Tulia Ackson: Gazeti la mwananchi, JamiiForums tunawategemea kuwapelekea taarifa sahihi, tusipeleke za upotoshaji

Tulia Ackson: Gazeti la mwananchi, JamiiForums tunawategemea kuwapelekea taarifa sahihi, tusipeleke za upotoshaji

Kwa kuwa taarifa zipo bungeni, tunaomba waandishi wa JF, mkachukue hii habari kama ni kweli ipo au siasa.

Vijana wa 90 tukiuliza tunaambiwa tunaropoka.

Vipi Tulia Ackson, huyu umembana na hili tamko hewa?
20230404_144227.jpg
 
Kongole kwa menejimenti na wanachama wote JF.Katika mitandao ya Kijamii JF tunaongoza kwa kutembelewa na wasomaji wengine wanafuata.wakati kwa upande wa Magazeti Mwananchi inaongoza.
Tutumie jukwaa hili kutoa maoni na ushauri kwa Serikali,
 
Wanabodi,
Hii ni Breaking News kutoka Bungeni Dodoma!. Baada ya Rais Samia kusema huwa anaingiaga JF, kutusoma na kubaki akicheka. Leo kwa mara ya kwanza mtandao numero Uno Tanzania, Jamiiforums, leo imetajwa rasmi Bungeni na Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson " Vyombo vya Habari Mwananchi na Jamiiforums, Tunawategemea" Kutusaidia Kuihabarisha Jamii taarifa sahihi za Bunge"

Naifuatilia clip

Mimi ni member wa JF kwa muda wa miaka 15 sasa, if imekuwa ikifanya mengi makubwa mazuri kuisaidia serikali na viongozi wake but was barely or hardly recognised, hivyo hii mention ya Spika, it's good kwa JF.

Sisi members wa jf tuwe makini zaidi, kama Mkuu wa Mhimili Mkuu, Rais wa JMT amesema anasoma JF, leo Mkuu wa Mhimili wa Bunge ametutaja, bado Mkuu wa Mhimili mmoja tuu wa Mahakama, of which its just a matter of time.

Mimi kwa niaba yangu binafsi kama mwana JF, nakiri kuwa niko very proud to be a JF member.View attachment 2576131

View attachment 2576132View attachment 2576133
Nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu Maxence Melo na timu yake ya JF kwa kazi kubwa na mzuri ya uhabarishwaji wa jamii, upashanaji habari, na kutupatia fursa adhimu na adimu ya kutupatia mawanda ya freedom of speech and expression kwa sisi members.

Pia natoa shukrani zangu kwa JF kutu recognizes baadhi yetu na kutupatia zawadi na bahasha nene ya chochote kitu!.

Thanks JF,
God Bless Mkuu Maxence Melo
God Bless JF Staff
God Bless JF Members
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Mkuu Paskali ..hongera..Ila ,by the way kwanini unapenda kuvaa nguo oversize au ndo uko mbele ya wakati!?
 
Wakati ulipoambiwa Mayalla maanake njaa kwa lugha ya Kizinza pia ulikenua sana humu jf😆
 
Hakika JF inazidi kupaa!

Alianza Rais Samia, kwenye kongamano la Chadema, akiitaja JF, na hivi leo nimemsikia mwenyewe Spika wa Bunge, Tulia Ackson, akiitaja JF, kuwa ndiyo kinara wa kutoa habari hapa nchini👏👏
 
Spika wa Bunge, Tulia Ackson ameongelea vyombo vya habari na kuwaomba waandishi hawapendezwi na habari za upotoshaji kuhusu Bunge kwasababu liko wazi.

Tulia kasema wanawategemea Mwananchi, JamiiForums kuwapelekea wananchi taarifa sahihi na si za upotoshaji, amesema haipendezi hasa kama waandishi hawajanyimwa taarifa.

Spika wa Bunge kutaja Mwananchi na Jamii Forums tena akivitaka kutoa habari kwa weledi na kuepuka upotoshaji sio suala la bahati mbaya, ni kwa sababu kwa mujibu wa Bunge, Mwananchi na JF Walipotosha.

Mwananchi walichapisha habari kuwa bunge limetunga kanuni mpya na ngumu kwa wanahabari. Link nimeweka chini hapo

Bunge latunga kanuni ngumu kwa wanahabari, wadau wang’aka

Pia JF waliandika habari hii, Link yake pia hii hapa



Bila kuathiri wa kutetea undani na maudhui ya kanuni hizo ni wazi kuwa walioandika habari hizi kutoka Mwananchi na JF aidha hawakufanya utafiti wa kutosha, hawana ufahamu wa kutosha au walifanya makusudi kupotosha kama anavyosema Spika kwani ni wazi kuwa Kanuni za mwaka 2023 na zile za awali hazina tofauti yoyote, hivyo kuandika "BUNGE LIMECHAPISHA KANUNI MPYA" zinazowabana wanahabari sio sahihi kwa sababu kanuni ni zilezile kwa upande wa wanahabari na mabadiliko yaliyofanywa hayajawagusa kabisa wanahabari
 
Spika wa Bunge, Tulia Ackson ameongelea vyombo vya habari na kuwaomba waandishi hawapendezwi na habari za upotoshaji kuhusu Bunge kwasababu liko waz...

Tulia Ackson yuko JF, kuna thread moja anaipenda sana.. 😋
 
Wanabodi,
Hii ni Breaking News kutoka Bungeni Dodoma!. Baada ya Rais Samia kusema huwa anaingiaga JF, kutusoma na kubaki akicheka. Leo kwa mara ya kwanza mtandao numero Uno Tanzania...

Duh, Paskali na Melo macho yanaelekea kuisha kabisa, jamani muwe makini na brightness za Smartphone, laptops, ipads or desktops, zinaua sana macho, kuweni makini mjue jinsi ya kuadjust brightness, hasa usiku na fonts za maandishi ziwe kubwa kusomeka kirahisi, la sivyo miaka michache baadae watu macho hakuna humu.
 
Sioni maana kwao kusema kila siku wanaifuatilia JF wakati hawayafanyii kazi kwa uzito stahiki yale yanayoandikwa humu ndani na wadau.

Hizi sifa wanazotoa mfululizo nikizitazama kwa makini sasa naona ni kama kuzubaishana tu.

JF imekuwepo Tanzania karibia miaka kumi na tano [15] toka sasa, sio kweli kwamba awamu hii ya Samia ndio wameanza kuifuatilia.

Walikuwa wakiifuatilia toka mwanzo, hata na wengine wao walikuwa member humu, tatizo uoga wao ndio uliowafunga midomo kusema haya wanayosema sasa, na wanafanya hivyo kwasababu bosi wao ameshawaonesha njia..

Nategemea after some days ataibuka mwingine nae aseme anaifuatilia JF, halafu tuendelee kushangilia kama kawaida yetu!.
 
Wanabodi,

Hii ni Breaking News kutoka Bungeni Dodoma!. Baada ya Rais Samia kusema huwa anaingiaga JF, kutusoma na kubaki akicheka. Leo kwa mara ya kwanza mtandao numero Uno Tanzania, Jamiiforums, leo imetajwa rasmi Bungeni na Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson " Vyombo vya Habari Mwananchi na Jamiiforums, Tunawategemea" Kutusaidia Kuihabarisha Jamii taarifa sahihi za Bunge"
Mkuu Mwenzangu ninakuunga mkono maneno yako unayo yasema hata mimi ni Member wa zamani sana karibu Miaka 14 iliyopita. Tuwe tunatoa habari zinazo husu bunge ziwe habari za uhakika sio kuleta mambo ya kufitinisha bunge na Wananchi tuwe makini kutoa taarifa za habari za bunge kwa Wananchi. Kwani viongozi wakuu wa nchi wanatufuatilia nyendo zetu hapa Jamii forums asante sina zaidi ya hayo niliyo yasema .
 
Korido za JF ni nyingi humu tunapigana vikumbo na watu wazito, wanyonge, matajiri kwa masikini, wenye mamlaka na wasio na mamlaka, mapadre jwa wapagani. Majambazi na vibaka bila kusahau matapeli.

Kifupi ni kama ka state /society fulani hivi inayoishi mtandaoni

Kweli kabisa JF ni Kama ka secret society fulani hivi.
 
Back
Top Bottom