Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Moja ya maandiko ya hovyo kabisa kuwahi kutokea ardhini na mbinguni. Sujui hii ni akili gani. Au ulikuwa umelewa
Mimi naweza kulikosoa andiko lake, lakini si kwasababu ni andiko la hovyo, nikilikosoa andiko lake ni sababu hajawahi kuona madhara ambayo wanahabari na vyombo vya habari vilikutana nayo chini ya JPM. Hata ukimuonyesha sasa bado atakataa, ila kwamba andiko lake hili la hovyo nitakukatalia na nitamtetea yeye,
 
Umeelezea vizuri sana; kuvujisha habari siyo sawasawa na uandishi wa uchunguzi. Mfano upo kwenye mada hii hii; mtu anaweza kuvujisha habari bila kwenda ndani zaidi ya hilo. Kudos!
 
Umesema sahihi, halafu Mwanakijiji amesahau alivyokuwa wakala wa JPM wa kuua ajenda za wananchi, wanachofanya wenzake yeye Mwanakijiji ndio muasisi
Acha kulaghai watu; angalia rekodi yangu uone. Yaani, kweli kabisa na akili zangu timamu ulitarajia niunge mkono mabadiliko ya kuvingirisha mikono? Nilimuandika JPM kabla hajawa Rais, nilijua akiwa Rais atakuwaje (na hakuna alichonishangaza); na nilimuandika akiwa Rais - pamoja na kuwa nilimuunga mkono. Nilipotakiwa kukosoa nilikosoa na nilipamua kuunga mkono niliunga mkono. Ukiweka kwenye mizani miaka yake mitano kimaendeleo ilikuwa ni bora zaidi kuliko miaka 25 kabla yake. Hutaki?
 
Huyo aliyesema hivyo labda hakuishi wakati wa JK... acheni masihara bana. Au labda wengine ni vijana wadogo kabisa mmesahau kabisa yaliyotokea wakati wa Mkapa na JK nyinyi...
 
Naam, I stand corrected.
 
Jamani, mbona kwenye hii hii mada hapo juu nimewawekea ni link ya kuwa sikuwa muunga mkono juhudi bila kukosoa. Au ni vigumu sana hata kubonyeza link hapo juu. Nilimkosoa Magufuli na sikutumiwa watu kunitafuta; wakati wa JK walitumwa watu hadi Marekani.. Hawa watu waache utani. Sina tatizo lolote la kumkosoa Magufuli alipokuwa hai au alipokufa. Jaribu ku "search" hapa JF mada nilizoanzisha zinamhusu Magufuli uone. Nimeweka link ya moja tu hapo juu.
 
Ulikuwa ukiwakosoa pia waliomkosoa (yaani mkiwa vitani halafu askari mwenzio anaelekeza silaha upande wako unaogopa), labda hapo ndipo wadau walipoona kwamba na wewe ulikuwa sehemu ya au mshirika wa "mhimili uliojichimbia chini zaidi."
 
Ndio maana sisi wengine tuliacha kabisa kusoma magazeti na kusiklize habari za media zaTanzania. Ni dhahiri waziri wa habari ni mtu hatari sana kwa uhuru wa vyombo vya habari, medio zote zimegeuka uchawa, habari za upinzani hautangazwi kabisa. Mbaya zaidi hata taarifa za ufisadi mkubwa unaofanywa na watawala zinazuiwa zisitoke. SSH ni janga jipya
 
Ndiyo linaloshtua...nimesoma ushahidi wa Mpina..ile ingekuwa habari kwenye gazette au hata hapa JF..na ushahidi wote u gewekwa. Sidhani kama mtu anaweza kuleta ushahidi hapa bila kupitiwa na kamati maalum ya JF na kuwauliza wahusika kwanza.
Nakumbuka JF ya zamani iliyokuwa home of great thikers and where we dared to talk/speak openly
 
ITV/Radio One viroboto wa CCM tangu Mengi alipofariki, WAPO Radio wao siku nyingi walijitambulisha na kujiunga na Polepole uchaguzi uliopita, ni pacha wa gazeti la Uhuru. JF imejifunika hijab gubigubi isitambulike kuwa imo!
 
Ukiona serikali inaungana na vyombo vya habari ujue hata sisi wachangiaji hatupo safe.

Jambo la msingi ni kuendelea na mazungumzo kuhusu umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na kuchukua hatua za kulinda na kuimarisha.

Kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinaweza kutekeleza jukumu lao muhimu katika jamii yenye demokrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…