Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aanza kukumbana na wananchi wakitaka maendeleo ya vitu

Hivi Lissu ana mpango wa kwenda kuomba kura Chato na Kigamboni? Akiffika huko atawaambia kuwa uwanja haustabili kujengwa? Na Kigamboni atawaambia daraja lao ni la kupunga upepo?
Acha upotoshaji wako wa kishetani, Lisu hajazungumzia Daraja la Kigamboni na wala hawezi kuliongelea kwani ni muhimu sana, Lisu kaongelea daraja la kutoka Aga kan kwenda Oyestarbay linalojengwa sasa chini ya utawala huu wa kidikteta, chato lazima Lisu aende na huko atawauliza umuhimu wa huo uwanja wa kutua Ndege za viongozi wa east Africa tu pasipo Abria wengine kuutumia
 

Itakuwa wewe ndiye mzito wa kuelewa sera CDM hakuna mahali ambapo inasema kufanya maendeleo ya miundo mbinu ni makosa ila mara zote wanasema maendeleo ya miundo mbinu yaende sambamba na maendeleo ya watu.

Kama serikali ina pesa ya kujenga SGR isiseme haina pesa ya kulipa nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi au pension au mikopo ya kusomesha wanafunzi au madawa katika hospitalini au huduma ya maji hivyo vyote ni vya muhimu kwakuwa kila kinachofanyika kilenge kumpunguzia mwananchi adha katika maisha yake ili aweze kulala pazuri, ale vizuri, avae vizuri atibiwe vizuri na watoto wake wapate elimu nzuri pia.

Sasa hii ya kusema mishahara haiwezi kuongezwa kwakuwa inajengwa SGR siyo sawa kwasababu mlengwa wa kwanza katika maendeleo ni mtu mwenyewe halafu mengine yafuate. Kwahiyo sioni kosa la kuhitajika barabara kwa jimbo la mdabulo. Sera ya CDM inasisitiza uhuru haki na maendeleo ya watu.

Chochote kinacholeta maendeleo ya watu kifanywe. Lakini siyo Haya maisha ya miaka mitano ya kumfanya mwananchi kuzidi kuwa masikini ashindwe hata kununua uniform ya mtoto wake aende shule kwa sababu kuna SGR inajengwa au Ndege zimenunuliwa Hiyo siyo sawasawa.
 
Unadhani hiyo pesa ya Chato na hilo daraja la baharini vingemaliza matatizo ya barabara Tanzania nzima?

Tunasema hivyo havikupaswa kuwa kipaumbele kwa sasa tena mara 100 lingejengwa daraja la magomeni hapo ambapo mvua ikinyesha barabara haipitiki kusingekuwa na kelele sasa lile daraja kule linakokwenda hata folen huwa hakuna folen huwa iko maeneo ya mwenge pale na pale salender kutokana na magari yanayotokea mwenge na kinondoni.

Magari yanayotokea kule masaki huwa hayana foleni pale muda wote huwa ni magari ya kawaida ndiyo maana kama unatoka mjini ukishapita traffic light za ubalozi wa urusi ukielekea barabara ya coco beach huwezi kuta folen kwahiyo lile daraja halikuwa kipaumbeli cha mambo muhimu ya kufanya.

Pia lingeweza kujengwa hata ile barabara ya kilwa kutoka kituo cha bandari kuunganisha majani ya chai hakuna mtu ange hoji lakini kule kwakwele ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi mimi mwenyewe naishi kinondoni lakini hilo daraja hapana halikupaswa kuwa kipaumbele.
 

Ninkweli kabisa ndiyo maana hata Nyerere aliyeanzisha wazo la kupeleka Dodoma makao makuu ya serikali hakuwahi kupeleka sababu aliona kuwa kuwaendeleza watu kwanza ndiyo kipaumbele cha muhimu zaidi

Hata marais wote watatu waliofuata waliliona hilo pia kwamba hicho siyo kipaumbele sababu tayari serikali ilikuwa na ofisi zake PAO moja na ikulu ambayo inatosha kufanya kazi za utawala.

Sasa kitendo cha kusitisha malipo ya nyongeza za mishahara ya watu malipo ya pension za wastaafu kununua madawa ya hospitalini na hata kusambaza maji na pesa kujengea majengo ya serikali Dodoma sidhani kama hicho kilikuwa ni kipaumbele kwa uchumi huu tulionao pengine muda ungefika wa kufanya hivo ila siyo sasa ambapo pesa SA kusomesha watoto wetu wa primary na secondary tunasaidiwa na wafadhiri.

Tulihitaji mjadala wa lini serikali ihamie Dodoma na mbona hilo halikuwa hata kwenye ilani ya uchaguzi ambayo ingesaidia wanainchi kuamuwa kama hiyo sera inafaa.
 
Hivi Lissu ana mpango wa kwenda kuomba kura Chato na Kigamboni? Akiffika huko atawaambia kuwa uwanja haustabili kujengwa? Na Kigamboni atawaambia daraja lao ni la kupunga upepo?

..I would not advice him to visit Chato.

..lakini kama akienda basi atafute hitaji la kweli la wananchi wa Chato.

..halafu awaulize kama kati ya hilo hitaji lao na uwanja wa ndege kipi kitakuwa faida kwao.

..daraja la coco-beach does not make sense to me, siyo priority ukilinganisha na barabara kama za Kilombero na Mlimba.
 

..mimi nitakuwa mfaidika wa daraja hilo lakini siliungi mkono.
 
Hovyo
 
Jamani hata nyerere alisema tunataka maendeleo ya vitu yanayogusa maisha ya watu, niwapi Lisu amepinga miradi ya maji na barabara ? Barabara nisehemu yamaisha yawatu wote Kila siku maji nisehemu yamaisha ya watu Kila siku,,
 
Lissu anawapa makavu live...

Ccm toka uhuru mpaka leo wananchi tunapewa ahadi za maji kweli?
 
Jamani hata nyerere alisema tunataka maendeleo ya vitu yanayogusa maisha ya watu, niwapi Lisu amepinga miradi ya maji na barabara ? Barabara nisehemu yamaisha yawatu wote Kila siku maji nisehemu yamaisha ya watu Kila siku,,
Wanamlisha maneno ili wapate unafuu, lakin hizi sio nyakati za giza kila mtu anajua ukweli
 
Lissu anawapa makavu live...

Ccm toka uhuru mpaka leo wananchi tunapewa ahadi za maji kweli?

Bora CCM inatoa ahadi za maji. CHADEMA haina ahadi ya kutoa. Inahamasisha nchi kufanya vurugu tu. Pamoja na madhaifu ya CCM lakini kuna unafuu kuliko CHADEMA. Wanayoyasema hawayafanyi ndani ya chama. Hawana rekodi ya utendaji iliyotukuka. Bado wanatakiwa wajisahihishe sana ili watupe imani. Sasa hivi CHADEMA ni kama SACCOS ya Wizi mtupu.
 

Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako ambao hawakukupeleka shule
 
We unafikiri ccm bila Dola kuna lolote hapo..??!

Chadema bila wasanii umeiona??.. Hujasikia Sera za Lissu?
 
Eti bwana,kienyeji sana aisee....kwamba ....Nakunyima hiki,nitengeneze kile...!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geita yote hakuna Chuo Cha Ufundi Stadi,enzi.na.enzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We unafikiri ccm bila Dola kuna lolote hapo..??!

Chadema bila wasanii umeiona??.. Hujasikia Sera za Lissu?

SERA ZA LISSU NIMEZISIKIA. NI KUTUKANA, KUPIGWA RISASI NA KUCHANGISHA WANANCHI FEDHA ZA KAMPENI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…