Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Miiko ya Maadili!
Mimi nachoomba mheshimiwa Lissu anyoe nywele zake zifananane na utamaduni wa nchi yetu! The way alivyonyoa haimpi status kimaadili kama anaweza kuwa Rais wa nchi yetu!

This is too personal!!

Kiukweli tangu mheshimiwa Rais kaanza kuondoa mpaka ndevu zake za asili namuona sio halisi!!

#personalopinion
 
Baada ya tamko la katibu, Mwenyekiti amesema tume ya Taifa ya uchaguzi baada ya kujiridhisha kuwa kiti cha Rais na Makamu wa Rais waliopendekezwa na CHADEMA wametimiza masharti tume imewateua ndugu Lissu, Antipas kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na ndugu Mwalimu, Salum kuwa mgombea wa makamu wa kiti cha Urais wa Tanzania.
Wallah Leo sirudi home, nalala nje kwa raha! Potelea mbali, sio kwa raha hizi, nyenyenyenheeeee sshenzy kabisa!
 
Tundu kama Tundu, Toto Tundu, Toto Tukutu...sixteen bullets In and Out of the body but still rolling like a desert stone...piiiiiipoooooooooooooz!!!!!!

huwez kuzuia mama wa mimba ya miez tisa asizae...muda ni ukuta....and to you jiwe[emoji117]....Mene mene tekeli na peres

Umkhonto we Sizwe...Mkuki wa Taifa...aluta continue....piiiiiiiiiiiipoooooooooooooooooooz!!!
Endeleeni kuota tu

Sent from my DUB-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna taarifa kwamba kishapitishwa, je atakuwa salama usiku huu? Je, kama kweli kapitishwa wahuni wa maccm hawatamuwekea pingamizi ili aenguliwe!? Tusubiri tuone.

Inavyosemwaa...
Walikuwa wanasubiri usiku ufike waweze kumteka na kumpokonya hizo fomu.
Subirini
 
Miiko ya Maadili!
Mimi nachoomba mheshimiwa Lissu anyoe nywele zake zifananane na utamaduni wa nchi yetu! The way alivyonyoa haimpi status kimaadili kama anaweza kuwa Rais wa nchi yetu!
Magufuli wakati anaanza kushika madaraka ya urais alikuwa anafuga ndevu na kuziacha kama ndanda Kosovo baada ya muda akaacha.

Hata lisu kuna mambo atayaacha akiwa Rais
 
Kuna taarifa kwamba kishapitishwa, je atakuwa salama usiku huu? Je, kama kweli kapitishwa wahuni wa maccm hawatamuwekea pingamizi ili aenguliwe!? Tusubiri tuone.
Shibuda na Lipumba wamepewa Dola laki nne advance wamuwekee pingamizi
 
Mhe. Tundu Lissu Kunguruma leo kwenye ofisi za Uchaguzi Dodoma akirejesha Form ya Kugombea Urais wa Tanzania

Updates
----
Tayari Mweshimiwa Tundu Lissu ambae ni mgombea urais na makamu wake Salum Mwalim wameshafika kwenye ofisi za tume ya Uchaguzi kwa urejeshaji wa Form

UPDATE:-
Tumehifadhiwa kwenye holding room ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa Dodoma kusubiri kuitwa ndani kwa ajili ya uteuzi!

UPDATE:- 9:40
Mgombea wa CCM John Pombe Magufuli hakumali nusu saa kwenye Tume na fomu zake zimepokelewa, akateuliwa na kuondoka. Sisi wengine fomu zetu zinakaguliwa tangu saa sita mchana kwa utaratibu gani wa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge? Upendeleo huu wa nini?
10:13
Kwa ajili ya kusimamia utaratibu wa kisheria, fomu za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA mhe. Tundu Lissu hazikupita kwa Wasimamizi wa Majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya zoezi la uhakiki. Zoezi la uhakiki ndio linaloendelea kwa sasa.
UPDATE:- 1:00 Usiku

I'm the only candidate who toured the country, met with actual voters and got their endorsement in person. All other candidates obtained their nominators from NEC registers without having to meet actual voters. Yet I'm the only candidate whose nomination is still under a cloud! - LISSU

1:03 Usiku - NEC
Mgombea mwenza wa CHADEMA, Bw. Salumu Mwalimu akishuhudia zoezi la uhakiki wa fomu za uteuzi za chama hicho. Zoezi hilo linaendelea Ofisi za Tume, Njedengwa, Jijini Dodoma.

UPDATE: 1:40 - LISSU APITISHWA
Katibu wa tume ya uchaguzi amesema wagombea wa Rais na Naibu Rais kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) wametimiza sifa na masharti ya uteuzi.

Baada ya tamko la katibu, Mwenyekiti amesema tume ya Taifa ya uchaguzi baada ya kujiridhisha kuwa kiti cha Rais na Makamu wa Rais waliopendekezwa na CHADEMA wametimiza masharti tume imewateua ndugu Lissu, Antipas kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na ndugu Mwalimu, Salum kuwa mgombea wa makamu wa kiti cha Urais wa Tanzania.

Haya Sasa wanachadema msimuangushe mgombea wenu, maana mlikuwa na woga kuwa jina lake litakatwa na NEC, Nendeni mfundisheni namna ya kuwasilisha hoja zake.
 
Quote me; chochote kinachofanyika Tanzania, kinafanyika kwa mapenzi ya Serikali na vyombo vyake. Tena ni baada ya kujiridhisha ya kwamba HAKUNA madhara. Lissu kugombea kama ilivyokuwa kwa Lowassa, tayari Serikali imeishajiridhisha HAKUNA madhara. Tukutane baada ya Oktoba 28!

Hivi hii nchi ni ya nani? Na nani mwenye haki zaidi ya mwingine hata aamue nani awe nani!!

Kuna baadhi ya watu tukiwa kwenye ofisi za umma ama au taasisi na idara fulani tunajiona tuna mamlaka ya kufanya chochote tutakacho.

Haiko hivyo, hii nchi ina sheria na imesimamiwa na katiba.
 
Back
Top Bottom