Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Kama unasaka uteuzi kwa uandishi huu pole sana hupati hata uteuzi wa kuwa house boy chato au chamwino
Inawezekana na wewe ni mmoja wanomeza lolote linalosemwa na Lissu bila kuangalia ukweli na sheria zinasemaje; nimewawekea sheria na kanuni hapo juu uone kama kweli Lissu alikuwa na ground yoyote. Niliwahi kuhudhuria mkutano mmoja wa Lissu pale DC mwanzoi mwa mwaka jana nilikuwa na shughuli nyingine mjini hapo, na niliposikia mkutano huwa watanzania, nikatafuta mda wa kuuhudhuria; ninamfahamu!
 

Mkuu Salary Slip wakati nwingine busara itawale chuki uliyonayo itakutia matatani nafsi yako. John Pombe Magufuli ni Rais anayemaliza muda wake, kwa maana hiyo anajua sheria, kanuni na taratibu za kugombea.

Ebu Mkuu jiulize:
√ Iweje leo asijue na kufanya kinyume?
√ Kama aliweza kupitishwa wakati wa awali asipokuwa na madaraka ya kutumia mwanasheria mkuu na hata wajumbe wa Tume kumwelekeza, iweje leo akiwa na madaraka ashindwe kuwatumia?

Lissu amedai Magifuli kaingizwa kwenye chaka, amini sasa ujuaji wake siyo kwamba umemwingiza kwenye chaka bali choo cha jinsi nyingine. Chuki yake dhidi ya Magufuli itaadhibiwa na wapiga kura, vivyo hivyo na wagombea wa chama chake. Chama chenye viongozi wa kupinga kila kitu.

All in all, shame on you.
 

Unamfahamu kwa huo mkutano mmoja tu?

Kama ndivyo akili yako inavyokutuma, unaweza kuwa na vinasaba sawa na vya nabii Tito kama si yeye mwenyewe

Vinginevyo labda ndiyo unatokea baa. Lala angalau pombe ikutoke kwanza upate akili mpya.

Usiku mnene saa hizi!
 

Kila kitu kipo wazi hapo juu. Soma kwanza kabla ya kuandika. Vipengele vyote vya sheria vimewekwa. Tume ndiyo imejibu jumla jumla kujilinda yenyewe na JPM baada ya kujichanganya. Lissu yupo sahihi kabisa.
 

Huelewi unachoandika.
 

Nimeshamsikiliza pia anavyooongea kwenye radio mbalimbali. Ile ya DC ninaisema kwa vile ilinigusa sana. Nilimwona zamani kidogo akiwa anatetea wanavijiji wa Nyamongo akiwa kijana mwenye nguvu sana.

Siku hiyo hapo DC nilimwona akiwa anatemebelea magongo nikiwa tayari najua kuwa alishambuliwa kwa risasi, kwa hiyo niliguswa kibinadamu nikajifikiria kuwa hiyo inaweza kunitokea hata mimi pia; ni experience iliyoniumiza sana. Ila ilipokuja maneno yake yalikuwa ni OFF kabisa; nilichoongelea hapo juu ni maneno anayotoa siyo yeye kama mtu binafsi.
 
Rais ana kazi kubwa sana ya kujenga nchi, hana mda wa kujadiliana na kichaa
 

Pana wengi wanamfahamu tokea o'level Arusha, A'level Tanga hadi UDSM. Wana account tofauti na yako kuhusiana na huyu bwana. Bado ungependa ya kwako isimame tu? Kwani demokrasia maana yake nini?

Uanasheria wake katika jamii haulingani na wengi wakiwamo kina nyoka ya makengeza na maprofesa lukuki wachumia matumbo yao wanaofahamika kwa majina.

Alikuwa bungeni na mchango wake huko unajulikana labda utake kumchukia tu.

Ni wazi kuwa, afisa kipenyo yupi atakuwa na mazuri ya kusema kumhusu huyu bwana? Kwani amewapa nafasi hata ya kupumua? Kawashika pabaya!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Pana wengi wanamfahamu tokea o'level Arusha, A'level Tanga hadi UDSM. Wana account tofauti na yako kuhusiana na huyu bwana. Bado ungependa ya kwako isimame tu? Kwani demokrasia maana yake nini?...
Sijasema kuwa hajafanya mazuri na ana uwezo gani, ila tangu alipoingia kwenye siasa akakosa objectivity na ndiyo maana ameishia kuwa anaropoka na kuongea pumba sana.
 
Sijasema kuwa hajafanya mazuri na ana uwezo gani, ila tangu alipoingia kwenye siasa akakosa objectivity na ndiyo maana ameishia kuwa anaropoka na kuongea pumba sana.

Ukweli mchungu huyu jamaa achana naye siyo saizi yako. Waulize jiwe, jaji K, na maprofesa lukuki na wengi wengine watakwambia:

 
Sijasema kuwa hajafanya mazuri na ana uwezo gani, ila tangu alipoingia kwenye siasa akakosa objectivity na ndiyo maana ameishia kuwa anaropoka na kuongea pumba sana.
Hebu taja hizo pumba alizowahi kuzisema.
 
Maelezo yote hayo hayasaidii lolote pasipo kupigania tume huru kwanza. Unataka tume imwengue anayeiteua!?
 
Hapo ndio tujue kuwa Lissu ni good presidential material. Wananchi tubadilike sasa, haki tuweke mbele. Taifa hili linaperekeshwa sana na kakikundi ka watu wachache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…