Tunasisitiza haki kutendeka kwa mashehe wa Kiislamu wa Uamsho kutoka Zanzibar

Nimposti kama ilivo
IMG-20210411-WA0000.jpg
 
TUNASISITIZA HAKI KUTENDEKA KWA MASHEHE WA KIISLAMU WA UAMSHO KUTOKA ZANZIBAR

Tarehe 27 Februari 2021, nilikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa wamealikwa na ACT Wazalendo kuhudhuria Dua ya kumuombea Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliyefariki hivi karibuni.

Siku hiyo, Sheikh Ponda aliongea jambo linaloutesa sana moyo wangu. Aligusia suala la Mashehe wa Kiislamu wa Uamsho kutoka Zanzibar wanaoshikiliwa Tanzania Bara kwa miaka kadhaa sasa! Jambo hili linautesa moyo wangu kwa kuwa naona haki yao imecheleweshwa mno!

Kuna 'watu' waliwahi kuniambia kuwa suala lao ni 'nyeti' hivyo halihojiwi! Maswali ni mengi kuliko majibu. Kuendelea kuwashikilia Mashehe hao pasipo maelezo yanayoeleweka kutachochea chuki za kidini. Hii ni kwa sababu wafuasi wa Mashehe hao wanaendelea kunung'unika chinichini kwa chini.

Najisikia kuwiwa af kuwapazia sauti yangu Mashehe hao pia! Haijalishi wametenda kosa zito kiasi gani, lakini haki yao katika nchi inapaswa ilindwe. Wanatakiwa watendewe haki kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania. Kutendewa haki kwao ni pamoja na kusikilizwa kwa kesi yao kwa haraka kama wana kesi ya kujibu.

Kama Askofu, ninaungana na Sheikh Ponda katika kuwapazia sauti Mashehe wa Kiislamu wa Uamsho kutoka Zanzibar wanaoshikiliwa Tanzania Bara kuwa watendewe haki kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania. Vinginevyo, waachiliwe huru pasipo masharti ye yote!

Mambo kama hayo ndiyo yalinisukuma kuanzisha kampeni za kuhamasisha umma wa Watanzania kuhusu umuhimu na uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
Nenda Guantanamo Bay ukajifunze mambo ya haki
 
Ushahidi wa kimazingira unaonesha kwamba baada ya kukamatwa wao na yale matukio ya uhalifu yalikoma,hivyo inawezekana walihusika moja kwa moja na huo uhalifu uliyokuwa ukitokea au pengine hawakuhusika moja kwa moja ila walikuwa ndio kichocheo cha hayo matukio ya uhalifu.
Hao ni Magaidi +
 
Hii mada mbona inajirudia kila wakati? Kama watu wamevunja sheria kwa nini unakosa usingizi? Au uliwatuma wewe?
 
Huyu mama hana akili ya kipumbavu hivyo, sio narrow minded hivyo

Pia kwenye hilo sababu linagusa maswala ya kiusalama inawezakana Mama akawa siyo wa mwisho kuamua isipokuwa vyombo vya dola na usalama wa nchi.

Tuukatae ugaidi kwa nguvu zote!
 
muislamu ndugu yake muislamu mwenzie lakini raisi kikwete ndiye aliyewafunga
 
Zaidi ya Polisi @ Uhuru.

Nimeandika vyombo vya Usalama siyo Jeshi la Polisi pekee .

Likitokea la kutokea matharani Ugaidi na usalama kuwa shakani wao huwa hawalali.
Hao wote wanatumika na ccm au tuseme wanatumika kisiasa kuanzia hao usalama wa taifa hadi jeshi lenye kufanya mazoezi barabarani ili kuwatisha rai na hao polisi ndio kama wanavyojulikana.
 
Mashehe wa UAMSHO wanaingia miaka tisa - Watu hawana hata harufu ya Ugaidi ukiulizia kwanini wapo ndani na hawapaswi kutembelewa unaambiwa ,ni amri kutoka juu .sasa Juu wapi ? Mbinguni au kwa Raisi ?
Au kwa kuwa ni waislamu tu ndio mkawafanyia hivi ? Eti magaidi hivi mnawajuwa magaidi au mnawasikia tu ? Nina hakika kama hao wengekuwa magaidi basi kingekwishanuka zamani sana,kuna nchi hazijakamata hata gaidi mmoja ila mnakijua kinachotokea. Eti hawa mashee wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi ,shukuruni mmewakuta watanzania walio wengi ni watu wa ajabu si raia si majeshi.
 
Likely this is the less evil compared to what they did
 
Watatoka bana, i predict, ila tukubali serikali ina taarifa nyingi sana wengine hamjui. Naamini wataachiwa
 
Watatoka sasa wakiwa wamekwisha dhulumiwa mno baada ya maelekezo kutoka juu kuwa sasa yamekoma hatimaye.
 
Wewe um
Mashehe wa UAMSHO wanaingia miaka tisa - Watu hawana hata harufu ya Ugaidi ukiulizia kwanini wapo ndani na hawapaswi kutembelewa unaambiwa ,ni amri kutoka juu .sasa Juu wapi ? Mbinguni au kwa Raisi ?
Au kwa kuwa ni waislamu tu ndio mkawafanyia hivi ? Eti magaidi hivi mnawajuwa magaidi au mnawasikia tu ? Nina hakika kama hao wengekuwa magaidi basi kingekwishanuka zamani sana,kuna nchi hazijakamata hata gaidi mmoja ila mnakijua kinachotokea. Eti hawa mashee wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi ,shukuruni mmewakuta watanzania walio wengi ni watu wa ajabu

Wewe umezaliwa lini?
Unajua waliingia kwa kosa gani na nini kikichosababisha wapelekwe huko?

Kama hujui lejea wakatibwa matamkobyao na matuku9byaliyokuwa yanatendeka huko zanziba.

Mara makanisa kuchomwa na mapadri kupigwa risasi na watalii pia kupigwa risasi,
Kuna mashee wasio wa uamsho walitegwa milipuko kwenye majumba yao
Sasa iam hujui historia hiyo ukae kimya.

Na toka walipokamatwa zamziba iko shwari mpaka sasa hakuna ujingaujinga.
 
Madai haya hapo ya mdau wa JF ananiuliza .

Ameandika kuhusiana na mashekhe wa Taasisi ya Uamsho,bahati mbaya ushahidi huo haupo mahakamani na kama upo aupelekea ili kesi iamuliwe. na moderators tukiandika habari za kuwazungumzia mashee wa Taasisi ya uamsho mnakuja mbio mnaondoa,kwa vile ni waislamu au inakuwaje hapo ?
 
TUNASISITIZA HAKI KUTENDEKA KWA MASHEHE WA KIISLAMU WA UAMSHO KUTOKA ZANZIBAR

Tarehe 27 Februari 2021, nilikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa wamealikwa na ACT Wazalendo kuhudhuria Dua ya kumuombea Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliyefariki hivi karibuni.

Siku hiyo, Sheikh Ponda aliongea jambo linaloutesa sana moyo wangu. Aligusia suala la Mashehe wa Kiislamu wa Uamsho kutoka Zanzibar wanaoshikiliwa Tanzania Bara kwa miaka kadhaa sasa! Jambo hili linautesa moyo wangu kwa kuwa naona haki yao imecheleweshwa mno!

Kuna 'watu' waliwahi kuniambia kuwa suala lao ni 'nyeti' hivyo halihojiwi! Maswali ni mengi kuliko majibu. Kuendelea kuwashikilia Mashehe hao pasipo maelezo yanayoeleweka kutachochea chuki za kidini. Hii ni kwa sababu wafuasi wa Mashehe hao wanaendelea kunung'unika chinichini kwa chini.

Najisikia kuwiwa af kuwapazia sauti yangu Mashehe hao pia! Haijalishi wametenda kosa zito kiasi gani, lakini haki yao katika nchi inapaswa ilindwe. Wanatakiwa watendewe haki kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania. Kutendewa haki kwao ni pamoja na kusikilizwa kwa kesi yao kwa haraka kama wana kesi ya kujibu.

Kama Askofu, ninaungana na Sheikh Ponda katika kuwapazia sauti Mashehe wa Kiislamu wa Uamsho kutoka Zanzibar wanaoshikiliwa Tanzania Bara kuwa watendewe haki kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania. Vinginevyo, waachiliwe huru pasipo masharti ye yote!

Mambo kama hayo ndiyo yalinisukuma kuanzisha kampeni za kuhamasisha umma wa Watanzania kuhusu umuhimu na uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
Hawa ni watuhumiwa wa ugaidi!! Zungumzia watuhumiwa wa ugaidi, siyo mashehe!!
 
Mashehe wa UAMSHO wanaingia miaka tisa - Watu hawana hata harufu ya Ugaidi ukiulizia kwanini wapo ndani na hawapaswi kutembelewa unaambiwa ,ni amri kutoka juu .sasa Juu wapi ? Mbinguni au kwa Raisi ?
Au kwa kuwa ni waislamu tu ndio mkawafanyia hivi ? Eti magaidi hivi mnawajuwa magaidi au mnawasikia tu ? Nina hakika kama hao wengekuwa magaidi basi kingekwishanuka zamani sana,kuna nchi hazijakamata hata gaidi mmoja ila mnakijua kinachotokea. Eti hawa mashee wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi ,shukuruni mmewakuta watanzania walio wengi ni watu wa ajabu si raia si majeshi.
Hawa si magaidi bali ni watuhumiwa wa ugaidi!! Acha mamlaka zinazohusika zilishughulikie jambo hili bila shinikizo. Pili hawa hawako rumande kwa ajili ya uislamu wao au kwa ajili ya ushehe wao! Wako rumande kwa ajili ya utuhumiwa wao wa ugaidi!! Walisumbua sana huko Zanzibar wakati wa rais Shein! Wako katika mikono salama!!
 
Mashehe wa UAMSHO wanaingia miaka tisa - Watu hawana hata harufu ya Ugaidi ukiulizia kwanini wapo ndani na hawapaswi kutembelewa unaambiwa ,ni amri kutoka juu .sasa Juu wapi ? Mbinguni au kwa Raisi ?
Au kwa kuwa ni waislamu tu ndio mkawafanyia hivi ? Eti magaidi hivi mnawajuwa magaidi au mnawasikia tu ? Nina hakika kama hao wengekuwa magaidi basi kingekwishanuka zamani sana,kuna nchi hazijakamata hata gaidi mmoja ila mnakijua kinachotokea. Eti hawa mashee wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi ,shukuruni mmewakuta watanzania walio wengi ni watu wa ajabu si raia si majeshi.
Hawa si magaidi bali ni watuhumiwa wa ugaidi!! Acha mamlaka zinazohusika zilishughulikie jambo hili bila shinikizo. Pili hawa hawako rumande kwa ajili ya uislamu wao au kwa ajili ya ushehe wao! Wako rumande kwa ajili ya utuhumiwa wao wa ugaidi!! Walisumbua sana huko Zanzibar wakati wa rais Shein! Wako katika mikono salama!
 
Back
Top Bottom