Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Mhe. Tundu Lissu Kunguruma leo kwenye ofisi za Uchaguzi Dodoma akirejesha Form ya Kugombea Urais wa Tanzania

Updates
----
Tayari Mweshimiwa Tundu Lissu ambae ni mgombea urais na makamu wake Salum Mwalim wameshafika kwenye ofisi za tume ya Uchaguzi kwa urejeshaji wa Form

UPDATE:-
Tumehifadhiwa kwenye holding room ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa Dodoma kusubiri kuitwa ndani kwa ajili ya uteuzi!

UPDATE:- 9:40
Mgombea wa CCM John Pombe Magufuli hakumali nusu saa kwenye Tume na fomu zake zimepokelewa, akateuliwa na kuondoka. Sisi wengine fomu zetu zinakaguliwa tangu saa sita mchana kwa utaratibu gani wa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge? Upendeleo huu wa nini?
10:13
Kwa ajili ya kusimamia utaratibu wa kisheria, fomu za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA mhe. Tundu Lissu hazikupita kwa Wasimamizi wa Majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya zoezi la uhakiki. Zoezi la uhakiki ndio linaloendelea kwa sasa.
Magufuli bado ni rais unataka akae foleni kama lisu
 
Mgombea Urais Uchwara Tundu Lissu ameanza kupatwa na homa ya kushindwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, kabla hata kipenga hakijapulizwa baada ya kugundua asilimia kubwa ya Watanzania wanamuunga mkono Dkt. John Pombe Magufuli.

Lissu anajifanya yeye ni msomi wa Sheria lakini nashangaa ni Mwanashera gani wa hovyo huyu ambaye hajui umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa na Tume ya Uchaguzi.

NEC iliweka utaratibu wa Wagombea Urais kurejesha fomu na kila mgombea Urais aliyerudisha ambaye amekidhi vigezo na taratibu amepitishwa kuwa mgombea kwenye Uchaguzi.

Lissu analalama eti Rais Magufuli amependelewa, tukwambie Lissu, Magufuli hapendelewi ila anafuata taratibu zilizowekwa, wewe uliamua kutofuata taratibu ndiyo maana ulianza Kampeni kabla ya wakati sasa tulia dawa iingie.

Kiufupi Lissu wewe ni mtovu wa nidhamu wa kutofuata taratibu na Sheria zilizowekwa, akiondolewa kwenye kugombea Urais atasema Rais Magufuli anapendelewa wakati ni upuuzi wake.

Lissu ukome kumsakama Rais Magufuli fuata taratibu hauko juu ya Sheria
Nyie ndio wauwaji na wachawi.
 
MWAMBA KATEULIWA kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Sasa mjiandae na kupiga push-ups jukwaani... sasa tunasubiri kujibu mapingamizi (amblyopia tunajua yapo mengi tu kkutoka kwa watu waoga).. #TunduLissu2020 #nohatenofear @TunduALissu
Yani nina furaha kubwa mno kuliko maelezo!

Sasa ngoja tusubiri wale walioko nje AKA wasiojulikana wana mpango gani!

Siyo siri ccm wanaenda kwa style ya ku “beep”, hawajui nyakati zishawatupa mkono.
 
Back
Top Bottom