mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Utanielewa ukitaka kunielewa pale utakapojinasua kwenye kisanduku cha kukaririshwa ili ujitegemeeHuelewi unachoandika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utanielewa ukitaka kunielewa pale utakapojinasua kwenye kisanduku cha kukaririshwa ili ujitegemeeHuelewi unachoandika.
Hahahahahaha ha yamekuwa haya eti vizingiti!Magufuli kavuka kizingiti kingine hiki cha pingamizi, ahsante Mungu kwa utukufu wako.
Kuhusu kuhonga mahakamu kama unaushahidi kamshitaki kwenye kamati ya Mawakili ili afutiwe leseni au asimamishwe uwakili na kamati ya MawakiliWale watu wana elimu kubwa kuliko ya Tundu Lisu huwezi walinganisha na kichaa huyo anayeona marofa wengi kisha anawadanganya
Tundu lisu hajawahi shinda kesi kwa uhalali zaidi ya kuwahonga mahakimu
Na ndo maana kipindi cha kikwete aliwadhalau sana mahakimu.
Mkuu uliandika haya kwa kutafakari au kushabikia!?Hatuwezi kutumia akili za kichaa kuongoza nchi, huyo huyo kasema tume inaweza kuwapa mamlaka wasimamizi, bado tena anasema sio harali,
Pili kuhusu picha
Naomba unipe tafasiri ya
pasport size?
full size na?
half size?
Medium size?
Big size
Je maana yake ni lazima uangalie mbele au ni kipimo cha ukubwa wa picha?
Kuhusu kuangalia mbele ni masharti ya taasisi au hitaji husika na sio kiwango cha ukubwa wa picha. Na ndo maana tunasema tundu ni kichaa ila bado mnamshangilia tu. Alisema magufuli katoa rushwa ya laki moja bado mkashangilia. Nyie ni mazuzu tu.
Ukitaka kujua tundu anamuogopa magufuri, toka jana usiku anatafuta makosa ya magufuli tu siku nzima na nadhani hajalala.
Bila mbeleko Jiwe ni mwepesi sana..!.Kinyago uchonge mwenyewe then kikutishe? Mabeberu wenye mdoli wanazodolewa mchana kweupe sembuse hicho kikaragosi chao?
Wengine eti Mh. Raisi uso kwa uso na....! Bulldozer ukikutana nalo uso kwa uso sijui kama watapata hata picha ya kuambatanisha kwenye simulizi ama ushahidi.
ndiyo hayo ya mgema akisifiwaUkweli mchungu huyu jamaa achana naye siyo saizi yako. Waulize jiwe, jaji K, na maprofesa lukuki na wengi wengine watakwambia:
View attachment 1549202
Huru kisiasaCorona tu imewashinda sasa wewe unasema nini?
Huko marekani kwenyewe huyo Trump ana mawazo, sasa ahangaike na sisi ili iweje?
Bado sisi ni taifa huru
Hawana cha kusema zaidi ya hayo waliyosemaWanazidi kutushangaza!Tungekuwa na Tume Huru, huenda Magu asingekuwa mgombea leo.
Kwa mujibu wa Lissu, Tume ndio iitoa maelezo yanayopingana na sheria, na mgombea uraisi Magufuli, akafuata maelekezo hayo yanayopingana na sheria, maelezo ambayo Lissu yeye alikataa kuyafuata na fomu zake akataka zikahakikiwa na NEC kama sheria inavyoelekeza(alisoma kifungu husika kwa wanahabari).
Swali:Kama Lissu alikuwa wrong,mbona NEC hao hao walikubali kukagua form zake na kuzihakiki kwa maana ya kuhakiki wadhamini wake tofauti na mgombea Magufuli na Lipumba ambao form zao zilihakikiwa huko mikoani na wasimamizi wa majimbo na wakazigonga mihuru badala ya fomu hizo kuhakikiwa na NEC?
Hoja nyingine ya Lissu ni kuhusu siku ya kurudisha fomu ambayo ilikuwa ni jana, na ndio siku ambayo,kwa mujibu wa sheria, ilikuwa ni siku ya uteuzi. Sasa hao wagombea wengine licha ya fomu zao kuhakikiwa na watu wasiostahili kisheria,lakini bado ziliwasilishwa katika siku ambayo haikuwa siku ya uteuzi(kwa maelezo ya Lissu) na hilo,kwa mujibu wa Lissu, pia ni kukiuka sheria ya uchaguzi.
Lissu pia kaweka wazi kuwa kwa mujibu wa sheria,Tume wanaweza kutoa maelekezo, ila sheria hiyo hiyo inatamka kuwa maelezo hayo hayapaswi kuwa kinyume na sheria yenyewe.
All in all,wahusika wamepata funzo tena bila shaka ni funzo kubwa tu hasa kuhusu hizi sheria zetu..
Cha ajabu,wao katika kujibu, hawatufafanulii zaidi ya kusema tu wametupilia mbali na kwamba majibu yatatolewa kwa muweka pingamizi kwa maandishi.
Mbona wanatupa mikopo mkuu, wanachangia bajeti,elimu eg wbNa ili muyapate hayo lazima muolewe kwanza
Katibu wa tume ya uchaguzi: Tume ya uchaguzi baada ya kupokea pingamizi dhidi ya wagombea hao, imewataarifu wawekewa pingamizi mapema iwezekanavyo na wahusika wamewasilisha utetezi wao.
Pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF kwamba hakurudisha fomu kwa mujibu wa masharti yaliwekwa na sheria, tume baada ya kupitia sababu za pingamizi pamoja na utetezi uliotolewa imejiridhisha, Professa Ibrahim Haruna Lipumba amerejesha fomu zake kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi hivyo tume ya taifa ya uchaguzi imejiridhisha pingamizi halina msingi na imelitupilia mbali. Professa Ibrahim Lipumba anaendelea kuwa mgombea halali wa kiti cha Rais kupitia chama cha CUF.
Pingamizi dhidi ya mgombea wa CCM
Tume baada ya kupitia sababu za pingamizi zote mbili kwa pamoja na utetezi uliotolewa imejiridhisha kuwa, Dr. John Magufuli, Mgombea wa kiti cha Rais kupitia chama cha mapinduzi amerejesha fomu zake ambazo zimeambatanishwa pamoja na picha kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya tume ya Taifa ya uchaguzi, hivyo tume ya Taifa ya uchaguzi imejiridhisha kwamba pingamizi hizo hazina msingi wa kisheria na imezitupilia mbali kwa maana hiyo, Dr. Magufuli anaendelea kuwa mgombea halali wa kiti cha Rais kupitia chama cha Mapinduzi CCM.
- Mleta pingamizi anadai kwamba, mgombea Urais kwa tiketi ya CCM hakuambatanisha picha kwenye fomu ya uteuzi.
- Hakurudisha fomu ya uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria
Kwa mujibu wa kanuni ya 39 kanuni ndogo sita ya kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2020, sababu za uamuzi huu wa tume watapewa kwa maandishi, aliyeweka na aliyewekewa pingamizi, kwa msingi wa uamuzi huu, vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu wa kiti cha Rais na makamu wa Rais vinabaki kuwa 15.
Imetolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi
View attachment 1549104
View attachment 1549105
View attachment 1549098
Itajulikana tuu kuwa ni ujuma ya mahakama, nayo mahakama mpaka itaona aibu, kwa ufupi rais wetu ni mfalme ila kuna mahala ufalme unagota tu.Hivi nikuulize tu kifupi rafiki
Akijaza fomu zingine usiku huu akaweka na kila kitu zikagongwa mihuri yote ya mahakama na tume kwa tarehe za nyuma na kwenda kubandika kwenye notisi bodi. Yeye Lisu akabaki na picha ya zamani ataitumia kama ushahidi?
Na unadhani itamsaidia?
Aanze kampeni aache kupoteza muda kwenda kwenye kesi la sivyo atanaswa mtegoni kupitia mbinu zake. Mwisho ziwe kesi za kimahakama halafu anze kupangwa kila baada ya siku mbili inasikilizwa au atawaleta Robert & Amstredam nao wanawekewa zengwe pia
Unachoongea sio kweliLissu ni woga wa kuangukia pua kwenye box la kura na vile vile kutaka kuonyesha wafadhili wake kuwa bado ni mtu relevant. Pingamizi la kusema jumla jumla tu hakurudisha kwa mujibu wa sheria bila kusema ni kifungu gani cha sheria hakikuzingatiwa ni pingamizi la kitoto sana kutoka kwa "mwanasheria msomi aliyebobea", kwa sababu jibu lake ni rahisi sana.
Aliyewekewa pingamizi atasema tu sheria zote zilifuatwa. Pingamizi kutupiliwa mbali (dismissed) ni aibu> Ni afahdali angeota pingamizi kimya kimya kuliko kutoa matangzani mengi kwa mbwebe kam haiku sababu ya kutafuta cheap popularity.
Kukosea kupoMkuu Salary Slip wakati nwingine busara itawale chuki uliyonayo itakutia matatani nafsi yako. John Pombe Magufuli ni Rais anayemaliza muda wake, kwa maana hiyo anajua sheria, kanuni na taratibu za kugombea.
Ebu Mkuu jiulize:
√ Iweje leo asijue na kufanya kinyume?
√ Kama aliweza kupitishwa wakati wa awali asipokuwa na madaraka ya kutumia mwanasheria mkuu na hata wajumbe wa Tume kumwelekeza, iweje leo akiwa na madaraka ashindwe kuwatumia?
Lissu amedai Magifuli kaingizwa kwenye chaka, amini sasa ujuaji wake siyo kwamba umemwingiza kwenye chaka bali choo cha jinsi nyingine. Chuki yake dhidi ya Magufuli itaadhibiwa na wapiga kura, vivyo hivyo na wagombea wa chama chake. Chama chenye viongozi wa kupinga kila kitu.
All in all, shame on you.
Lissu atakata rufaa. NEC mtajibeba mwaka huu.
NECCCMWanazidi kutushangaza!Tungekuwa na Tume Huru, huenda Magu asingekuwa mgombea leo.
Kwa mujibu wa Lissu, Tume ndio iitoa maelezo yanayopingana na sheria, na mgombea uraisi Magufuli, akafuata maelekezo hayo yanayopingana na sheria, maelezo ambayo Lissu yeye alikataa kuyafuata na fomu zake akataka zikahakikiwa na NEC kama sheria inavyoelekeza(alisoma kifungu husika kwa wanahabari).
Swali:Kama Lissu alikuwa wrong,mbona NEC hao hao walikubali kukagua form zake na kuzihakiki kwa maana ya kuhakiki wadhamini wake tofauti na mgombea Magufuli na Lipumba ambao form zao zilihakikiwa huko mikoani na wasimamizi wa majimbo na wakazigonga mihuru badala ya fomu hizo kuhakikiwa na NEC?
Hoja nyingine ya Lissu ni kuhusu siku ya kurudisha fomu ambayo ilikuwa ni jana, na ndio siku ambayo,kwa mujibu wa sheria, ilikuwa ni siku ya uteuzi. Sasa hao wagombea wengine licha ya fomu zao kuhakikiwa na watu wasiostahili kisheria,lakini bado ziliwasilishwa katika siku ambayo haikuwa siku ya uteuzi(kwa maelezo ya Lissu) na hilo,kwa mujibu wa Lissu, pia ni kukiuka sheria ya uchaguzi.
Lissu pia kaweka wazi kuwa kwa mujibu wa sheria,Tume wanaweza kutoa maelekezo, ila sheria hiyo hiyo inatamka kuwa maelezo hayo hayapaswi kuwa kinyume na sheria yenyewe.
All in all,wahusika wamepata funzo tena bila shaka ni funzo kubwa tu hasa kuhusu hizi sheria zetu..
Cha ajabu,wao katika kujibu, hawatufafanulii zaidi ya kusema tu wametupilia mbali na kwamba majibu yatatolewa kwa muweka pingamizi kwa maandishi.
Jamaa anatia hurumaNimependa body language yake na akamalizia na "hakuna maswali".