If Official,
Tanzania sasa ni rasmi a failed state. Nchi imeanguka rasmi kwenye kikundi kidogo cha dola ya CCM. Kikundi hiki ndo kinaamua mambo yaendeje, lipi litokee na lipi lisitokee, kipi kifanikiwe na kipi kisifanikiwe. Yupi anastahili kuishi na yupi hastahili kuishi. Wananchi muone nini, muongee nini na msikie nini.
kuanzia vyombo vya ulinzi na usalama, mifumo ya uwajibikaji na kutazamana ( Accountability, Checks and Balances), Mifumo ya Haki (Mahakama), Mifumo ya Kisiasa (Vyama vyote vya Siasa kasoro Chadema), Bunge na Madhehehu ya Dini vyote vimekamatwa na kikundi hiki kidogo cha dola ya CCM.
Kwa sasa kikundi hiki hakiogopi kumshughulikia mtu yeyote anayejaribu kuwafungua macho wananchi awe Kiongozi wa Dini ( Mfano Gwajima na Father Kitima) awe mwanasiasa au chama cha siasa ( Mfano Tundu Lissu na Chama chake Chadema) au kiumbe yeyote yule.
Poleni sana Watanzania. Sasahivi hatuna tofauti na Congo DRC ( Nchi ya Uchawa,Mziki, Michezo, Starehe na Ufisadi wa Kutisha) na Eritrea ( Nchi yenye total control ya dola juu ya Wananchi na Maisha yao)
Tujiandae tu na matokeo ya haya.
Lord denning
Mwanza