Tuliopitia Vita Na Chuki Makazini Tushirikishane Hapa

Brother umeni furahisha sana.
Ukawapiga ndoige!!
 
Nakumbuka 2021

Nimeanza kazi boss ananipenda sana basi kila idea za michongo naropoka tu aamue yeye kuzifanya au kuacha, nikiona wazo zuri la kuboresha clinic yake namfungukia tu bila wasi wasi .....

Miezi michache baadae wateja/wagonjwa wakawa wananikubali basi jina lina kuwa kwa kasi ya ajabu kupita wale nilio wakuta hapo nna miezi mitatu boss ananiita pembeni na kunifanya kuwa mkuu wa idara

Mimi natumia nafasi hiyo hiyo kubanana tuongezeane mshahara nae bila hiyana anafanya ivo .... shida inakuja baadae nilianza kuuza vifaa tiba nikiwa eneo la kazi then ikaleta conflict of interest... ikumbukwe kuwa mwanzoni nilileta wazo kwa boss ila hakulifanyia kazi.....

Wiki mbili mbele nkachukua faida kidogo na kilie kiji akiba kwenye mshahara nikachanga ninunue ka vitz bhana wee..... songo mbingo likaanza

Kazini nashinda asubuhi mpaka jioni nnahitaji leseni kwaajili ya baby walker nikatenga muda ijumaa baada ya kazi nikimbie TRA mara moja Kisha nirudi, loooh!
Mke wa boss (mpare) ananambia umetoka kazini hapa sio getto kwamba ujiingilie na kutoka.... kwa heshima na kuepusha migogoro nilirudi mchana ule nikabadilisha uniform na kutoka kazini ili nirudi kesho hali ikiwa imetulia.

Kumekucha nirudi kazini nakutana na work mate mwenyeji wangu (mfipa) ananambia hapa boss kasema ukija usiguse chochote mpaka yeye atakapo sema.

Haya nimekaa home week nzima siitwi nampigia cm boss ananiambia Kwan nn kinaendelea kima yule kama hajui...

Akanipa appointment tuonane j3
Nimefika akanipa sababu za kipumbavu za kukatisha mkataba
1.umemjibu vibaya mkurugenzi wako (mke wake)
Sikufaham kuwa mke wake ni mkurugenzi maana sikutambulishwa wala hakuhusika katika mchakato wa kuniajiri pia siku tambua majukumu yake wala kwenda ku report kwake.

2.natangaza kuwa nnalipwa mshahara mkubwa. Sikuwahi fanya ivo....
Pili kwani kuna ubaya kujivunia matunda ya ujuzi wako kuna sehemu yoyote katika mkataba inayo zuia kufanya ivo?

3. Eti nauza vifaaa ili hali kuwa nayeye pia anauza vifaa .... lakini muda huo hakuwa na stock yoyote na hakuweza jua ni vifaa gani vilivo kuwa na uhitaji kwa muda ule ndio maana tukavileta.


Nilicho jifunza

1.usiwapende na kuwaamini wote kazini
Boss nilimwona kama baba ❌

2.usioneshe mafanikio yako we walilie shida tu hata kama unacho hii itafanya boss pia ajiamini kuona atakutawala milele

3.marafiki wa kazini ni wanafiki tenga muda ujifunze unafki pia ila usiwe mfitini.... hii itasaidia kuweza kuzichapa ki intelijensia ukiwa hapo hapo kazini

4.fanya kazi masaa ya kazi tu hizo extra hours nenda kafanye kazi kwingine fanya kazi zako vizuri na kwa ufanisi wa hali ya juu ila usiifanyie zaidi taasisi .... hii itasaidia hata siku ukifukuzwa usipate maradhi ya moyo au sonona.

5.usiwe na mpenzi/wapenzi kazini.... maana hii huleta wivu hata kwa wafanyakazi wenzio kama kuna mwanamke anakukubali ataanza kuleta wivu au kama kuna mtu alivutiwa na huyo ulie nae atakuletea shida pia ( hapo juu kipindi jina limekua nilitafuna piss kali sana kias kwamba mpare mmoja MD alifurahi sana alipoona nmeachana na ile yule dada) sema tulio soma Cuba tukaelewa shida yake ilikua nini maana hata tulipo kuwa tukienda kulewa na jamaa alikua anampigia cm yule dada niongee nae mbele yake kima yule.

6.Marufuku kunywa pombe na work mates wako hii itakusaidia sana kufanya wasikujue.
 
Sio kweli hakuna watu wako peace kama wafipa,mm nafanya kazi unyakyusani Cha moto nakiona mm Nina upendo na Kila mtu lkn hii mijamaa imezidi ukabila na roho mbaya.
Hawa wapumbavu ni wabaguzi sijapata ona.
Mm naona issue hii ipo kwa kila kabila ila namna ya Kuvunja hizi kero ni kujifanya kama wao ..... unakumbuka vile wanasema when in Rome be roman sio vinginevyo...
 
Noma sana
 

Wewe ndo sababu ya fitina zote. Hizo sio fitina, ni malipo ya matendo yako. Maama halifi ya fitina ni kutokuhusika na kusababisha.
 
Uko sahihi dada angu anafanya KAZI Kwa wahindi mpk Leo hawajui km ana nyumba wakifanga renovation nyumba zao wanampa milango na Baadhi ya furnitures akauze ye anaenda kuweka kwake wanaamini Kwa mshahara wake hawezi Jenga Yaani akienda kazini Yuko very low key,anaomba Kila siku Kwa wale wadosi wanampa
Kuna mmoja alifukuzwa KAZI na wahindi walipojua kua amejenga nyumba wakasema alikua anawaibia walimpeleka mpk polisi kua ni mwizi
 
Asehhh...pole sana watu walikupiga sayansi ya kiutamaduni ukasarenda
 
Sio kweli hakuna watu wako peace kama wafipa,mm nafanya kazi unyakyusani Cha moto nakiona mm Nina upendo na Kila mtu lkn hii mijamaa imezidi ukabila na roho mbaya.
Hawa wapumbavu ni wabaguzi sijapata ona.
Wanyakyusa hawana shida kabisa. Mimi ni mnyakyusa nafanya kazi kaskazini yaani natamani kurudi nyumbani tu maana hawa watu wa kaskazini especially wachaga wana roho chafu sana yaani itoshe tu kusema haya mashetani ni ma mbwa kabisa
 
Wanyakyusa hawana shida kabisa. Mimi ni mnyakyusa nafanya kazi kaskazini yaani natamani kurudi nyumbani tu maana hawa watu wa kaskazini especially wachaga wana roho chafu sana yaani itoshe tu kusema haya mashetani ni ma mbwa kabisa
Mkuu tunaomba kisa kimoja πŸ˜…πŸ˜…
 
Wanyakyusa hawana shida kabisa. Mimi ni mnyakyusa nafanya kazi kaskazini yaani natamani kurudi nyumbani tu maana hawa watu wa kaskazini especially wachaga wana roho chafu sana yaani itoshe tu kusema haya mashetani ni ma mbwa kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…