Jaribio la Kwanza
CCM kimekuwa chama cha ajabu sana, ktk siku muhimu hapa nchini kama hii ya leo, kinathubutu kukosa subira na kuyatenda mambo ya hovyo kiasi cha kuogofya cha kuwahusisha makada wake kuchelewesha kwa makusudi haki kutendeka kwa wakati. Hivi huo uharaka wa kutaka kulazimisha kusikilizwa kwa kesi za muda mrefu za Tundu Lissu zilitoka wapi ktk kipindi ambacho kinafahamika kabisa ni chenye shughuli muhimu za kisiasa zinazotokea kwa nadra kwa ajili hatma ya Taifa zikiwa zinaendelea.
Jaribio la Pili
Kutaka kumtoa katia reli ktk kipindi hiki, haya ni matumizi mabaya ya vyombo vyetu vya dola. Hii ni mojawapo ya njia ya hovyo kabisa ya kutaka kuhujumu uchaguzi wa mwaka huu kwa kumpendelea mtu fulani. Hii ni dalili ya hofu kubwa ambayo inamnyima usingizi mtu fulani asiyejiamini.
Jaribio la Tatu
Kama kutaka kumpeleka mahakamani kwa njia ya namna ya kitekaji, hii itakuwa ni njia ovu ya kutaka kumuengua mtu ambaye anaonyesha kukubalika zaidi hata kuungwa mkono na watu wengi. Inatafutwa njia rahisi ya watu kupiga kampeni kwa kupiga "push ups" tu badala ya kujibu hoja ngumu kutoka upande wa ushindani. Mapingamizi ya namna hii ya kihuni HAYAKUBALIKI.