Tunaomlaumu Tundu Lissu hebu basi tuvae viatu vyake

Mbona Billicanas ilivunjwa lakini Mbowe haongei ujinga ujinga kama huyo Tundu Lisu?
Mbona tundu alisema kipindi cha kampeni kwamba amewasamehe wote watesi wake ila nikiona twit zake kule Twitter yule bwana bado anakinyongo.
Kwa akili zenu . Nikuwa ukiumizwa na system urudi ushukuru na kupiga magoti ?! . Huo ni unyama zaidi ya mkoloni mjerumani
 
Tundu Lissu hafai kuwa Rais wa JMT. Mimi siyo CCM wala CHADEMA, yaani sina chama. Lakini sina trust na Lisu kabisa kwa usalama wa Taifa letu.
Usalama upi? kwanza hujui chochote kuhusu usalama
 
N

Mbwiga yule boss wenu Lisu analilia mafao ya ubunge!
Rest easy
1. Godfrey Luena,
2. Leopold Lwabaje
3. Akwilina Akwilini Bafta
4. Daniel John


Tunawakumbuka:
1. Azory Gwanda
2. Simon Kanguye
3. Ben Saanane
 
Labda tuvae viatu vya usaliti kwa nchi yake.

Wakati tunapigania madini alisimama upande wa mabeberu.
Hiyo siyo kweli. Lissu alikuwa mpinzani mkubwa dhidi ya mikataba ya hovyo ya uchmbaji dhahabu iliyosababisha wachimbaji wadogo wafukiwe kwenye migodi. Kwa kufanya hivyo aliitwa mchochezi akawekwa ndani na kufunguliwa mashtaka. Wasaliti ni wale walioingia na kusaini mikataba ya hovyo. Ajabu haohao waliosaini hiyo mikataba wakaja kulalamika kuwa ni mikataba ya kinyonyaji
 
Mbona tundu alisema kipindi cha kampeni kwamba amewasamehe wote watesi wake ila nikiona twit zake kule Twitter yule bwana bado anakinyongo.
Kusamehe siyo kusahau.

Lissu alifanyiwa ukatili mkubwa mnooooo. It's very painful.

Halafu hata hakustahili adhabu hiyo. Dola nzima ilipambana naye wakati akiwa mahututi Nairobi.
 
Kusamehe siyo kusahau.

Lissu alifanyiwa ukatili mkubwa mnooooo. It's very painful.

Halafu hata hakustahili adhabu hiyo. Dola nzima ilipambana naye wakati akiwa mahututi Nairobi.
simpendi sana Lissu na chama chenu cha chadema.
 
Kwa akili zenu . Nikuwa ukiumizwa na system urudi ushukuru na kupiga magoti ?! . Huo ni unyama zaidi ya mkoloni mjerumani
Kwa akili zenu . Nikuwa ukiumizwa na system urudi ushukuru na kupiga magoti ?!
Huko ni kukubali utumwa uliopigwa vuta na waasisi wa taifa hili. Nyerere angeliona hilo angepata kichefuchefu.
 
That fool amefanya campaign zote hukuwahi dhihirisha vision yake zaidi ya kumsema Magufuli ,
Hana vision yule, he can only criticize other people Vision,
Kama aliamua ku side na Mzungu kwenye makinikia and they both lost it that is good for nothing lunatic.
 
Kwani makinikia haziendi ?!. Haya yote alaumiwe Mkapa
 
mimi namshukulu sana tundu lisu bila yy watanzania tusingejua km rais wetu ni mgonjwa na hataumauti ulipompata yy ndie aliyekua wa kwanza kutupa habari huku serikali ikutudanganya kua rais yupo ofsini anachapa kz na anatusalimia kuhusu aliyofanyiwa ni ushetani wa hari ya juu sana ila kinyume chake waliomfanyia hayo wengine walishataungulia na wengine ndio hao na nasikia kua na wengine zaidi watapukutika hiyo siri nakuibia kutoka kwa izrail mtoa roho
 
Kwani makinikia haziendi ?!. Haya yote alaumiwe Mkapa
I agree with you on that, JPM tried his best to fix the deeds of his predecessors and the ccm mafia,
Matatizo ya nchi hii yameletwa na ccm, but I hate what Lisu did, Despite all JPM alikuwa na watu wengi sana waliompenda na kumkubali he could've done better by taking the Advantage just to mourn with them or just stay quiet,
Kiongozi mzuri siku zote hujipambanua kwa Upendo katikati ya chuki na kutafuta maridhiano kama alivyofanya Mandela dhidi ya Watesi wake, na kwa hili that stupid Lunatic Tundu hatakuwa kiongozi kamwe tena na waliomfanyia ule unyama bado wako, asiache kujihami.
 

Siri ya kushambuliwa Mh Lisu anaifahamu fika ndio maana hataki ukweli uwekwe wazi mahakamani. Muulize kwa nini mpaka kesho amemficha dereva wake ambaye ni shahidi wa muhimu kuliko mtu mwingine yeyote. Muulize kwa nini IOGP Simon Sirro aliposema kuwa atawatuma vijana Nairobi kwenda kumhoji Lisu na dereva wake yeye Lisu akawa wa kwanza kupinga na kusema kuwa polisi wa Tanzania hawezi kwenda kuwahoji wakiwa Kenya bila kupata kibali cha mwanasheria mkuu wa Kenya. Kwani kama hiyo ni taratibu kwa nini adhani kuwa IGP Sirro alikuwa hafahamu hayo?? Na baada ya tamko la Sirro ndani ya wiki moja Lissu na dereva wake wakahamia Ubeljiji!! Au wengine hamkufuatilia hayo? Ukweli ni kuwa MH Lisu sasa ameajiriwa. Hata mambo mengine anayoandika kuichafua nchi yeye mwenyewe hayaamini ila kwa kuwa ni ajira lazima aandike ili apate mshahara. Pole kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…