Katika siasa hizi hali ni kawaida sana kutoke kwani udhaifu wko ni faida kw wengine lkn bado nawaza sidhani kama ndugu Lissu yuko sahihi sana na haya mapingamizi yake' ngoja niwaze kwa sauti, iwapo anasema fomu za mgombe uraisi magufuli zilihakikiwa mikoani wakat wa kutafuta wadhamini hili sio kosa kwan walio hakiki hizo fomu ni ofisi za Ccm na si NEC hivyo sio kosa kwani sheria za hizo fomu kua halali ziko wazi kw kila mtu hata mie nikitaka kuhakiki ni swala la kufahamu tu kanuni zinasemaje juu ya hizo fomu. Pili picha ktk fomu ni jambo la muhimu sana na kama zilihakikiwa kabla na wasimamizi wa majimbo kila mkoa aliopita haiwez kuwezekana hao wote wasigundue kwamba mwenyekiti wao hajaweka picha ktk fomu zake, tuanze kua tunafikiria zaidi na kwa kina. La mwisho binafsi nimeshuhudia urudishwji wa hizo fomu kwa wagombea wote yaan Lipumba na Magufuli kwa siku hiyo moja ambayo pia ndugu Lissu ndio siku aliyorudisha fomu yake, sasa akisema walirudisha siku ambayo si ya uteuzi nadhani hayuko sahihi au washauri wake wanamlisha matango pori humu kuna uzi ulitoka kwmba siku ya yeye kurudisha fomu aliwekwa chumba cha masubirio kwa muda mrefu ambayo ndo siku hiyi hiyo alisema ndugu magufuli hakumaliza hata nusu saa(30dk) ktk urudishaji wake. Sasa wana JF wenzangu hebu tuanze kua tunawaza na kufikiri zaidi ya tunachoambiwa kwa manufaa ya Taifa letu. Niwe mkweli binafsi nimekuzwa na malezi ya Ccm na mpaka leo kwa matukio ya ccm sikua tayari kuwapa kura yangu kutokana na madudu yao ikiwemo ufisadi na upendeleo lkn hawa wapinzani nao wana kasoro zikiwemo washauri wabovu na mifumo yao ya kiutendaji mfano walitumia miaka mingi kujijenga na kupinga ufisadi kabla ya mwaka 2015 na kweli walifanikiwa na ilikua kweli ccm na viongozi wao kua na maadili mabovu lkn baada ya ccm kucheza na kuamua kuwatoa hao mafisadi ikiwemo Lowasa na wengineo tena dk za mwisho na eti wao upinzani kwa maana ya iliyokua UKAWA kuja kuwakumbatia hao mafisadi na kutaka kutuaminisha wamekua safi JUST BY OVERNIGHT hiyo haikua sawa na hapo ndo walipoteza tena imani kwa baadhi yetu ikiwemo mimi binafsi na washakji zangu ambao hatufuatilii siasa moja kwa moja. Upinzani unatakiwa kuja na hoja za kuendesha inchi yetu na namna gani mipango yao kimaendeleo inavyofanya kazi. Sitaki kuamini CCM ni borq zaidi au hatuwezi kusonga zaidi bila wao kua madarakani HAPANA mabadiliko ni lazima yawepo lkn hao wanaotaka hayo mabadiliko wanatuaminishaje kwamba na wao Upinzani ni watu sahihi?????????!!!!!!!!! Hayo ni mawazo yangu binafsi nami naishi hapa hapa Tanzania na kila siku naona na kusikia kinachiendelea hapa kwetu JMT.