Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Hapo wagombea wote waliokata rufaa ni wapinzani, maana yake kwa vyovyote vile watakaoumia ni wapinzani, hata kama wapo watakaorejeshwa kugombea lakini kwa hao ambao hawatarejeshwa nalo bado litabaki pigo kwa upinzani.

Hivi kwanini hakuna mgombea wa CCM hata mmoja aliekatwa? au wao walienda kusomea wapi kujaza hizo fomu? Tume iwaache wagombea wote sanduku la kura ndio likaamue.
Hapo ndio huwa inashangaza y not ccm hata mmoja asiwepo aliyekosea kujaza hizo form? ?
 
Kuna mtu yeyote mwenye taarifa ya hatima ya Meya Jacob wa Ubungo?
 
Hapo bado la kutafuta tunalitafuta.

Suruhu hapa ilikuwa kuacha sanduku la kura kufanya kazi yake.

Ushindi wa mezani wa nini?

Kwanini mlikosea na mnataka tume iwabebe?
 
NEC inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, na haipo pale kufanya hisani ya nani arudi nani akatwe.
Tume imefanya kazi yake kwa kuzingatia vielelezo vilivyo tolewa na kutoa maamuzi
Nakubaliana na wewe maana hivi NEC ipitishe tuu watu hata kama hawana sifa? Tuwaachie NEC wafanye kazi yao.
 
Nguvu ya umma mitandaoni?

Lisu aliwahamasisha muandamane nchi nzima kushinikiza wabunge walioenguliwa warudishwe, lakini mmeishia kuandamana humu mitandaoni huku wenzenu wana wabunge 20 tayari!

Haya hiyo nguvu ya umama au umma?
Usiombee hiyo kitu ndugu, na wala usitambe wee omba haki itendeke tuu.
 
Iwarudishe wote wakapambane uwanjani hakuna ushindi mezani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutoa matokeo ya rufaa za udiwani na ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi mkuu wa 28 Oktoba 2020.

Leo tume imetoa matokeo ya rufaa 55 kama ifuatavyo...
 
Nikionaga jina NEC namkumbuka yule mtalaam wa Zanzibar 2015, ZECHA sijui JECHA😂
 
akasema najua wa hapa washapita labda kwingine huko ndio watarudishwa.

Vipi wewe.. hujui ya kuwa na IMANI.. yapoje!!! au ndio kuwa mfuasi wa chama kilicho.. ndani ya futi sita.. unajikoronga.. kama vile Magufuli alikuambieni.. mutende mliyotaka.. na kumsema sema tangu awatumbue majipu kwa kila namna.. mimi kwandika kutamu.. ndugu pokea hizi mapema 💉💉💉💉za tarehe mbili nane hutakuwa imezikimbia..😀😀😀😀

Mulitaka aongee kwa uoga.. museme hajiamini.. 😀😀😀😀

Magufuli jembe.. yeye ni anashusha nondo kwa kujiamini..

Upinzani munampenda kupita kumsikiliza Rais Jembe aliyeweka historia tele nchini..

wengine tushaamua kura ni zake..

Njoo ujiunge nasi ndugu.. 😀😀😀
 
Ndiyo maana,siku alikuwa na kikao cha kutumbua,akisema, naona mahakama Kuna watuhumiwa wa ufisadi wapo magerezani kwa muda mlefu,hivyo kama kuna namna ya kufanya,ingefaa mahakama ikae na watuhumiwa,kama itafaa waone Hindi watuhumiwa wenye uwezo wakulipa waelewane ili waachiwe.

Kesho yake tuliona mahakama ikufanya sensa nchi zima kwa watuhumiwa wakaanza kukadiliwa Ida's ya pesa wanazotakiwa kulipa kulingana na kesi,mwisho wengi wao waliachiliwa.
Hivyo mihimili yote gaiko huru,ipo mfukoni mwa mtu mmoja.
Nadhani Marais wengi wanakuaga na Veto, kwani Rais ndio msimamizi mkuu wa Mambo yote ya nchi hii Kwa niaba ya wananchi..so sometimes anaweza kutoa maamuzi ya mwisho pamoja na kuwa pardon wale waliohukumiwa kunyongwa . Kosea kuchangia mbunge sio Rais.
 
Leo asubuhi Magufuli wakati yuko Misungwi amesikika akisema hapa kuanzia Mbunge hadi Madiwani wamepita bila kupingwa. Na akaenda mbali zaidi na kudai najua kuna mapingamizi yako Tume ila kwa dharau akasema najua wa hapa washapita labda kwingine huko ndio watarudishwa...
Hakuna tume huru sema tume ya magufuli
 
Leo asubuhi Magufuli wakati yuko Misungwi amesikika akisema hapa kuanzia Mbunge hadi Madiwani wamepita bila kupingwa. Na akaenda mbali zaidi na kudai najua kuna mapingamizi yako Tume ila kwa dharau akasema najua wa hapa washapita labda kwingine huko ndio watarudishwa...
Hakuna Tume hapo,ni kamati ya uchaguzi ya sisiem.
 
Binafsi nitasikitika sana na ubabe unaofanywa na Tume ya uchaguzi ya awamu hii. Kusema ukweli awamu zilizopita hayakuwepo haya madudu. Hata kama yalikuwepo ila sio kwa uwazi na ubabe wa nje nje kwa namna hii.

Hapo awali wagombea waliweza kupita bila kupingwa endapo mgombea mwenza kajiengua au kaacha kurudisha form. Sasa hii tume ya leo inakutaftia kosa ili ikukate na mgombea wanaotaka apite bila kupinga.

Hii ni kama vile Tume ndyo inatuchagulia viongozi na sio sisi kuchagua viongozi tunaotaka.

Swali la msingi kujiuliza hapa ni, "Kama leo tume inataka ikukate usigombee je ukigombea ukashinda itakutangaza?"

Hii tume inakotupeleka ni kubaya.
 
Kwanini mlikosea na mnataka tume iwabebe?

Tulikosea wagombea wakawa wanashikiliwa na polisi ili muda upite?

Mkururo wa udhalimu ambao utarekebishwa kwenye serikali ya haki ya Lissu ni pamoja na hizi:

Mamlaka (polisi, tume, mahakama nk) kuwajibika kwa watu.

Tuyaonayo haya ni matokeo ya mamlaka kuwajibika kwa watawala.

Kumbuka kwa yote haya mnatukumbusha zaidi umuhimu wa haki, uhuru na maendeleo.

Mwaka huu tutaelewana tu.
 
8 September 2020
Dar es Salaam, Tanzania


NEC YAWAKATA 15 KUGOMBEA UBUNGE
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akitoa taarifa kwa Umma kuhusu zoezi la kupitia na kufanya uamuzi wa rufaa za Wagombea Ubunge leo Septemba 8, 2020 Jijini Dar es Salaam.

Kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, kinatoa fursa kwa wagombea wa Ubunge kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.

Zoezi la kuzijadili na kuzitolea uamuzi rufaa hizo linaendelea na kuanzia leo, Tume itakuwa inatoa uamuzi na kuwajulisha wahusika kwa kadri rufaa hizo zitakavyokuwa zinamalizika kushughulikiwa. Leo Tume imetoa uamuzi wa rufaa 55 za wagombea Ubunge kama ifuatavyo:

i. Imekubali rufaa 15 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea.

ii. Imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa.

iii. Imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.

Tume imechambua vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa vilivyowasilishwa ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa Mujibu wa Sheria na kanuni za Uchaguzi.

Uamuzi uliofanywa na Tume katika rufaa hizo umewarejesha baadhi ya warufani kwenye orodha ya wagombea. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kuanzia leo, kesho na kuendelea.

Wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume kuanzia leo.
 
Siyo huru alafu mnaendelea kupiga kampen nakujiita mmeshashinda?
Kwa hiyo mnafanya makusudi ili watu wawasusie? Mwaka huu mpaka kieleweke! Kura zikijaa mkataka kuziiba tunaingiza raia barabarani pumbavu nyie!
 
Back
Top Bottom