Tunaunga mkono kwa kauli ya RC kurudisha mabasi yote katika stendi ya Magufuli Mbezi

Ila huwezi kuruhusu kila basi kuwa na stand yake, huo ni upumbavu na kukosa dirt kama jiji. Tutembee kudogo mataifa yaliyoendelea tujifunze jamani, sio kwenda kushangaa magorofa na njia 18 za barabara.
Hakuna haja ya kupoteza pesa kwenda kutembelea huku, mtafute mtu tu anayejua Kingereza akutafsirie haya maelezo kuhusu Seoul ya Korea Kusini iliyo na ukubwa sawa na Dar👇
 
Kwa nini umetaka kuwe na stendi 3 na sio 4, 5, 6 au 10? Na kwa nini umeamua yawe na hayo maeneo tu peke yake??

Vigezo gani umetumia?
Njia kuu zinazoingia Dar, hii ikiwa ni kigezo yaweza fanya kazi. Tatizo mambo haya yanaanzia kwa viongozi wa siasa badala ya ma-engernia wa city
 
Njia kuu zinazoingia Dar, hii ikiwa ni kigezo yaweza fanya kazi. Tatizo mambo haya yanaanzia kwa viongozi wa siasa badala ya ma-engernia wa city
Wazanzibar wanaotoka Zanzibar, wakazi wa Kigamboni, Posta na Kariakoo wao wapandie na kushukia wapi kwenda au kutoka mikoani ?

Kwa nini umefikiria njia kuu zinazoingia tu Dar na hujafikiria kuhusu njia kuu zinazotoka Dar pia ambapo watu wanaishi?
 
Wazanzibar wanaotoka Zanzibar, wakazi wa Kigamboni, Posta na Kariakoo wao wapandie na kushukia wapi kwenda au kutoka mikoani ?
Wataenda stend kuu zilizopo katika hizo njia kuu, mfano kama mtu anasafiri kwenda Mtwara anaenda kupanda basi terminal pale Mbagara kando ya Kilwa road. Kama kampuni za usafirishani wanataka kupunguza usumbufu wa abiria wao hata wakianzia ofisini kwao mie sioni shida. Basi zao zipite njia ya mwendokasi kwa malipo maalum kuzifikia hizo stand kuu za mabasi
 
Kama kampuni za usafirishani wanataka kupunguza usumbufu wa abiria wao hata wakianzia ofisini kwao mie sioni shida. Basi zao zipite njia ya mwendokasi kwa malipo maalum kuzifikia hizo stand kuu za mabasi
Wenzako hawataki hivi sasa, wanataka bus zote Dar nzima safari zao zianzie na kuishia Magufuli Stendi Mbezi, wao wanaita "stendi kuu". Na kusiwepo kabisa matumizi ya Ofisi binafsi za gari kupakiza au kushusha abira. Yani kama unaishi pembeni ya office za New Force hapo Ubungo au umetoka na mzigo wako Kariakoo na unataka kwenda Mbeya usipandie hilo bus hapo Ubungo bali upande dalaladala mkakutane na bus lilitoka Ubungo Mbezi Magufuli Stendi!
 
Kwa nini umetaka kuwe na stendi 3 na sio 4, 5, 6 au 10? Na kwa nini umeamua yawe ni hayo maeneo tu peke yake??

Vigezo gani umetumia?
Tumia bongo kufikiri mkuu, hiki ni kitu very basic kwa jiografia ya Dar.
 
Hakuna haja ya kupoteza pesa kwenda kutembelea huku, mtafute mtu tu anayejua Kingereza akutafsirie haya maelezo kuhusu Seoul ya Korea Kusini iliyo na ukubwa sawa na Dar👇
View attachment 3649597View attachment 3649598View attachment 3649599
Kwani hoja yangu ya terminals zaidi ya moja hapo juu hukuiona? Lakini kujifunza ni pamoja na kupata experience za wengine. Miji mikubwa duniani inakuwa na terminals nyingi, ila sio private bus stands, kama una uelewa mdogo tu ukaenda Shekilango hadi Kagera utaona ni ukosefu wa uongozi bora, ila kama umezaliwa na kukulia mazingira yetu bila exposure hata ya kujisomea utaona ni maendeleo makubwa sana kuwa na stands za mabasi kama maduka ya mangi. Sihitaji kutafsiriwa na mtu, kama sijaelewa kuna njia nyingi za kujua nini kimeandikwa.
 
Miradi mingi ya Magufuli ilikuwa ya kulazimisha, matumizi mabaya ya pesa za umma, angalia Chato Intl. Airport, stand ya mabasu Nanenane-Dodoma ni aibu. Kupeleka Stand kuu nje ya mji ni ushamba ukizingatia Magu ni mshamba sana! Stand kuu ingeweza kuwa katikati ya jiji ikawekewa njia pana za kutosha za kuingia na kutoka ikiwepo flyovers. Msongamano wa Dsm utapungua tu km miundo mbinu ya kisasa itapelekwa mikoani na wilayani ajenda ambayo Samia hana, Samia yuko kujenga kwao, kila mwaka ni orodha ya miradi ktk kijiji chake cha Kizimkazi. Rais wa mwisho nchi hii alikuwa Kikwete hawa wengine ni wabinafsi, wabaguzi. Samia anang'ang'ania SGR mpaka Kigoma kwa kuwa anajenga njia ya Zanzibar kuja kufanya biashara na nchi za DRC, Burundi siyo kwa mapenzi mema ya kujenga nchi yetu, barabara zina hali mbaya sana bila aibu wanawekwa makandarasi eti wazawa barabara kubwa km za Moshi-Arusha watu wasio na uwezo wa pesa, teknolojia, vifaa, barabara wanamopita watalii kwa maelfu kila siku, ni taswira ya nchi yetu, ila angalia uhuni unaofanyika. Samia ni janga la Taifa letu, tumepigwa. Ile barabara ilitakiwa ijengwe njia 4 mpaka KIA tena na mkandarasi wa maana mwenye uwezo awe Mchina, Mjapan, au mzungu kutoka Ulaya, nchi sahv haina uongozi
 
kwani unafikiri mtu wa mbezi bus likipitia bagamoyo akishukia pale shekilango naye hapati usumbufu huo? sheria ifuatwe bila kuingiza siasa
 
kwani unafikiri mtu wa mbezi bus likipitia bagamoyo akishukia pale shekilango naye hapati usumbufu huo? sheria ifuatwe bila kuingiza siasa
Kwa nini apande basi la kupitia Bagamoyo wakati yapo mabasi ya kupitia Chalinze-Kibaha- Mbezi??
Nyie watu mnaoihusudu hiyo stendi Magufuli mna ubongo kama wa kuku.
 
Mkuu ndiyo maana nimesema ni 50/50.

Serikali inatakiwa itambue hilo wasijiangalie wao tu.
 
Mkuu mji umekuwa na watu ni wengi sana. Pia mabasi ni mengi sana kuliko miaka kumi iliyopita. Huwezi kulazimisha mipango ya miaka ya 80 iwepo Leo.
 
Mkuu mji umekuwa na watu ni wengi sana. Pia mabasi ni mengi sana kuliko miaka kumi iliyopita. Huwezi kulazimisha mipango ya miaka ya 80 iwepo Leo.
Duniani kote hakuna stand mitaani..
Watu wanapanda buses main bus terminal..
Kuacha mitaa ijazane mikokote na maguta ya mizigo ndy uzamani wenyewe huo..
 
Kwanini unalazimisha basi zote zipaki Mbezi?. Dar ni kubwa sana usijifungie sehemu Moja tu. Mbona Mwanza hawapigi kelele na karibia Kila basi Lina ofisi yake kuanzia Allys, Katarama, Chakany, Sama etc. Mwanza ni kubwa huwezi kulazimisha Kila basi liishie Nyegezi.
 
Waliobuni ubungo walisema ubungo ilikuwa katikati ya wilaya zote za Dar. Hiyo Magufuli ipo nje ya Dar, tukubali kukosolewa. Mkikosolewa mnadai kupingwa ndio shida yenu. Jiji la watu milioni tano unalazimisha stendi iwe Moja? Tuwe serious
 
Hukatazwi kufunguwa ofisi mitaani bali ni marufuku kupakia au kushusha abiria mitaani..

Abiria wote shusha ,au pakia mbezi Magufuli...
Shida ya ofisi mitaani haijulikani ni garage,au godown,au ofisi ya mizigo..ni fujo tupu mitaani..
Hili haikubali hata kidogo...
 
Muwe mnasafiri japo huko duniani mjifunze, nchi ya kipumbavu ndio inaruhusu "stand binafsi" ila kama mnajielewa hamuwezi kuruhusu kila mtaa kuwa na stand ya mtu binafsi.
Kila mtaa hauwezi kuwa na stendi. Ila tuangalie wepesi kwa abiria.
 
Shida mmezoea watu kuishi kwa ugumu. Kama basi linaanzia Kigamboni linapitia Mbezi shida ipo wapi?. Yani eneo la watu milioni tano unataka wawe na stendi Moja ya kupandia na kushuka ?. Tuwe serious
 
Waliobuni ubungo walisema ubungo ilikuwa katikati ya wilaya zote za Dar. Hiyo Magufuli ipo nje ya Dar, tukubali kukosolewa. Mkikosolewa mnadai kupingwa ndio shida yenu. Jiji la watu milioni tano unalazimisha stendi iwe Moja? Tuwe serious
Yale yale unazani kila mtu mwanasiasa, mara kwanza Stand ilikuwa Kisutu, kabla ya kupelekwa Ubungo? Vipi hapa napo.......

Unaposema Ubungo ni katikati ya wilaya zote za Dar sikuelewi? Unaongelea dimensionally au mazoea? Maana mwanzoni watu walizoea Stand ilikuwa Kisutu,ilivyo hamishwa Ubungo, still walilalamika kama wewe unavyo lalamikia Mbezi,ila wakazoea. So now imeamishiwa Mbezi watazoea kama ilivyokuwa Ubungo,msipende kuingiza siasa kwenye kila kitu, sijui discussion mara ziundwe kamati kupoteza mda,sometimes kinachotakiwa ni maamuzi ya mtu mmoja.
 
Nikusaidie. Zamani stendi zilikuwa tatu. Kisutu, kariakoo na

Sio kisutu tu hata Kariakoor mabasi yalikuwa yanadhusha na kupakia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…