BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
TUNASISITIZA HAKI KUTENDEKA KWA MASHEHE WA KIISLAMU WA UAMSHO KUTOKA ZANZIBAR
Tarehe 27 Februari 2021, nilikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa wamealikwa na ACT Wazalendo kuhudhuria Dua ya kumuombea Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliyefariki hivi karibuni.
Siku hiyo, Sheikh Ponda aliongea jambo linaloutesa sana moyo wangu. Aligusia suala la Mashehe wa Kiislamu wa Uamsho kutoka Zanzibar wanaoshikiliwa Tanzania Bara kwa miaka kadhaa sasa! Jambo hili linautesa moyo wangu kwa kuwa naona haki yao imecheleweshwa mno!
Kuna 'watu' waliwahi kuniambia kuwa suala lao ni 'nyeti' hivyo halihojiwi! Maswali ni mengi kuliko majibu. Kuendelea kuwashikilia Mashehe hao pasipo maelezo yanayoeleweka kutachochea chuki za kidini. Hii ni kwa sababu wafuasi wa Mashehe hao wanaendelea kunung'unika chinichini kwa chini.
Najisikia kuwiwa af kuwapazia sauti yangu Mashehe hao pia! Haijalishi wametenda kosa zito kiasi gani, lakini haki yao katika nchi inapaswa ilindwe. Wanatakiwa watendewe haki kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania. Kutendewa haki kwao ni pamoja na kusikilizwa kwa kesi yao kwa haraka kama wana kesi ya kujibu.
Kama Askofu, ninaungana na Sheikh Ponda katika kuwapazia sauti Mashehe wa Kiislamu wa Uamsho kutoka Zanzibar wanaoshikiliwa Tanzania Bara kuwa watendewe haki kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania. Vinginevyo, waachiliwe huru pasipo masharti ye yote!
Mambo kama hayo ndiyo yalinisukuma kuanzisha kampeni za kuhamasisha umma wa Watanzania kuhusu umuhimu na uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.