Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Unachoongea sio kweli
Lissu ametaja kanuni,sheria ya uchaguzi vifungu specifically, na hata kwenye ile fomu ya pingamizi kataja specifically kwamba kipengele Fulani nadhani ni n,halafu baada ya kukitaja akaenda kwenye sheria what does the law says akakuta ni contrary to kifungu Fulani cha sheria ya uchaguzi,na kanuni.
Sheria na kanuni za uchaguzi zinazosimamia uteuzi wa wagombea na mapingamizi dhidi yao ni hizi hapa: Uchaguzi 2020 - Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali. Ni kifungu gani kilichokiukwa kama Lissu hakutaka kufurahisha wafuasi wake tu ambao anajua hawasomi sheria zenyewe bali kukubali kila anachowaambia?
 
Afanye chochote atakacho, lakini tayari hata hiyo tume itajua hizo sheria wanazosimamia na kuengua wagombea wa upinzani ni hujuma za wazi, na wanatengeneza njia za machafuko. Mpaka sasa imeonyesha wazi pasi na shaka kuwa tume ya uchaguzi sio huru.
Hujuma kama zipi? Za wazi
Nani aanzishe machafuko na mtekelezaji wa hayo
 
Naomba mhombea yeyote anaejitoa ufahamu muwe mnapuuza hivohivo..
Lissu niwa kupuuza tu na hii ndo dawa yake.
 
Katika siasa hizi hali ni kawaida sana kutoke kwani udhaifu wko ni faida kw wengine lkn bado nawaza sidhani kama ndugu Lissu yuko sahihi sana na haya mapingamizi yake' ngoja niwaze kwa sauti, iwapo anasema fomu za mgombe uraisi magufuli zilihakikiwa mikoani wakat wa kutafuta wadhamini hili sio kosa kwan walio hakiki hizo fomu ni ofisi za Ccm na si NEC hivyo sio kosa kwani sheria za hizo fomu kua halali ziko wazi kw kila mtu hata mie nikitaka kuhakiki ni swala la kufahamu tu kanuni zinasemaje juu ya hizo fomu. Pili picha ktk fomu ni jambo la muhimu sana na kama zilihakikiwa kabla na wasimamizi wa majimbo kila mkoa aliopita haiwez kuwezekana hao wote wasigundue kwamba mwenyekiti wao hajaweka picha ktk fomu zake, tuanze kua tunafikiria zaidi na kwa kina. La mwisho binafsi nimeshuhudia urudishwji wa hizo fomu kwa wagombea wote yaan Lipumba na Magufuli kwa siku hiyo moja ambayo pia ndugu Lissu ndio siku aliyorudisha fomu yake, sasa akisema walirudisha siku ambayo si ya uteuzi nadhani hayuko sahihi au washauri wake wanamlisha matango pori humu kuna uzi ulitoka kwmba siku ya yeye kurudisha fomu aliwekwa chumba cha masubirio kwa muda mrefu ambayo ndo siku hiyi hiyo alisema ndugu magufuli hakumaliza hata nusu saa(30dk) ktk urudishaji wake. Sasa wana JF wenzangu hebu tuanze kua tunawaza na kufikiri zaidi ya tunachoambiwa kwa manufaa ya Taifa letu. Niwe mkweli binafsi nimekuzwa na malezi ya Ccm na mpaka leo kwa matukio ya ccm sikua tayari kuwapa kura yangu kutokana na madudu yao ikiwemo ufisadi na upendeleo lkn hawa wapinzani nao wana kasoro zikiwemo washauri wabovu na mifumo yao ya kiutendaji mfano walitumia miaka mingi kujijenga na kupinga ufisadi kabla ya mwaka 2015 na kweli walifanikiwa na ilikua kweli ccm na viongozi wao kua na maadili mabovu lkn baada ya ccm kucheza na kuamua kuwatoa hao mafisadi ikiwemo Lowasa na wengineo tena dk za mwisho na eti wao upinzani kwa maana ya iliyokua UKAWA kuja kuwakumbatia hao mafisadi na kutaka kutuaminisha wamekua safi JUST BY OVERNIGHT hiyo haikua sawa na hapo ndo walipoteza tena imani kwa baadhi yetu ikiwemo mimi binafsi na washakji zangu ambao hatufuatilii siasa moja kwa moja. Upinzani unatakiwa kuja na hoja za kuendesha inchi yetu na namna gani mipango yao kimaendeleo inavyofanya kazi. Sitaki kuamini CCM ni borq zaidi au hatuwezi kusonga zaidi bila wao kua madarakani HAPANA mabadiliko ni lazima yawepo lkn hao wanaotaka hayo mabadiliko wanatuaminishaje kwamba na wao Upinzani ni watu sahihi?????????!!!!!!!!! Hayo ni mawazo yangu binafsi nami naishi hapa hapa Tanzania na kila siku naona na kusikia kinachiendelea hapa kwetu JMT.
Msikilize vizuri Lisu alisema JPM hakurudisha form Kama sheria za uchaguzi zinavyosema unaweza ukamwona mtu ndani ya dakika 30 Kama ulivyosema ila hakukidhi vigezo vilivyotakiwa kwa maana hiyo hajarudisha form.
 
Nani kakatwa , kama magufuli karudishwa unadhani nani ataondolewa ?

Kama kuna makosa watakatwa Magufuli hakuwa na kosa lolote kwenye fomu yake shida yenu mnasaidiwa kufikiri na Lissu
IMG_0710.png
 
Hiyo ndio mbinu inawafanya ccm watangazwe washindi siku hizi.
Mkuu Lisu hapa kaonesha umbumbumbu!

Unaposema form zimehakikiwa na wasimamizi wa uchaguzi majimboni hao ndio NEC yenyewe ndio maana hata matokeo ya uchguzi yanaanza kutolewa huko.

Alipocheleweshwa pale kwenye tume ile juzi tume walitoa maelezo kwamba waliopitisha form zao huko majimboni hajakaa sababu tume haikupata shida ya kuanza kukagua maelfu ya hao wadhamini.

Kwahiyo wote tangu kina Membe ni wajinga ila yeye Lisu tu ndio alikuwa na akili?
 
Yako NEC ulitaka waKuletee nyumbani kwako?

Halafu wewe unamwamini Lisu fomu Ina Hadi sehemu ya kubandika picha unaamini kweli kuwa picha haulikubandikwa?

Lisu anatafita kiki kwenye media kwa.kila hali hata kwa kutunga vitu vidogo vya uongo
Sio kwamba hakuweka picha Ila shida aliweka picha isiyo sahihi
 
Lieu anachekesha.
Tume aiteue Magu. Leo hii anataka imuite. Hizi ni dalili kuwa katiba yetu ni mbovu. Chadema hawataki kusikia ila time itamtangaza meko mchana kweupe
Baada yabkushinda kwa kishindo na si vinginevyo,
Wewe unaamini tundu.lisu anachoongea chote ni sawa?
Alisema tutanyolewa bila maji, sasa hao wanyozi walienda wapi?
Tundu ni mhalibifu kwa nchi na si mshauri mzuri kwenye nchi yake.
 
Msikilize vizuri Lisu alisema JPM hakurudisha form Kama sheria za uchaguzi zinavyosema unaweza ukamwona mtu ndani ya dakika 30 Kama ulivyosema ila hakukidhi vigezo vilivyotakiwa kwa maana hiyo hajarudisha form.

Kwani Tume wajibuje? Hahahaha chadema bhana hahaha hata Membe alihakikiwa kule kule majimboni wadhamini wake kwanini Lissu hakunuwekea pingamizi? Lissu amesoma sheria bila kusoma kanuni hahaha

Na picha je? Hahaha
IMG_0710.png
 
Mkuu Lisu hapa kaonesha umbumbumbu!

Unaposema form zimehakikiwa na wasimamizi wa uchaguzi majimboni hao ndio NEC yenyewe ndio maana hata matokeo ya uchguzi yanaanza kutolewa huko.

Alipocheleweshwa pale kwenye tume ile juzi tume walitoa maelezo kwamba waliopitisha form zao huko majimboni hajakaa sababu tume haikupata shida ya kuanza kukagua maelfu ya hao wadhamini.

Kwahiyo wote tangu kina Membe ni wajinga ila yeye Lisu tu ndio alikuwa na akili?

Unachikiuliza leo ndio tumekuwa tukijiuliza kila siku kuwa ccm tu ndio wanaojua kujaza fomu nchi nzima? Wakati ccm wanashinda kwa mbinu hizo ulikuwa unatamba kuwa wapinzani ni vilaza, leo jiwe ndio kuonyeshwa kilaza unalialia. Mnashabikia uovu, mkibadilishiwa kibao mnalialia. Na kwa pingamizi hili ndio tume imeonekana ni jinsi gani sio huru. Halafu kwa tume hiyo dhaifu , ndio mnasema eti tarehe 28 mnashinda.
 
Yako NEC ulitaka waKuletee nyumbani kwako?

Halafu wewe unamwamini Lisu fomu Ina Hadi sehemu ya kubandika picha unaamini kweli kuwa picha haulikubandikwa?

Lisu anatafita kiki kwenye media kwa.kila hali hata kwa kutunga vitu vidogo vya uongo
Na anaangaliwa tu. Next atafanya nn?
 
Unachikiuliza leo ndio tumekuwa tukijiuliza kila siku kuwa ccm tu ndio wanaojua kujaza fomu nchi nzima? Wakati ccm wanashinda kwa mbinu hizo ulikuwa unatamba kuwa wapinzani ni vilaza, leo jiwe ndio kuonyeshwa kilaza unalialia. Mnashabikia uovu, mkibadilishiwa kibao mnalialia. Na kwa pingamizi hili ndio tume imeonekana ni jinsi gani sio huru. Halafu kwa tume hiyo dhaifu , ndio mnasema eti tarehe 28 mnashinda.
Kwenye form za Magufuli kulikuwa na kosa gani?
 
Back
Top Bottom