihama ila wakati tunahama tayari anko wako na yule jirani yake walikuwa hawapatani tena maana waliingia mgogoro wa kiwanja ilikuwa vita hatari ila yule demu aliolewa..
Siku zikaenda miaka ikapita.. siku moja mke wa anko akanipigia ameonana na dem sokoni demu akamuuliza habari zangu akaambiwa nishaoa na nina watoto akaomba namba yangu na yeye akamwambia anti kuwa alirudishwa kwao kwa kuwa hazai jamaa yake akaoa mwingine kwa hiyo yuko home tu.
Siku moja namba ngeni ikaita kupokea ni demu stori za hapa na pale mzee cha kufuia nini nikamweka ndani kicheche akasepa huwezi amini mwaka uliofuata demu mjamzito ni wife material kweli kweli... wife material ni wale ambao unawajua malezi yao tangu utoto wao. 😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…