Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Urais, Fomu kuhakikiwa na Kutangazwa Kuteuliwa , kisha kusubiria kama kuna pingamizi

Baada ya fomu kuhakikiwa na kutangazwa kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa kila kitu kipo sawa kuna zoezi muhimu la kubandika majina ili umma kuwafahamu.


Muda wa pingamizi ni kuanzi saa 10:00 jioni ya tarehe 25 Agosti 2020 hadi saa 10:00 jioni siku inayofuata yaani tarehe 26 Agosti 2020.

Zoezi hilo muhimu ni hatua inayofuata ni kusikia kama wagombea wamewekewa pingamizi na wale wadau wanaotambulika na Tume ya Uchaguzi, kisha wagombea wateuliwa kupata nafasi ya kujibu.

Wenye haki ya kuweka pingamizi ngazi ya Urais na Makamu ni hawa wadau watatu yaani Mkurugenzi wa Uchaguzi, Msajili wa Vyama Vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pingamizi ngazi ya Urais linatakiwa kuletwa kwa maandishi katika fomu namba 9A na pingamizi hilo liwakilishwe ndani ya muda muafaka unaoanzia muda uliotajwa hapo juu na sababu za pingamizi litajwe.

Hivyo waliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ngazi ya Urais kama wateule baada ya kuhakiki fomu na nyaraka wote wanaweza kuwekewa pingamizi muda wowote kuanzia muda wa saa 10:00 jioni ya leo tarehe 25 Agosti 2020 na mwisho wa kuwakilisha pingamizi ni kesho saa 10:00 jioni tarehe 26 Agosti 2020.
 
Urais, Fomu kuhakikiwa na Kutangazwa Kuteuliwa , kisha kusubiria kama kuna pingamizi

Baada ya fomu kuhakikiwa na kutangazwa kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa kila kitu kipo sawa kuna zoezi muhimu la kubandika majina ili umma kuwafahamu...
Wamkate Lisu sasa.
 
Wengine wamejaza wadhamini wachache kazi rahisi kuhakiki Lisu kaweka wadhamini maelfu Tume kumaliza kuhakiki itachukua muda .Yeye ndie kasababisha hiyo shida.Wenzie walijaza tu idadi minimum inayotakiwa na Tume Ili uhakiki uwe rahisi na ichukue muda mfupi yeye kajaza wadhamini dunia!!
kuzihilisha kura anazo nyingi no kuchakachulia sbb atajua
 
Ebu tukumbushane Mkuu. Mwaka 2015 Lowassa alishindana na nani kuwa Mgombea Urais wa Chadema? Ahahahahahahah!

Uliona wapi nikishangilia Lowassa kuwa mgombea pekee? Acha tu hiyo kuwa mgombea pekee, hata hiyo tu kuwa mgombea wa Cdm tafuta kama niliwahi kushangilia.

Mimi ninasimamisha vizuri kama mwanaume, huwezi kunikuta nashangilia ushindi wa mbeleko. Ccm kwakuwa imechoka kushindana, ndio nyie bila aibu mnashangilia kupita kwa hila.
 
Uliona wapi nikishangilia Lowassa kuwa mgombea pekee? Acha tu hiyo kuwa mgombea pekee, hata hiyo tu kuwa mgombea wa Cdm tafuta kama niliwahi kushangilia. Mimi ninasimamisha vizuri kama mwanaume, huwezi kunikuta nashangilia ushindi wa mbeleko. Ccm kwakuwa imechoka kushindana, ndio nyie bila aibu mnashangilia kupita kwa hila.
Nchi hii bado hakuna chama cha kusimamia Serikali zaidi ya CCM. Kwahiyo, uwe unataka. Uwe hautaki, Serikali ya CCM itakuongoza tu Jana, leo na kesho. Jiandae tu Kisaikolojia.
 
Bagamoyo kama kawaida yako, hautuangushi. Unafanya kazi yako kwa weledi sana.

Ndiyo haki tunayolilia ya kupata na kubadilishana taarifa, habari na ufahamu maana vyombo vingine vya habari wamejipiga ganzi, hivyo sote kimbilio letu ni hapa JamiiForums kwa habari za kina na zenye vyanzo sahihi.
 
Vyombo vingi vya dola hawapendi uonevu wanaowafanyia wapinzani hata wakitumwa kwenda kuwanyanyasa wapinzani huenda kwa shingo upande
Nakubaliana na wewe kabisa,kwa sababu wote tunapigika sawa tu,Askari wote Wana ndugu ambao sio Askari hivyo wanaona machungu wanayopotia ndugu zao.
 
Jamii forum imewatisha NECCCM mpaka wakaacha ushetani wao wa awali ingawa sasa wameandaa ushetani wa pili kupitia pingamizi la Lipumba na shibuda
Hii komenti imekua ikijirudiarudia Sana,lakini watu hawaipi umuhimu Sana,Sasa nakuomba fanya jitihada zote kuwafikishia VIONGOZi wa CDM moja kwa moja,inawezekana walikua bize na kurudisha fomu,hawajui juu ya njama hizi juu ya Lipumba na shibuda.
 
Nchi hii bado hakuna chama cha kusimamia Serikali zaidi ya CCM. Kwahiyo, uwe unataka. Uwe hautaki, Serikali ya CCM itakuongoza tu Jana, leo na kesho. Jiandae tu Kisaikolojia.

Hata waingereza walikuwa wanasema watanzania hatukuwa tayari kujiongoza bali kuongozwa tu. Hivyo haya maneno yako yalikuwa yakitumika miaka na miaka kwa wafaidika wa mfumo. Narudia tena, kama ww ni mwanaume unayesimamisha vizuri, ni bonge la aibu kushangilia kupita bila ridhaa vya wananchi.
 
Back
Top Bottom