Tulilalamika sana siasa kuingilia Utendaji. Sasa tumeanza kuvuna matokeo yake

Du!!!!!....
 
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.




Siungi mkono hoja
 
Andiko Bora kabisa hili. Nipo mkoa Fulani Kwa kazi Fulani, huyu Boss anasema oogh huwezi kwenda kufanya KAZI huko Hadi tukupatie Afisa Mawasiliano maana tunataka kila sehemu CCM alimaanisha Serikali, itajwe kila kwenye shughuli
 
Yule mabasi ya kijani yamedhihirisha yasemwayo
 
Haya Mawazo ya ajabu mno mno
 
Huu ni ukweli mchungu lakini utabaki kuwa ukweli tu, nakumbuka wakati ule CDF alipoonya kuhusu wahamiaji haramu kujipenyeza hadi kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi katika serikali yetu wengi waliponda na kumkejeli. Ukicheka na nyani utavuna mabua.
CCM wameharibu Nchi, sasa hivi chochote kinachofanywa ni Kwa maslahi ya CCM ibaki madarakani
 
Magufuli alifanya kwa ukubwa ujinga alioanzaga kuufanya Kikwete

Kuna ujinga mkubwa sana huwa unafanywa kumuondoa huyu jamaa kwa mauchafu yote ya nchi hii, inathibitisha udogo wa IQ za watanzania, tupo kama kuku yani, unateseka kwa njaa mwaka mzima ukija kupewa debe la mahindi siku ya mwisho na yuleyule aliyekutesa unasahau yote na kumuona ni malaika!
 
Magufuli ndiye aliyeingiza watendaji wengi nje ya mfumo bila kuzingatia uwezo. Magufuli ndiye alitengeneza compromise na Ofisi ya Taifa ya ukaguzi kwa kumwondoa Assad kwa nguvu
Yes Magufuli alifanya kwa sehemu kubwa haya ila mwanzilishi alikuwa Jakaya Kikwete
 
Hizi ni fikra mgando. Upinzani umeshakomaa vya kutosha kuweza kuiongoza Tanzania.

Kikubwa lazima tupate KATIBA MPYA kwanza maana bila hii tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.
 
Nchi hii magufuli aliikosea sana aisee!! Ni vile tu Watanzania wanapenda kuangalia vitu juu juu. Watanzania ni watu wa kuzuzuka na vitu vidogo vidogo ambavyo havina Future. Ila kwa watu wenye maono na jicho la kuona mbali watakubaliana na Mimi kwamba magufuli ametuharibia nchi.
 
Saana. Ila upuuzi huu ulianza hata kabla yeye hajawa Rais kipindi cha Jakaya Kikwete.

Magufuli alifanya tu na kupitiliza na matokeo yake ndo haya tunayaona leo.
 
Umewaza mbali sana mkuu ( nakuunga mkono) lkn huu udhaifu unaoonekana wa vyama vya upinzani unatokana na mfumo wenyewe hauko tayari kutengeneza /kulea chama mbadala wa ccm.
Vyama vya upinzani vinafanya kazi ktk mazingira magumu sana ya kuhujumiwa na mifumo usisahau Hilo pia, japo nimekuunga mkono kwa hoja Yako.
 
Yule mabasi ya kijani yamedhihirisha yasemwayo
Ajirekebishe. Akakae na Wastaafu wamwelekeze.

Taasisi anayoiongoza ni nyeti sana na ndo imekuwa inayotegemewa baada ya wanasiasa kuziharibu TISS na Polisi.
 
Jaribu kutofautisha kufanya kazi kwa sifa au ili uonekane unafanya kazi na kufanya kazi kwa weredi.

Nafasi za Utendaji kama Katibu Mkuu ( Permanent Secretary) ni nafasi nyeti sana.

Mahali tuliporithi mfumo huu (Uingereza) watu hawa hawaondolewi hadi wanapostaafu. Ndo Think Tank wa Mawizara na Inachukua muda mrefu sana kumtengeneza mtu hadi anafikia nafasi hiyo.


Watu hawa ndo wanafanya tafiti kuhusu sera na kushauri kwenye maamuzi makubwa ya kitaifa kwa mamlaka. Wanatakiwa wawe watu wenye competence, integrity, experience na exposure za kutosha. Watu hawa huwa wenye exposure na ndani na nje ya nchi na huwa wanatengenezwa ndani ya Serikali humo humo.

Unapomchukua kijana au mtu kutoka Chama cha Mapinduzi ambaye hajui hata utumishi wa Umma, au katoka tu chuoni au katoka kufanya kazi Chama cha Mapinduzi tu unampa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu au DED unadhani kwenye masuala nyeti anayoletewa na anapaswa kufanya analysis kubwa na kufanya maamuzi mazito atafanya maamuzi gani?

Yanayosemwa huko Serikalini yanatisha. Ngoja tukae kimya kuwalinda wenzetu walioko huko.
 
Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana huahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), a.k.a chawa tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo

Tumefika hapa tulipo kwasababu ya kuongozwa kwa tabia ya unyumbu, (unyumbu wa kisiasa)

Tunaishi kwenye jamii ya kanyaga twende yaani jamii ya bora liende jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi pia unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…