Tuliopitia Vita Na Chuki Makazini Tushirikishane Hapa

Nlikuwaga ofisi Moja hivi Ina wafanyakazi watano tu. Lakini wakitoka nje kula au kuwa field Kila mtu anamkandia mwenzake kuwa jau mara fitna. Mara mjuajiii. Nikachunguza sana nikagundua hapa ili uwe salama Bora uwe neutral.
Kuna kijamaa kikawa kinajifabza ndo kiongozi pale lakin mshahara ukitoka anaitwa mwingine kabisa kwenda kusaini na kuruhusu hela zitoke.
Nilichokuja kugundua kni kuwa binadamu tuna rangi nyingi sana. Sijui kama kinyonga anatufikia
 
Msala naopitia sasa hivi Mwenyezi Mungu ndio mjuzi wa yote
Don't give up mkuu ndio uanaume huo pendelea kusoma vitabu mkuu soma kiatabu kinaitwa the power of POSITIVE THINKING na the magic of THINKING big you will be fine mkuu nilishapitia huko kote mkuu ni kawaida hasa kwa wanaume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm wakat naanza kazi nilikuwa namla bosi nlchokuja kukosea et nkaajatoka na Staffmates nkawa nkagonga wote,,, bhana bhn msijaribu hii michezo makazini... Nlchukiwa na bos na kunyimwa kla aina ya fursa mpk nliomba uhamisho mwenyewe
 
Believe believe believe guys we have to believe and working harder.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilifanya kazi na "WAPALE" kwenye ofisi Moja

Aiseee Hawa watu ni noma sana aisee

Sitakuja kusahau jamaa ni wanafki sana

Yaani ni hatari...Wana majungu sijwahi ona...
Ndicho kinachonikuta mimi kwenye hili kabila.Aisee kaa mbali nao na hili kabila kabisaaa
 
Kiufupi waafrika hatupendani kuna ile story ya HR wa barrick gold mine kuwalipa pesa kiduchu wafanya kazi licha ya management kuidhinisha pesa kubwa ila HR alikataa akasema kama hawataki tutaleta wengine ndio utajua wabongo jinsi tulivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! inasikitisha sana aisee,roho mbaya haijengi kabisa,kwa style hii,hayo maendeleo yatakujaje sasa?
Poleni sana mkuu.
We acha tu mkuu nilipoenda sehemu nyingine nikapewa nafasi ya assistant nikakataa nikapendekeza mtu mwingine management ikakataa na mpaka leo boss akiondoka ofisini ananiachia mimi na barua ya kuondoka nafanya hvyo hvyo japo kishingo upande kwasababu mimi napenda sana uhuru na nina experience mbaya sana na uongozi baada ya kumuona mtu anaacha kazi ya million 15 salary per month kwasababu ya fitna na majungu nachukia sana uongozi sema kuna mazingira hamna namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Skilizia. Kwa kuwa ashajua unataka kusepa atakuwekea mambo flan flan sawa ili ukae kama anakuhitaji. So jipe muda kidogo uangalie upepo.
 
Aisee pole sana.
 

Unapoenda officin kumbuka wale ni work mates sio friends. Nilijifunza hiki kitu mapema mno maana yalinikuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…