Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Hebu angalia yaani wanampangia maisha mtu mwenye mali yake

Kuna siku cousin yangu aliita usaili wa madereva garage
Madereva wakajitokeza, wakiwa wanasubiri kuitwa wakawa wanaongea zao
Hapo alikuwa amekaa mtoto wa boss akiwasikiliza na kucheka kwa story zao
Basi akaja dereva mtarajiwa akakaa nae basi kwa ukiherehere akawauliza waliomtangulia akasema jamani kuna upigaji lakini hapa au ni ka mshahara tu?
Yule dogo mtoto wa boss akaenda kumtonya anaefanya interview
 
Kama Boss muhindi acha anyooshwe ila ninavyojua ukiona mfanya kazi anakusifia kama boss inabidi ujitafakari sana.
 
Safi sana watu wote wakiwa kama wewe hawa madalali majambazi watanyooka.
 
Yaani umelenga humohumo.
Na kama unataka kupanga nyumba, jua wanakuja madalali kama 6 hv.
Hiyo madalali kuwa wengi unakuta dalali wako wa kwanza hana nyumba so chain inaanza kila anayepigiwa kama hana nyumba anampigia mwenzie ndio unakuta wanafika mpka sita....mdalali me nawapaga nusu ya hela ninyolipa kodi nikivurugwa mpaka robo.
 
Mzee wangu kila mtu ana-past zake hizo ndio past zangu tena wala sio mbaya kivile ni vile wabongo wa JF ni malaika wanaishi mbinguni.
Kuna majizi humu mpaka wa silaha, ila akichangia utafikiri ustadh
Kweli wengi wanajipamba tu na kupinga na katu hawasemi ukweli
Kama wote tungekuwa wema humu kama wanavyojiweka watu basi tusingesikia mauwaji wala ujambazi wala umalaya maana tungekuwa tuko na maisha kama Ulaya vile
 
Hiyo madalali kuwa wengi unakuta dalali wako wa kwanza hana nyumba so chain inaanza kila anayepigiwa kama hana nyumba anampigia mwenzie ndio unakuta wanafika mpka sita....mdalali me nawapaga nusu ya hela ninyolipa kodi nikivurugwa mpaka robo.
Hela robo🥺🥺
We jamani, utaua watu na familia zao ujue
 
Sometimes madalali (mawinga) Ni muhimu sn ili ufanye biashara,hasa kwa majiji na maeneo mengn yenye mzunguko na ushindan mkubwa sn WA biashara Kama dar n.k

Unapowakwepa madalali, uwezi Kuuza na utasingizia sn unarogwa Ila hamna Hata uchawi.

Ni hivi
Mtu anapokuletea mteja sio kwamba hakuyaona maduka mengine, Bali anajua Kuna namna flani anafaidika na Wewe kuliko akimpeleka mteja kwingine.

Nna biashara ya hardware na electronics. Ila udalali wangu naufanya Sana na mafundi (mafundi electronics,umeme na maji na ujenzi)

Kwenye biashara zangu Huwa nna Bei mbili, Bei ya mteja na Bei ya fundi Kwa Kila bidhaa inayouzwa.

Mafundi nawauzia Kwa Kila bidhaa Kwa Bei ya JUMLA Hata kama wakinunua kwa reja reja.

Hii hunisaidia kupata wateja wengi maana fundi akileta order labda ya laki 5 Hadi mil 1 hakosi total elfu 50 Hadi laki kutoka kwny punguzo analopata Kwa kila bidhaa mteja aliyonunua.

Binafsi inanisaidia Sana,
maana Hata nikichelewa kufungua, mteja kwangu haruki,ntapigiwa sim na fundi nije chap kumhudumia, maana kwingine fundi akimpeleka mteja anaondoka mikono mitupu.

Anabaki kusubiria Ela yake ya ufundi kwny Kazi itakayofanyika.

Fundi Yuko radhi cement itoke k'koo mpk chanika ili mradi TU anauhakika Kila mfuko ukiuza,kwake anaingiza 500 yake.

Boss ukihoji Kwann cement itokee k'koo na Bei ni Ile ile, utaambiwa maduka ya mbagala na chanika wanauza cement feki , iliyoexpai au haitimii kg 50.

Sasa kama boss wee,
Either ufuate ushauri wa fundi wako ujenge kitu imara fundi wako aishi au uokoe gharama fundi wako alale njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…